GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

24. MFANO WA KARAMU KUU Luka 14:12-24


KUMBUKA: Wageni ambao waliopokea mwaliko wa kwanza walikuwa ni Wayahudi. Sasa tunaweza kutumia mistari ya 16-20 kwa wote ambao wameitwa na Mungu kupitia kwa upatiso na neon la Mungu.
1. Kumbuka mara ya mwisho ulipokuwa na sherehe. Je ungefanya nini kama mtu angali kuambia ufanye kilingana na mstari wa 12-14?
 • Kwa nini Yesu anatwambia tuwaalike masikini na wagonjwa katika sherehe zetu?
  2. Tazama mistari ya 18-20. Sababu ilikuwa nini hasa kwa nini hawa watu watatu walikataa kuingia katika karamu?
 • Kwa nini mara nyingi tufikiria juu ya tulivyo navyo (18), kazi zetu (19), na maisha yetu ya ndoa (20) kuwa muhimu zaidi kuliko ufalme wa mbinguni?
 • Ni sababu gani hizi tatu unaguza maisha yako? (Jibu moyoni mwako.)
  3. Ni katika kiwango gani waalikwa walimtambua? Mmoja wapo ya tafsiri ni, kwamba walioalikwa walikataa mwaliko kwa sababu walijua kwamba wasingaliweza kulipa deni katika siku za usoni (12b) Kama hili ni kweli inasema nini juu ya wale waliokataa kufika?
 • Ni kosa gani kubwa wale ambao walikataa kufika walifanya?
  4. Karamu katika mfano huu ina maanisha mbinguni. Kwa nini watu wengi hawataki kwenda huko?
  5. Kuna tofauti gani kati ya wale ambao walialikwa kwanza na wale ambao miwshowe walifika katika karamu?
 • Kwa nini kundi la pili lilikubali mwaliko hata kama wale walioalikwa kwanza hawakuweza?
  6. NI akina nani ambao ni "maskini, na vilema, na vipofu, na viwete" -Wale ambao wanakubali kwa furaha mwaliko kwenda mbinguni (21)?
 • Kwa nini hawa watu hawakujali juu ya kuwaalika pia ili kuwali waliowaalika kwanza?
  7. Je mstari huu wa 23 unamaanisha nani?
 • Je mstari huu unatufundisha nini juu ya uinjilisti (Kutangaza Injili)?
  8. Je unaegemea upande gani katika makundi haya? (Jibu katika moyo wako.)
 • Je Mungu amefany nini katika moyo wako ili kuweza kukuhamisha kutoka kundi ili mbalo linakataa mwaliko katika kundi ambalo linakubali ?
  9. " Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari!" (17) Je Yesu aliweza kulipa nini ili aweze kukupa karamu hii?
 • Yesu anasema katika maneno haya: "Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari!" Jibu lako ni nini?
  HABARI NJEMA: Yesu alifanyika masikini "maskini, vilema, viwete, vipofu" ili kuweza kulipia karamu mbinguni. Hii ndio sababu mwaliko sasa ni bila malipo kwa kila mtu ambaye anataka kuja.


  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster