GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

30. MFANO WA MJANE Luka 18:1-8


KUMBUKA: Wanawake wakati wa Yesu wasingaliweza kumstaki mtu wala kuwa shahidi kotini. Ndugu zao wa kike waliweza kuwazaidia wakati wa mambo ynayohusu mahakama kianiaba yao. Mjane huy bila shaka hakupata msaada wowote wa namna hiyo. Pengine ndugu zake wa kiume walijaribu kuchukua urithi kutoka kwa watoto wake.
1. Kumbuka wakati ulimlilia msaada kutoka kwa Mungu usiku na mchana. Ni kwa nini ni raisi sana kuacha kuomba wakati kama (1 na 7)?
2. Fikiria maisha ya huyu mjane. Ni shida gani alikumbana nayo alipowalea watoto wake pekee yake?
3. Ni nini kinawafanya watu sawasawa na kadhi huyu katika mfano huu: Kwamba hawamwogopi Mungu na wala kujali wanadamu (2)?
 • Kwa nini Yesus alimfananisha Mungu na kadhi asiyetenda haki?
 • Je umewahi kujisikia kana kwamba Mungu ni hakimu asiye mhaki? Kama umewahi ni lini?
  4. Mjane aliridhika kwamba kadhi asiye asiye mhaki mwishowe atamzaidia. Kwa nini?
 • Tunawezaje kuwa na uhakika kwamba Mungu mwishowe atawazaidia wapendwa wetu na sisi pia?
  5. Ni nini kilifanyaki katika moyo wa huyu mjane alipokuwa analilia msaada kila wakati?
 • What happens in our hearts while we are praying a long time in spite of God's silence?
  6. Je maneno ya Yesu katika mstari wa 7-8 yana maana gani?
  7. Yesus alisimama mble ya kadhi. Je kulikuwa na mfanano na tofauti gani katika hali hizi mbili-ile ya kwake na na ya mjane? (Usisome, jadili kutoka kumbukumbu katik akilini mwako.)
 • Maombi ya Yesu yanatofautianaje nay ale ya huyu mwanamke (3)?
 • Je hukumu ya Yesu ilitofautianaje na ile ya yule mjane?
 • Hukumu ya Yesu ilikuwa ya haki au sio haki?
  8. Mstari wa 8b unahusu nini juu ya mfano huu?
  9. Mfano huu unakufundisha nini wewe binafsi juu ya maombi? (mstari wa 1, 5, 7, 8)?
  HABARI NJEMA: Pilato alipomhukumu Yesu alikuwa kadhi asiye mwenye haki. Lakini Mungu alipomhukumu Yesus kufa alikuwa mhaki, kwa sababu dhambi zako na za kwangu zilihesabiwa kwake wakati ule.


  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster