GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

9. MWANAMKE ALIYETOKWA DAMU (Mk 5:25 - 34)TAARIFA MUHIMU: Kulingana na Sheria za Musa za kidini, mwanamke alichukuliwa kuwa mchafu wakati wake wa hedhi. Hakuna aliyeruhusiwa kumgusa au kukigusa chochote alichokuwa amekigusa. Aidha hakuruhusiwa kuingia hekaluni akiwa katika hali hiyo (Walawi 15). (KUMBUKA: Ukihisi kuwa ugonjwa kama huu hauwezi kujadiliwa katika jamii yako, unaweza kukiacha kifungu hiki na uendelee na vingine.)

1. Labda mwanamke huyu alikuwa na miaka thelathini au arobaini na alianza kuwa mgonjwa akiwa na umri mdogo kabisa. Ugonjwa huu ulikuwa na matokeo gani katika maisha yake ya kijamii (25)? (Ulikuwa na matokeo gani kama alikuwa ameolewa/alikuwa hajaolewa?

 • Utokwaji na damu ulikuwa na matokeo gani katika hali yake ya kimwili?
 • Ugonjwa kama huo huwa na athari gani katika kujistahi kwa mtu?

  2. Mwanamke huyu alifikiria nini kuhusu Mungu baada ya kuupata ugonjwa kama huu katika miaka yake ya ujana?
 • Uhusiano wake na Mungu ulibadilikaje wakati wa ugonjwa wake wa miaka mingi?

  3. Katika aya ya 26, inasemekana kuwa mwanamke huyu alikuwa tajiri hapo awali. Zifikirie njia mbalimbali zilizompatia pesa na kwanza zilikusudiwa kwa nini.

  4. Tunaweza kufikiria kuwa matabibu (wanajinakolojia) wa nyakati hizo hawakuwa mabingwa sana. Kwa nini ilikuwa muhimu kwake kuwa tayari kuyapata matibabu kama hayo na hata kuzitumia pesa zake zote kwa "madaktari" kama hao (26)?

 • Mwanamke huyu alihisije kuhusu madaktari na waponyaji wa kila aina wakati huu wa maisha yake (26 - 28)?

  5. Je, inawezekanaje kuwa mwanamke huyu aliyekuwa amevunjwa moyo na waponyaji wengine alikuwa na hakika kuwa kuigusa tu nguo ya Yesu kungemponya (27 - 28)?

 • Una hakika kama mwanamke huyu kuwa Yesu anaweza kuzitatua shida zako mbaya zaidi? Kwa nini? Kwa nini huna uhakika?

  6. Kwa nini mwanamke huyu hakumuuliza Yesu msaada jinsi wagonjwa wengine walivyofanya (28 - 29)?

 • Kwa nini mwanamke huyu alikuchagua kugusa kama njia ya kumponya?

  7. Yesu angewezaje kujua kwa uangalifu kuwa mtu fulani ameigusa nguo yake (30 - 31)?
 • Kwa nini Yesu hakumwacha mwanamke huyu aende nyumbani bila kuzungumza naye (30 -32)?

  8. Unafikiri mwanamke huyu alihisije alipolisikia swali la Yesu katika aya ya 30?
 • Mwanamke huyu alikiona nini machoni mwa Yesu wakati Yesu aligeuka na kumwangalia usoni moja kwa moja (32)?

  9. Mwanamke huyu hakutarajia kulisema hata neno moja kwa Yesu na baadaye aliishia kumwambia hadithi nzima. Unafikiri alimwambia nini kwa kweli (33)?

 • Je, umewahi kumwambia Yesu ukweli mtupu kuhusu maisha yako kwa maneno mengi sana?

  10. Aya ya 34 unaweza kutafsiriwa kwa njia mbili: "Imani yako imekuponya." Au: "Imani yako imekuokoa." Kwa nini Yesu alitaka kuyasema maneno haya hasa kwa mwanamke huyu?
 • Kwa nini Yesu alimwita mwanamke huyu bintiye ingawa labda walikaribiana katika umri (34)?

  11. HABARI NJEMA: Yesu pia alikuwa mchafu kidini damu yake ilipomwagika alipochapwa mijeledi na aliposulubiwa. Kila mmoja aliyemgusa alikuwa mchafu. Hii ndiyo gharama aliyoilipa Yesu kwa kumwokoa huyu mwanamke - na kwa kukuokoa wewe!

  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster