GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

6. ADHABU YA KIFO (Marko 6: 16-29, kwa undani zaidi)Historia: Herode hakuwa mfalme bali mkuu wa mkoa - yeye alitawala zaidi ya robo moja ya Palestina kwa idhini ya Warumi'. MwanahistoriaYosefu anatuambia takriban mambo sawa kuhusu maisha ya Herode ya ndoa kama Biblia inavyoeleza. Kulingana na yeye binti wa Herode aliitwa Salome. Wakati alikamatwa Yohana alikuwa na umri wa miaka 30.

1. Jaribu kutafuta sababu kwa nini Herode alimtwaa mke wa kaka yake (17-18).
 • Unafikiria kwa nini Herode alitaka kubadili mumewe kwa mwingine?
  2.Kwa nini John aliingilia kati maisha ya ndoa ya Herode ingawa alijua hili ilikuwa ni hatari?
 • Utasemaje kwa mtu atakayekuja kwako na kukwambia makosa aliyokufanyia?

  3. Je, unaamini John alikuwa anafikiria nini wakati wamekaa katika minyororo jela baada ya kazi na mafanikio kama mhubiri? (Mk1: 5 inatuambia kwamba alikuwa maarufu sana)
 • Je, unafikiri John alikubali katika baadhi ya hatua kwamba alimhukumu Herode?


  4. Kwa nini Herode alimhofia John ingawa John alikuwa tu mfungwa (20)?
 • Kwa nini John hakumhofia Herode ingawa alikuwa mfungwa?
 • Labda kulikuwa na kitu alichokisema Yohana ambacho kilimvuta nia ya Herode. Kilikuwa ni kitu gani?

  5. Salome, binti wa Herode, alikuwa katika umri wa kuvunja ungo. Jaribu kufikiria maisha ya msichana huyu yalikuwaje.
 • Kwanini msichana hakutamani zawadi ya kusherehekea siku ya kuzaliwa iwe farasi au nguo maridhawa, vitu ambavyo wasichana na umri huo hutegemea kuvipata?
  6. Unaamini Yohana alikuwa anafikiria nini katika saa yake ya mwisho? Unadhani Yohana alikuwa ameelewa maana ya maisha ndani ya Yesu? Yohana alijua maandiko vizuri pamoja na unabii wa Yesu katika Agano la Kale. Tusome Isaya 53: 3-6.7.
 • Unadhani ni nini kilikuwa mawazoni mwa Wanafunzi wa Yohane kuhusu hatima ya mwalimu wao (29)?
 • Ni yapi yanayofanana na ni tofauti gani unaweza umepata kati ya maisha na vifo vya Yohana na Yesu? (Kiongozi anaweza kuorodhesha kwenye karatasi au kwenye ubao)
  8. Yohana aliwaandaa watu tayari kukutana na Yesu (Yohana 1:28). Yohana alifanyaje hili?
  9. Unafikiri ni ujumbe upi muhimu zaidi katika hadithi hii kwako na kwa rika lako?
  5b. MIKATE 25,000 NA SAMAKI 10,000 (Mark 6: 30-44)
  Historia: Kiongozi wa kundi anaweza kuonyesha kwenye ramani eneo la kulisha miujiza hii mkabala na Bethsaida (45) na kuhesabu ni kilomita ngapi kutoka huko hadi muhimu zaidi katika Galilaya. Kumbuka kwamba ni Yesu 'na wanafunzi wake' nia ni kupumzika wakati wa safari hii (31-32).

  1. Nini kawaida ya mtu ambaye ana kazi muda mwingi hadi anakosa muda wa kula (31)?
 • Unadhani ni nini kilichokuwa katika ma walipoona umati juu ya pwani kusubiri kwa Yesu (32-33)?
 • Kwa nini Yesu hakukupata wasiwasi wa umati huu ingawa alipoteza siku yake (34)?

  2. Wakati Yesu alipomaliza kuhutubia muda ulikuwa umesogea sana na ilikuwa tayari ni alasiri. Unadhani wanafunzi walikuwa katika hali gani kwa wakati huo?
  3. Chapati tano na samaki wawili inamaanisha ni chakula kwa mtu mmoja. Kwa fedha za nchini kwako unakoishi sasa ingekugharimu kiasi gani cha fedha?
 • Ni vijiji vingapi ambapo takriban kila mmoja angepata ili aweze kuzalisha chakula cha watu 5,000 chapati 25,000 na samaki10,000?
  4. Kwa nini yesu aliwaambia wanafunzi wake : "Wapeni kitu cha kula"(37)?
 • Wanafunzi walijibu nini kuhusu maagizo haya ya Yesu?
  5. Wanafunzi walipata wapi ujasiri wa kufanya jinsi Yesu alivyowaambia? (39)
 • Je, watu waliamini kwamba watapata chakula wakati wao waliketi kwenye nyasi na kama waliamini, wapi walifikiria chakula hicho kilitoka wapi (40)?
  6. Angazia sababu mbalimbali kwanini waaminio kwa dunia ya kileo siyo mar azote wanaamini kuwalisha wenye njaa?
 • Wenye njaa wako wapi wale ambao Yesu anakutaka uwalishe?
  7. Unaamini ya kwamba Yesu anaweza kuzidisha mara 5000 zawadi ambazo unampa (hata kwa kiasi kidogo)?


  HABARI NJEMA: Baada ya kufanya ishara hiyo Yesu alisema: "Mimi ni mkate hai ulioshuka kutoka mbinguni. Mtu yeyote akila mkate huu ataishi milele. Mkate huu ninaoutoa ni mwili wangu "(Yohana 6:51). Wakati akifa juu msalabani Yesu akawa mkate wetu wa kisakramenti na mkate wa uzima wa milele (kwa kuamini katika kifo cha Yesu Msalabani tuna uzima wa milele).

  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster