GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

16. KUFUFUKA KUSIKOAMINIKA (Mk 16:1 - 8)


TAARIFA MUHIMU: Kulingana na desturi za kale, Marko alikuwa mkalimani wa Petero; na injili yake ilihusu maisha ya Yesu jinsi yalivyoonekana machoni pa Petero. Mojawapo ya dhamira katika injili hii ni ukosefu wa imani ya mwanafunzi huyu. Ingawa Yesu alikuwa amekitabiri kifo na ufufuo wake mara tatu tayari, wanafunzi wake walikuwa wazito sana kumwamini. Kumbuka kuwa mwili wa Yesu ulikuwa umepakwa mafuta tayari siku ile aliyokufa.

1. Kwa nini wanawake kutoka Galilaya walisisitiza kulitembelea kaburi licha ya jiwe na askari ambao (kulingana na Mathayo) walikuwa wakilichunga kaburi (1 - 3)?

2. Tayari wanawake walikuwa wameshuhudia mwili wa Yesu ulioshughulikiwa vibaya ukipakwa mafuta siku mbili zilizotangulia. Kwa nini unafikiri walitaka kuupaka mafuta tena?
  • Unafikiri ungependa kuuona na kuugusa mwili wa mpendwa wako katika hali hiyo?
  • Ni Yohana tu aliyeshuhudia kifo cha Yesu; wengine walikuwa wametoweka kutoka mahali hapo. Kwa nini hawakuja sasa kulitembelea kaburi la Bwana wao? (Unafikiri kuna tofauti kati ya wanawake na wanaume kuhusu tukio hili? Kama ipo, tofauti ni ipi?)

    3. Iwapo wanawake waliamini katika ufufuo kulingana na utabiri wa Yesu, unafikiri wangetendaje Jumapili hiyo asubuhi (1 - 4)?

    4. Wanawake walifikiria nini walipoyasikia maneno ya malaika (6 - 7)?
  • Ni nini kilichowaogofya sana wanawake (8)?

    5. Kwa nini Yesu aliwachagua wanawake kuwa mashahidi wa ufufuo wake licha ya kuwa hawakukubaliwa kuwa mashahidi katika mahakama wakati huo (7, 10)?

    6. Ni vipi na ni lini imani ya ufufuo wa Yesu ilianza mioyoni mwa wanawake hawa?

    7. Petero alimkana Bwana wake siku mbili zilizokuwa zimetangulia. Ilimaanisha nini kwake Yesu alipomtumia salamu maalumu (7)?

    8. Kuna chochote maishani mwako kinachoonekana kutowezekana kwako kama maiti kufufuka tena? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

  • Ungejibu nini kama Yesu angekukemea kwa kuikosa imani jinsi alivyowakemea wanafunzi wake katika aya ya 14?

    9. Kuna tofauti gani baina ya ufufuo wa mwili (unaofundishwa tu katika imani ya Kikristo) na kuishi milele kwa roho (ambako ni imani ya kawaida katika dini nyingi)?

    10. Kama ufufuo wa mwili haungekuwepo, Ukristo ungewapa nini wanadamu?
  • Chukulia kwamba mtu fulani aliyaamini mafundisho yote ya Kikristo isipokuwa ufufuo wa mwili. Kwa nini hatungemwita Mkristo?

    11. HABARI NJEMA: Hatimaye wanafunzi walipothibitisha kuwa kweli Yesu alikuwa amefufuka kimwili kutoka kwa wafu, waliwaendea mashahidi wake thabiti. Wengi wao walikufa kama wafiadini wakikataa kuiacha imani yao kwa vyovyote vile. Walijua kuwa Yesu angekuwa nao milele katika ulimwengu huu na ule ujao.

    ***

    Version for printing    
    Downloads    
    Contact us    
    Webmaster