GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

32. MTOSHA USHURU JUU YA MTI Luka 19:1-10


KUMBUKA: Siku za Yesu, watosha ushuru walifahamika kwa kutokuwa waaminifu. Walitosha ushuru zaidi kutoka kwa watu na kujiwekea sehemu kubwa kuliko walitakiwa. Kwa kawaida tunafikiri kuwa Yesu alikuwa upande wa walionekewa na masikini, na hapa tunaona yuko upande wa kumgandamizaji. Katika utamaduni wa Kiyahudi, kuingia katia nyumba ya mtu kwa chakula ilikuwa ni ishara ya urafiki.
1. Je maisha ya kila siku ya Zakayo yalikuaje, mku wa watosha ushuru Yeriko? Ni yalpi yalikuwa mazuri na mabaya?
2. Je Zakayo angali halalisha mwenendo wa biashara yake na mtindo wa maisha yake?
 • Unafikiri ni kwa nini Zakayo alitaka pesa nyingi?
  3. Unafikiri ni kwa nini Zakayo alitaka kumwona Yesu-toa ababu nyingi uwezavyo?
 • Je unafikiri mkuu wa watosha ushuru angependa kuonekana akiwa juu ya mti? Toa sababu.
  4. Kumbuka wakati mtu Fulani alichukua pesa zako kinyume na sharia. Kam ungalikuwa mmoja wapo wa wadhiriwa wa Zakayo, je ungechukuliaje tabia za Yesu katika mstari wa 5?
  5. Je nini ambacho ni cha kushangaza juu ya Yesu kukutana na Zakayo mora ya kwanza-Kumbuka hii ilikuwa nia mara ya kwanza nay a Miwsho kuingia Yeriko?
  6. Je unafikiri ni lini Zakayo alianza kumwamini Yesu (5-8)? Jadili uwezekano mbalimbali.
  7. Je unafikiri Zakayo angalifanya nini kama Yesu angalisema, "Shuka chini mara moja na wape masikini nusu ya mali yako. Ndipo nije nyumbani kwako"?
 • Ungefanya nini kama Yesu angalikwambia: "Kwanza tubu dhambi zako ndipo niwe rafiki yako"?
  8. Ebu fikiri itakuwaje kama ungetoa nusu ya mali kwa siku mmoja. Ni nini kingelikufanya ufanye hivyo?
 • Je Zakayo alipata nini badala ya hela aliyopoteza?
  9. Kuna tufauti gani kati ya Zakayo na raia wa Yeriko? (Tazama mstari wa.7.)
 • Kwa nini alitaka kumtembelea mtu mbaya katika mjiti?
  10. Yesu anasema nawe leo: "Nitakuwa mgeni wako leo." Anataka kwenda nawe na kukaa katika nyumba yako. Utamjibu nini?
  11. Ninani alimtafuta nani katika somo: Je Zakayo alikuwa anamtafuya Yesus au Yesu ndiye alikuwa namtafuta Zakayo? (3,9,10)?
  HABARI NJEMA: Akiwa njiani kwenda Yerusalemu kwenda kusulupiwa, Yesu alipitia Yeriko. Pengine ni kwa ajili ya Zakayo. Yesus aliposamehe dhambi za Zakayo, alijua kuwa angalipata adhabu yaye. Msamaha wa dhambi ni bure kwa ajili ya Zakayo na ni bure kwa ajili yetu- lakini limgharimu Yesu maisha yake.


  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster