GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

9. MPENDE ADUI YAKO! Luka 6:27-38


KUMBUKA: Ulipokuwa unasoma somo hili, fikiria juu ya juma lililopita - Ni kwa kiwango gani ulitimiza amri hizi katika maisha yako ya kila siku.
Mistari ya 27-30
1. Wengi wetu tunaweza kukubaliana kwamba kila mmoja wetu tunahitaji kuishi kama vile Yesus anafundisha hapa. Kwa nini ni vigumu kuishi hivyo?
 • Je ingekuwa raisi kufuata mafundisho ya Yesu kama angesema: "Uwe mwema kwa adui zako"
  2. Fikiria kuwa ungeweza kuanza kufwata sheria hizi ndani ya nyumba yako, shuleni ua kazini. Je unafikiri kutakuwa na mabadiliko gani, nyumbani kwako/Shuleni/kazini?
 • Je unafikiri uhusiano wako na mtu ambaye humpendi ungeweza kubadilika kama ungemwombea (28b)?
  3. Yesu alifwata amri zote hadi mwisho. Kwa nini bado alikuwa na maadui?
  4. Je chuki huleta madhara gani kwa mwenye chuki?

  Mstari wa 31-38
  5. Kuna tofauti gani kati ya "Wana wa aliye juu" na "wenye dhambi" kama vile wanavyoelezewa katika mistari hii?
 • Ni kwa njia gani unafanana na wana wa aliye juu nan i kwa njia gani unafanana na wenye dhambi?
  6. Je wale wanaolalamika juu ya watu wengine kuwa hawawatambui wanaelewakaje vibaya (36-38)?
 • Ni watu gani ambao wanahitaji upendo usio na mipaka zaidi ya wote ?
  7. Mstari wa 35 unaelezea juu ya upendo wa Yesu kwetu hata kama tungekuwa maadui wake. Soma mtari huo na ujibu swali: Je nivigumu au raisi kwa mwanadamu kuamini katika upendo huo usio na vipimo?
  8. Thawabu kubwa imea ahidiwa kwa wale ambao wanafwata amri hizi (35). Yesu alifanya na badala ya kupewa thawabu alisulubiwa. Kwa nini?
  9. Je tunawezaje kujifunza kuwapenda maadui zetu?
 • Wale ambao wameshindwa kuwapenda adui zao watawezaje kuwa wana wa aliye juu?

  HABARI NJEMA: Kwa maana halisi ya neno, Ni Yesu tu ambaye ni mwana wa Mungu aliye juu. Aliwapenda maadui zake na kuwapenda hadi mwisho. Hakuchukua thawabu kweke yeye binafsi, ila anawapa wale ambao wanamwomba msamaha wa dhambi kwa ajili ya kutoweza kutunza amri hizi zote.  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster