GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

7. MAFUNDISHO ZAIDI YA YESU: JIRANI YANGU NI NANI? (Lk 10:25 - 37)TAARIFA MUHIMU: Barabara iliyopitia mlimani kati ya Yerusalemu na Yeriko ilikuwa ya umbali wa kilomita 30 na ilikuwa hatari sana kwa sababu ya majambazi wa barabara kuu waliowavizia wasafiri. Maana ya Mlawi ni mtu aliyefanya kazi hekaluni kama mhudumu wa ofisi. Nyakati za Yesu, Wayahudi walichukiana sana na Wasamaria walioishi katika nchi moja nao. (Uchukue mfano kutoka katika nchi yako. KENYA: Ni rahisi kuuelewa mfano huu iwapo unafikiria kuwa watu wengine wote katika hadithi hii ni Wakenya isipokuwa Msamaria - ni mfuasi wa "Mungiki". UGANDA: Ni rahisi kuuelewa mfano huu iwapo unafikiria kuwa watu wengine wote katika hadithi hii ni Waganda isipokuwa Msamaria - ni mfuasi wa Yusufu Kony wa Jeshi la upiinzani la Bwana"LRA".)

1. Mtu anaweza kufurahi iwapo hajali kabisa jinsi wenzake watesekavyo lakini anajifikiria tu mwenyewe na familia yake?

 • Ni mara ngapi unazitoa pesa zako kwa ajili ya kuwasaidia wenye haja?

  2. Katika mafundisho yetu yaliyotangulia, tulijifunza kuhusu mwanasiasa mmoja aliyemuuliza Yesu swali sawa na aliloliuliza mwalimu wa sheria katika hiki kifungu. Njia ya kwendea mbinguni ni ipi kulingana na anachokisema Yesu katika hiki kifungu (25 - 27)?

 • Uwezekano wako wa kwenda mbinguni ni upi iwapo masharti ni yale anaoatoa Yesu katika aya ya 27?

  3. Yesu anautoa mfano wa mtu aliyepigwa na genge la majambazi na akaachwa akiwa mahututi. Yafikirie mawazo ya majeruhi huyu alipokuwa amelala kando ya barabara saa baada ya saa (30).
 • Je, mke na watoto wake walikuwa wakifikiria nini wakati hakuwasili nyumbani mda ule aliokuwa amewaahidi?

  4. Kulikuwa na hatari gani kwa wapita njia kumsaidia majeruhi huyu?

 • Kuhani na Mlawi walikuwa njiani kwenda kuutekeleza wajibu wao wa kidini hekaluni. Unafikiri watu hawa wawili wangefanya nini iwapo majeruhi angekuwa mtoto wao wenyewe?
 • Zifikirie sababu nyingi uwezavyo zilizowafanya hawa watu wawili kukataa kumsaidia mwathiriwa wa uhalifu huu (31 - 32).

 • Unafikiria mwenywe ungefanya nini iwapo ungempata mtu akiwa katika hali hiyo?

  5. Je, Kuhani na Mlawi waliifafanuaje amri ya upendo waliyokuwa wamefundishwa tangu walipokuwa watoto? Utazame aya ya 27.

 • Ungefikiria nini kuhusu mtu aliyesema hivi: "Ninampenda Mungu kwa moyo wangu wote lakini kwa bahati mbaya sina nafasi ya kuwasaidia watu wengine."

  6. Iwapo Msamaria angepita na ampate Myahudi majeruhi, angeziteteaje tabia zake? Itazame taarifa muhimu.

 • Ni jinsi gani ambavyo Msamaria alifanya zaidi ya kile ambacho yeyote angekitarajia katika hali hii (33 - 35)?

  7. Dinari mbili zilikuwa sawa na mshahara wa kazi za siku mbili, kumaanisha sehemu moja kwa kumi na tatu ya wastani ya mshahara wa mwezi mmoja. Kwa kiasi hicho cha pesa, mtu angeishi hotelini kwa miezi miwili. Dinari mbili zingekuwa sawa na pesa ngapi katika sarafu zetu?

 • Zifikirie sababu mbalimbali zilizomfanya Msamaria akitoe kiasi hicho cha pesa kwa mtu asiyemjua (35).
 • Kwa maoni yako, ni asilimia ngapi ya amri ya upendo aliyoitimiza Msamaria huyu msafiri? Itazame aya ya 27.

  8. Yesu alimaanisha nini juu ya jirani?

 • Ni majirani wapi wa karibu na wa mbali unaopaswa kuwasaidia?

  9. Ungeulizwa kuichagua nafasi katika mfano huu, ni nafasi ipi ambayo ingekufaa zaidi: ya majeruhi, jambazi wa barabara kuu, kuhani, Mlawi au mwenye hoteli? Zitoe sababu zako za kuichagua nafasi hiyo.

 • Ni kwa njia zipi Yesu anafanana na Msamaria katika mfano huu?
 • Yesu anamfananaje Myahudi majeruhi?
 • Yesu aliitayarisha njia nyingine ya kwendea mbinguni isipokuwa ile inayoelezewa katika aya ya 27. Ni njia ipi hiyo?

  10. MASWALI YA HABARI NJEMA: "Nenda ukafanye vivyo hivyo", Yesu akasema - na akaenda na akafanya hivyo mwenyewe. Hata kama watu wote wamekupita bila kuzijali huzuni zako, hawezi kufanya hivyo. Sasa anasimama karibu nawe na anataka kuvifunga vidonda vya moyo wako. Unamjibu nini? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

 • (Kwa kila mshiriki kujibu): Ni jambo gani muhimu zaidi ulilojifunza kutokana na haya Mafundisho ya Biblia?

  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster