GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

2. YESU ANAKUTANA NA MTU ALIYEPOOZA (Mk 2:1 - 12)



TAARIFA MUHIMU: Nyakati za Yesu, nyumba zilijengwa kwa mawe ya chokaa na vigae na zilikuwa na mapaa bapa. Kulikuwa na ngazi nje ya nyumba zilizoelekea paani. Kawaida, mtu hupooza akiwa na umri wa makamu au zaidi kwa sababu ya utokaji wa damu katika ubongo. Mtu aliyepooza hawezi kutembea wala kuongea. Mwana wa Adamu ni jina alilolitumia Yesu alipojizungumzia mwenyewe.

1. Unafikiri mtu anaweza kufurahi iwapo amelala kitandani mwake akiwa haongei wala hatembei?

  • Ni malezi ya aina gani aliyoyahitaji mtu huyu katika maisha yake ya kila siku?

  • Yafikirie maisha ya kila siku ya mlezi wa mtu huyu?

    2. Wayahudi wote walimwamini Mungu nyakati hizo. Mtu huyu alifikiria nini kuhusu Mungu na imani baada ya kupooza?

    3. Katika aya ya 5 tunaweza kuona kuwa mtu huyu alikuwa na dhambi katika dhamiri yake.

    Ni dhambi za aina gani ambazo mtu anaweza kuzifanya anapokuwa hawezi kutembea au kuongea?

  • Kwa maoni yako: je, uchungu na ugonjwa vinaweza kutubadilisha ili tuwe binadamu wema au tuwe binadamu wabaya zaidi?

    4. Shida ya kumsafirisha mtu aliyepooza kwa blanketi kupitia mjini ni ipi?

  • Kwa nini watu wengine hawakutoka nje ya nyumba ili wamruhusu huyu mtu maskini apelekwe kwa Yesu (4)?

  • Kwa nini marafiki zake wanne hawakurudi nyumbani baada ya kugundua kuwa ilikuwa vigumu kwao kuingia kupitia mlangoni?

    5. Watu hawa wanne walikuwa na uhusiano upi na mtu huyu aliyepooza? Fikiria uwezekano mbali mbali (3).

  • Ni hadhari zipi zilizochukuliwa mtu huyu alipopelekwa juu ya paani? (Itazame taarifa muhimu kuhusu jinsi nyumba ilivyojengwa).

  • Ni vifaa gani vilivyohitajika ili kuweza kulivunja paa la nyumba? Watu hawa wanne walivipata wapi?

  • Ni maoni yapi yaliyosikika kutoka chumbani kutoka paa la nyumba lilipokuwa linavunjwa?

    6. Wanaume wanne walikuwa wamemleta rafiki yao kwa Yesu ili aweze kuponywa. Kwa nini Yesu alimsamehe dhambi zake kwanza (5)?

  • Kwa nini Yesu aliufuata utaratibu huu: kwanza kusamehe dhambi halafu kuuponya ugonjwa?

  • Ilimaanisha nini kwa mtu huyu aliyepooza kwamba alisamehewa dhambi zake zote alizokuwa amezifanya hapo awali?

    7. Ifikirie hali ambayo unamwendea Yesu na kumwuliza akusuluhishie shida yako kubwa zaidi. Iwapo atakujibu: "Mwanangu/binti yangu, dhambi zako zimesamehewa." Je utafurahi au utahuzunika?

  • Iwapo ungeweza kuchagua, ungechagua nini: dhamiri nzuri au suluhisho la shida yako kubwa zaidi?

  • Mtazamo wa mtu aliyepooza ulibadilikaje kuhusu ugonjwa wake alipogundua kuwa angeenda mbinguni mwishowe?

    8. Katika aya ya 5, Yesu hazungumzii kuhusu imani ya mtu aliyepooza bali ile ya marafiki zake. Ni wazi kuwa mtu huyu mwenyewe hakuwa na imani yoyote kabla ya kukutana na Yesu. Itaje aya ambapo unafikiri kuwa alianza kumwamini Yesu.

  • Kwa nini walimu wa sheria hawakuamini kuwa Yesu angeweza kuwasamehe watu dhambi zao (7 - 8)?

    9. Yajibu maswali ambayo Yesu anayauliza katika aya ya 9.

  • Ilimgharimu nini Yesu kumtibu mgonjwa huyu? Ilimgharimu nini kumsamehe dhambi zake?
  • Ungefikiria nini kuhusu Yesu kama ungekuwa umeshuhudia kwa macho yako yale yanayoelezewa katika aya ya 10-12?

    10. MASWALI YA HABARI NJEMA: Iwapo moyo wako unakushtaki kwa kosa ulilolitenda, sikiliza akwambiayo Yesu: "Mwanangu/binti yangu, dhambi zako zimesamehewa!" Ili kuigharamia ahadi yake, ilimpasa Yesu afe msalabani. Ahadi yake ina maana gani kwako leo? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

  • (Kwa kila mshiriki kujibu): Ni jambo gani muhimu zaidi ulilojifunza kutokana na haya mafundisho?

    ***

    Version for printing    
    Downloads    
    Contact us    
    Webmaster