GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

3. YESU ABATIZWA 3:13-17


Historia: Wanaume wawili ambao umri wao ulikadiriwa miaka thelathini walikutana kando ya mto Yordani.Walikuwa ni binamu.Mmoja wao alikuwa amevaa mavazi ya ajabu.Kwa muda huo Yesu alikuwa anaishi Galilaya,John katika jangwa la Yuda.Haijaelezwa kama watu hao walishakutana hapo kabla.(Kiongozi anaweza kufafanua kwa ufupi kama ilivyoandikwa 3:13-17)
1. Kulikuwa na tofauti gani ukilinganisha maisha ya watu hawa wawili utotoni na ukubwani?
  • Unafikiria ni lini Yohana alielewa kwamba Yesu ni mwana wa Mungu?
  • Kwa nini umaarufu haukumharibu Yohana?
    2.Kulikuwa na tofauti gani kati ya Yesu na watu wengine waliotaka kubatizwa?
  • Kwanini Yohana hakutaka kumbatiza Yesu?
  • Kwanini Yesu alitaka kubatizwa ijapokuwa ubatizo ulikuwa kwa wenye dhambi?
    3.Neno la Mungu katika mstari wa 15 unamaanisha nini?
  • Msomaji anatkiwa kusoma Yohana 19.30.Yesu alitimizaje haki kwa wamwaminio?
    4.Kifungu hiki kinatuambia nini kuhusu uhusiano kati ya Yesu na Mungu?
  • Kifungu hiki kinatueleza nini kuhusu utatu?
  • Roho mtakatifu alikuwa katika Yesu wakati wote.Kwanini hakuonekana baada ya Yesu akibatizwa?
    5.Kwanini Mungu alitaka kuelezea watu wote mambo aliyoyasema katika mstari wa 17?
  • Fikiria kilichokutokea mwezi uliopita.Je unafikiri Mungu angeweza kusema kitu gani kwako kama alivyosema kuhusu Yesu kwenye mstari wa 17?
    6.Yohana alibatiza watu tu pale walipokiri kutenda dhambi,ndiyo maana ubatizo wake uliitwa ubatizo wa toba.Kuna tofauti gani kati ya ubatizo wa Kikristo na ubatizo wa Yuda? (Angalia pia Matendo 2:38)
    7.Wakati wa ubatizo wa Kikristo Mungu aliwaambia waliobatizwa maneno yaleyale aliyomwambia mwanaye(17) Kwa misingi ipi anaweza kuyasema haya kwa wakosao?
    8.Kiongozi anatakiwa kuelezea jinsi Ibrahimu alivyomtoa mwanawe kwa Mungu(Mwanzo 22).Maneno katika mstari wa 17 bila kufafanua yanakumbusha maneno ambayo Mungu alimwambia

    Ibrahimu(Mwanzo 22:2) Kuna siri gani kati ya Mungu na Ibrahimu inayopelekea Ibrahimu kutoa sadaka wanawe?
















    ***

    Version for printing    
    Downloads    
    Contact us    
    Webmaster