GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

12. KILIO CHA KIPOFU MWOMBAJI (Mk 10:46 - 52)TAARIFA MUHIMU: Tunavyofahamu, Yesu alitembelea Yeriko mara moja tu. Alifanya hivyo wakati wa safari yake ya mwisho ya kwenda Yerusalemu. Yesu alikuwa wa kizazi cha Daudi moja kwa moja. Mungu alikuwa amemwaahidi mfalme huyu kuwa mwanawe angekikalia kiti cha enzi cha Israeli milele (2 Sam 7:12 - 16). Warumi waliokuwa wanaitawala nchi hiyo nyakati hizo, hawakumvumilia yeyote aliyewataja wafalme waliopita na waliokuwepo. Yesu alizungumziwa kama mwana wa Daudi mara moja tu kabla ya tukio hili na aliyefanya hivyo wakati huo alikuwa mgeni (Mt 15:22).

1. Ni nini kingekuwa kigumu sana kwako iwapo ungekuwa unajipatia riziki ya kila siku kwa uombaji?
 • Furaha na huzuni za kila siku za kipofu huyu mwombaji zilikuwa zipi?

  2. Hata kipofu anaweza kujifunza nini anapokuwa ameketi kando ya barabara kila mwaka iwapo ana masikio mazuri?
 • Wakati wa miaka mitatu ya mahubiri ya hadharani ya Yesu, Bartimayo alisikia jinsi alivyokuwa anatembelea sehemu zingine. Kwa nini hakuyataka matibabu, kwa mfano, mji wa Yerusalemu ulikuwa na umbali wa kilomita 30 mahali Yesu alienda kila mara nyakati za sikukuu za kidini?

  3. Bartimayo alishindwa kufanya nini Yesu alipofika katika mji wake hatimaye (46)?
 • Ni mpango gani Bartimayo alikuwa nao tayari wa kuwasiliana na Yesu wakati angekuja Yeriko mwishowe?

  4. Bartimayo angewezaje kujua kuwa Yesu alikuwa mwana wa Mfalme Daudi (47)?
 • Kwa nini Bartimayo hakuwaogopa Warumi bali alimsalimia Yesu kama mwana wa mfalme atakayerithi ufalme au mfalme kwa sauti ya juu sana (47)?

  5. Kwa nini watu walijaribu kumnyamazisha Bartimayo? Yatafute majibu mengi uwezavyo (48).
 • Kwa nini yeyote hakumshika Bartimayo mkono na kumwongoza hadi kwa Yesu (48)?

  6. Ni vipi na kwa nini Bartimayo alikibadilisha kilio chake? Ilinganishe kwa makini aya ya 47 na ya 48.
 • Yesu alizionyesha hisia gani kwa cheo cha mfalme (49 - 51)?

  7. Unafikiri Bartimayo alihisi vipi watu walipomwambia kuwa Yesu alikuwa anamwita (49 - 50)?
 • Labda Bartimayo alikuwa amelitunza vizuri joho lake lililokuwa godoro na tandiko lake usiku. Kwa nini hakulitupa ghafla (50)?

  8. Kwa nini Yesu alimwuliza Bartimayo swali wazi kama hilo (51)?
 • Yesu anakuuliza swali lilo hilo sasa (51). Tafakali mjibu kwa uaminifu. (Unaweza kufanya hivyo kimoyomoyo.)

  9. Yesu aliyaponyaje macho ya huyu mtu (52)?
 • Aya ya 52 inaweza kutafsiriwa kwa njia mbili:"Imani yako imekuponya" au "Imani yako imekuokoa." Kwa nini Yesu alitaka kuyasema maneno haya kwa Bartimayo katika hali hii?

  10. Bartimayo alimfuata Yesu barabarani labda hadi Yerusalemu (52b). Siku iliyofuatia, kila mtu alikuwa akimwamkua Yesu kama "mwana wa Daudi" alipokuwa anaingia mjini (Mk 11:9 - 10). Wajibu wa Bartimayo ulikuwa upi katika yote haya?
 • Baada ya wiki tu, Bartimayo alimshuhudia mfadhili wake akisulubiwa msalabani. Unafikiri alifahamu nini kuhusu kilichomfanya Yesu afe?

  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster