GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

3. MTEGO ULIOANDALIWA KWA YESU (Mark 3:1-6 )


Historia: Ugomvi wa kwanza wa Yesu ulihusu siku ya mapumziko (siku ya Sabato) kwa walimu katika Agano la Kale ilivyoelezwa katika sura iliyotangulia (Mk 2: 23-28). Ugomvi huu ulikuwa ni wa pili katika utaratibu. Kwa walimu maadhimisho ya kimila katika Sabato yalimaanisha utambuzi wa mambo mawili: 1) kuja kwa Masihi, Mwokozi baadaye, Yesu na 2) ukombozi wa mwanadamu.

1. Jinsi gani mkono uliopooza (haribika) unaweza kuathiri maisha ya mwanadamu? (Kazi, masuala ya fedha, familia, imani? Ni aina gani ya kazi moja katika siku hizo inaweza kufanywa kwa kutumia mkono mmoja?
 • Katika mstari wa 5 tunagundua kuwa hapo awali mkono ulikuwa mzima. Je, unafikiri mtu alipata changamoto gani baada ya mkono wake kupooza, pengine kutokana na ajali?
 • Je mwanadamu anapata aina gani ya hisia katika kifungu hiki? Anajichukuliaje? (Aibu, waoga, waoga ...)
  2. Mazingira ya sinagogi yalikuwaje wakati wa Sabato?
 • Katika maandiko tumegundua ya kwamba mwanadamu hakukwenda kwenye sinagogi kuponywa. Kwa nini alikwenda?
 • Kwa nini mwanadamu hakumuomba Yesu amsaidie?
 • Linganisha kati ya mwanadamu mgonjwa na mwalimu (Mafarisayo) sababu za kuja kwenye Sinagogi siku ya Sabato.
  3. Kwa nini Yesu alimwambia mwanamume simama? Kwa nini yeye hakumponya bila kujulikana katika nafasi yake mwenyewe?
 • Je, unafikiri kwamba mtu angekuja mbele ya mkutano kwa amri ya mtu yeyote?
  4. Ghadhabu ya Yesu ni nadra kutajwa katika vitabu vya Injili. Kwa nini Yesu wakati wote alikuwana hasira na shida(5)?

  5. Je, mwanadamu alimfikiriaje Yesu ambaye aliweka misuli katika mkono uliopooza tena?
 • Unasema nini kuhusu Yesu?
  6. Kwa nini uponyaji wa mtu huyu ulikuwa muhimu sana kwa Yesu ili hali alikuwa tayari kuhatarisha maisha yake kwa sababu hiyo (4)?
 • Kwa nini Yesu aliuawa ingawa, ili kunukuu mstari wa 4, yeye alisaidia na kuokola watu?

  HABARI NJEMA: Sabato inamaanisha kitu tofauti kati ya Yesu na Mafarisayo. Kwa Mafarisayo ilimaanisha sheria ambazo watu walichunguza ili kuokolewa. Yesu kwa upande wake, siku ya Sabato ilikuwa tafakari ya Injili, ishara ya Mungu kuwapa watu wake mwenyewe kupumzika kutokana na kazi zao kupitia msamaha wa dhambi zao (Ebra 4: 9 - 10). Isomwe kwa pamoja!

  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster