GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

21. MKUYU TASA Luka 13:6-9


KUMBUKA: Mfano huu unazungumza juu ya Israeli. Kwa mda wa miaka mitatu Yesu alijihuzisha katika na taifa hili bila kupata matunda yakutosha katika taifa hili. Mfano huu hata hivyo unazungumza juu yetu pia. Wewe ndiye mkuyu, Mungu ndiye mmliki wako na Yesu nidye anaye tunza mti. Ujumbe nyuma ya mfano huu unaweza kuangalia pia katika Mathayo 21:18-19.
1. Udongo katika shamba ulikuwa udongo bora kabisa. Je Yesu alitaka kusema nini juu ya Israeli kwa kuweka mkuyu miongoni mwa misabibu?
 • Je huyu Mkuyu tasa ulileta madhara gani kwa misabibu iliyo uzunguka?
  2. Je ni matunda ya aina gani labda Mungu alitarajia kutoka maishani mwako kwa miaka mitato iliyopita? (Jibu maishani mwako.)
 • Ni sababu gani ahsa zinazokuzuia kuzaa matunda kwa ufalme wa Mungu?
  3. Je mtunzaji wa misabibu alikuwa na hisia gani dhidi ya mkuyu tasa?
 • Kwa nini Yesu anawapenda Wakristo hata wale ambao hawazai matunda yoyote?
  4. Ebu fikiria Yesu amesimama mbele za Baba yake akiomba nyongeza ya mda kwa ajili yako. Ni nini kunamfanya afanye hivyo?
  5. Mtuzaji wa misabibu ana ahidi kupalilia kuutilia samadi. Je Yesu amefanya nini maishani mwako kwa mka wa miaka mitatu iliyopita ili kukuwezesha kuzaa matunda kwa baba yake wa mbinguni?
 • Je ni jinsi gani kukata tama na mateso katika maisha yetu vinachangia katika kuzaa matunda?
  6. Kulingana na mfano huu, kitatendeka kwa Mkristo ambaye mwishowe hatazaa matunda?
  7. Geukia Mathayo 21:18-19. (Kingozi asome mistari hii.) Tukio hili lilitokea katika juma la mwisho la maisha ya Yesu. Fikiria sababu mbalimbali kwa nini Yesu alitaka kuulaani mkuyu tasa?
 • Mistari hii miwili ina uhusiano gani na kifo cha Yesu.
  HABARI NJEMA: Baada ya kulaani mkuyu tasa, Yesu alichukua nafasi yake - Nafasi ya Israel, nafasi yako na yangu. "Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti." (Wagalatia 3:13).  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster