GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

4. YESU AKIWA KIJANA Luka 2:40-52


KUMBUKA: Watoto wa kiume wa Kiyahudi huwa wanaume wakiwa na umri wa 13. Mwisho Yesu alikuwa na ndugu zake wa kiume wanne na dada zake (Mathayo 13:55-56). Baba yake alikuwa seremara na alijifunza biashara ya baba yake. Hekalu ni mahali pekee ambapo Wayahudi waliruhusiwa kutoa kafara kwa ajili ya dhambi zao. Mungu aliahidi kuwa uwepo wake utakuepo pale.
1. Mariamu alitunza familia ambayo iliendelea kukua. Je unafikiria safari ya pasaka ya kila mwaka ilimaanisha nini kwake?
 • Je ni maandalizi ya aina gani ambayo alikuwa nayo ili kuzesha kufanya safari ya majuma mawili?

  2. Fikiria maisha ya kila siku ya mvulana Yesu kama mtoto wa kwanza katika familia ambayo iliendelea kukua.
 • Ilikuwa na maana gani kwa mvulana Yesu kwamba aliweza kusafiri, pengine kwa mara ya kwanza kwenda Yerusalemu na wazazi wake?
  3. Kwa nini Yesu hakuwaambia mapema wazazi wake kwamba asingali rudi nyumbani pamoja nao ?
 • Zaidi ya sehemu zote, kwa nini Yesu alitaka kwenda Hekaluni?
  4. Je mistari ya 46-47 inatuonyesha nini juu ya Yesu?
 • Ni nini ambacho kilivutia huyu mvulana wa miaka ?
  5. Kwa nini Yesu alishngaa kwamba wazazi wake hakujua alikwa wapi?
  6. Kwa nini ilikuwa muhimu kwake Yesu kukutana na baba yake wa mbinugni Hekaluni badala ya mahali aikokuwa?
  7. Je mstari wa 48 unatuonyesha nini juu ya Mariamu?
 • Je Mariamu alifanyaje alipokosa kumwona mwanae miongoni mwao?
  8. Je wazazi wa Yesu wajisikiaje waliposikia mvulana wao akijibu katika mstari wa 49?
 • Je Yesu alitaka kuwafundisha nini wazazi wake kutokana na tukio hili?
  9. Kulingana somo hili, lini tuna haki kuenda kinyumbe na wazazi wetu?
 • Kulingana na somo hili, ni nini mapenzi ya Mungu dhidi ya kijana?
 • Kulingana na somo hili, tunahitaji wa kuwatenda vijana wetu?
  10. Je uhusiano wa Yesu na wazazi wake ulikuaje na watu wengine katika kipindi cha miaka 18 katikati ya tukio hili na kwanzo wa huduma yake ya hadharni (51-52)?
  HABARI NJEMA: Sababu ambayo Yesu alipenda Hekalu imeandikwa katika Yohana 2:19-21. Kiongozi anaweza kusoma mistari hii.


  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster