GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

4. YESU ANAKUTANA NA TAJIRI (Mk 10:17 - 27)TAARIFA MUHIMU: Tawasifu zingine za Yesu zinatuambia kuwa azungumziwaye katika kifungu hiki alikuwa kijana na bado alikuwa mbunge (mjumbe wa baraza kuu). (Mt 19:22 na Lk 18:18). Mtu huyu alijua kutoka Biblia kuwa baada ya kifo chake angeurithi uzima wa milele au angeingia jahanamu. Kumbuka kuwa katika desturi za jamii hii, mwanaume hakumkimbilia au hakumpigia magoti mwanaume mwenzake.

1.Unafikiriaje: mwanadamu anaweza kuwa na furaha bila kujua kitakachotendeka kwake baada ya kifo chake?

 • Ni nini kilichomfanya huyu kijana mbunge kuzionyesha tabia hizi zisizokuwa za kawaida za kumkimbilia na kumpigia magoti Yesu (17)?
 • Je, mtu huyu alimchukulia Yesu kama Mungu au kama mtu mwenye busara isiyokuwa ya kawaida (17b - 18)?

  2. Kwa nini mtu huyu hakuwa na hakika dhidi ya wokovu wake ingawa alikuwa amezitunza Amri za Mungu maishani mwake?

 • Kwa nini daima hatuna hakika ya kwenda mbinguni baada ya kifo chetu?

 • Unafikiri mtu anaweza kuwa na hakika ya kwenda mbinguni baada ya kifo chake? Zitoe sababu zako.

  3. Ni amri ipi iliyo ngumu kuiweka ambayo Yesu anaitaja hapa (19)?

 • Wanasiasa wengi hujaribiwa kuwa fisadi katika mambo ya pesa na ngono. Mtu huyu aliwezaje kuhepukana na majaribu haya yote (20)?

 • Kumbuka kwamba kulingana na Yesu, amri hizi lazima ziwekwe sio tu kwa matendo bali pia kwa maneno na mawazo. Je, unafikiri kijana huyu alifaulu kufanya hivyo (19 - 20)?

 • Kwa kweli ungeyasema maneno sawa na yale aliyoyasema kijana huyu katika aya ya 20?

  4. Kijana huyu mwanasiasa alipungukiwa kitu kimoja. Ifupishe aya ya 21 na useme kitu alichokuwa amepungukiwa.
  5. Yesu anaitaja hazina ya mbinguni katika aya ya 21. Mtu anawezaje kujiwekea hazina mbinguni?

 • Kuna tofauti gani kati ya hazina ya mbinguni na hazina ya ulimwenguni?

 • Ni vitu gani ambavyo vijana wa nyakati hizi zetu wanavitukuza kama "hazina" yenye thamani kubwa zaidi?

 • Ni nani au ni nini hazina yako nzuri kuliko zote? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

  6. Labda kijana huyu alikuwa na familia au wazazi wazee ambao aliowatunza. Ni nini kingetokea kama angekuwa amemfuata Yesu katika aya ya 21?

 • Jifikirie mwenyewe kuwa katika hali aliyokuwa nayo kijana mwanasiasa huyu. Ungeamini kuwa Mungu angeweza kuitunza familia yako hata baada ya wewe kuiacha nyumba yako na mali zako zote?

 • Je, unaweza kufikiria kuziacha hazina zako za ulimwenguni iwapo kufanya hivyo kungekuwezesha kwenda mbinguni? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

  7. Kulingana na aya ya 21, Yesu alimpenda huyu kijana mwanasiasa. Kwa nini basi aliyasema maneno hayo magumu yaliyomfanya aondoke?

  8. Baada ya kugundua kuwa hasingaliweza kuyatimiza yale Yesu alimtaka ayafanye, ni nini kingine ambacho mtu huyu angekifanya kuliko kumwacha Yesu (22)?

 • Labda Yesu angeweza kujibu nini kama mtu huyu angeungama kwake: "Nisamehe kwa kupenda mali kuliko wewe!"
  9. Yafikirie maisha ya kijana huyu kuanzia sasa na kuendelea: Alikuwa na furaha? Alifikiria nini kuhusu kifo chake?

 • Lilinganishe jibu ambalo Yesu alimpa kijana huyu na jibu alilompa Petero (aya ya 21 na 27). Je, kimsingi jibu lake lililingana au lilikuwa tofauti?

 • Ni nani atakayekwenda mbinguni baada ya kifo chake?


  10. MASWALI YA HABARI NJEMA: "Kwake Mungu mambo yote yanawezekana" ina maana kuwa: Yesu aliiacha hazina yake mbinguni na akaja humu ulimwenguni kuteswa na kufa ili uweze kukipata kibali cha kuingilia mbinguni. Kosa kubwa alilolifanya kijana huyu ni kumwacha Yesu. Je wewe utafanya nini? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

 • (Kwa kila mshirika kujibu): Ni jambo gani muhimu sana ulilojifunza kutokana na mafundisho ya kifungu hiki wakati huu?

  ***
  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster