GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

15. YESU ANAKUTANA NA WAHALIFU WAWILI (Lk 23:32 - 43)TAARIFA MUHIMU: Katika Himaya ya Kirumi kusulubiwa kulitumika tu kwa uhalifu mbaya zaidi. Basi tunaweza kuchukulia kuwa watu hawa wawili walikuwa wahalifu wajuzi ambao labda walikuwa wamewaua watu kwa sababu ya pesa. (Masiha au Kristo) kilikuwa cheo cha mfalme aliyengojewa na Wayahudi tangu nyakati za Agano la Kale.

1. Mtu anayewapiga wengine kwa ngumi au kwa ulimi wake anaweza kuwa na furaha?
 • Kwa nini vijana wengi wa nyakati hizi zetu hukimbilia vurugu na hufurahia kuwafanyia ghasia wengine?

  2. Zifikirie sababu mbalimbali zilizowafanya hawa watu wawili wakimbilie vurugu katika ujana wao.
 • Labda ni nani angeweza kuwakomesha hawa wawili kabla ya wao kuwa wabaya kupindukia?
 • Daima unaweza kuzibadilisha tabia zako unapofahamu kuwa zinakudhuru wewe na wengine?
  3. Wahalifu hawa wawili wangezichunguza tabia za Yesu kutokana na kukaribiana naye kuliko mtu mwingine yeyote. Ni maneno na matendo yapi yaliyoweza kuwashangaza zaidi (34 - 38)?
 • Kwa nini Yesu alitaka kuwatetea wale waliomtesa mbele ya Baba yake wa mbinguni (34)?
 • Unaweza kumwombea adui mbaya kuliko wote: "Mungu, msamehe. Hakujua ni vipi alivyonitendea vibaya" (34).

  4. Tafuta kutoka aya kwa nini umati, watawala, wanajeshi wa Kirumi na mmoja wa wahalifu walimpigia Yesu ukelele (34b - 39).
 • Hawa watu walimdhihaki Yesu kwa sababu gani (35 - 39)?
 • Kwa nini mmoja wa marafiki zake Yesu hakumtetea?
 • Je, ungesema na ungefanya nini kama ungekuwa unasimama chini ya msalaba?

  5. Ni nini kilichomfanya mmoja wa wahalifu kulifikia hitimisho kuwa Yesu alikuwa mfalme na alikuwa na ufalme wake mwenyewe (37 - 38, 42)?

 • Mlinganishe Yesu msalabani na wafalme wengine wa ulimwengu huu. Kuna tofauti zipi za kuvutia zaidi kati yao?

 • Ni nini kilichomfanya mmoja wa wahalifu ahitimishe kuwa Yesu hakuwa tu mfalme bali alikuwa Mungu pia (40 - 41)?

  6. Wahalifu wengi hawakubali kabisa kuwa walikuwa wameyatenda maovu yoyote. Ni nini kilichomfanya mmoja wa wahalifu akubali kuwa hukumu ya kifo ilikuwa adhabu halali kwa uhalifu wake (41)?

 • Kwa nini mhalifu yule mwingine hakuikubali hatia yake hata katika hali hii?
 • Ni nani kati ya hawa wahalifu wawili unayemwelewa vyema: yule aliyeikubali hatia yake au yule aliyeikana?

  7. Aya ya 42 ina ombi fupi sana: "Unikumbuke!" Kwa nini ni muhimu kwetu binadamu kuwa mtu fulani tunayempenda anatukumbuka tunapokuwa matesoni?
 • Kwa nini mhalifu huyu hakuuliza moja kwa moja aruhusiwe kuuingia ufalme wa Yesu?

  8. Mhalifu huyu alikuwa amefikiria nini alipolisikia jibu laYesu (43)?
 • Kwa nini Yesu alimruhusu mwuaji katili kuingia Paradiso (mbinguni)?
 • Ni wakati upi, kulingana na maoni yako, ambapo mhalifu huyu alianza kumwamini Yesu? Taja aya.

  9. Zifikirie saa za mwisho za mhalifu aliyekuwa muumini wa Yesu. Alikuwa mwenye furaha au alikuwa mwenye huzuni saa hizo?

 • Labda mamake, mkewe au mtoto wa aliyekuwa mhalifu alikuwa anasimama chini ya msalaba. Ni kumbukumbu ipi aliyoiacha kwa familia yake?
 • Ni ushuhuda upi aliouacha mhalifu huyu kwa vizazi vijavyo vitakavyozisoma habari zake katika Biblia?

  10. HABARI NJEMA: Milango ya Paradiso ilifunguliwa mbele ya mhalifu lakini badala yake ilimpasa Yesu mwenyewe kuiingia kupitia milango ya jahanamu. Unataka kuliomba ombi sawa na la mhalifu huyu? "Yesu, unikumbuke!" Kama unaweza, atakupa jibu sawa: "Siku moja utakuwa nami Paradiso." (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)
 • (Kwa kila mwana kikundi kujibu): Ni jambo gani muhimu zaidi ulilojifunza katika haya Mafundisho ya Biblia?
  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster