GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

37. MATEMBEZI YA KWENDA EMAU Luka 24:13-35


KUMBUKA: Emau ilikuwa ni mji ambalo ulikuwa 11 kilometa kutoka Yerusalemu. Ilichukua angalau masaa mawili kutembea umbali huu. Mariamu mke wa Clopa, alitajwa kama mmoja wa wanawake ambao walisimama karibu na msalaba Yesu alipokufa (Yohana 19:25). Inawezekana ni mke wa Cleopa ambaye anatajwa katika somo hili.
1. Kama umewahi kuteza mtu ambaye unampenda, unajua ni mawazo ya aina gani, hisia na majuto ambayo unakaa nayo baada ya mazishi. Simulia.
*Yesu alikufa siku mbili zilizopita katika kifo cha uchungu. Je unafikiri ni nini ambacho kilikuwa kigumu kwa Kleopa na marafiki zake siku zile?
2. Kwa nini Yesu aliwaruhus kwanza hawa wanaume wawili waombolezaji kuongea juu ya uchungu wao (15-17)?
 • Ni nini kingalifanyika kama Yesu angalianza kuwambia juu ya maelezo ya Bibilia moja kwa moja?
 • Yesu anajua masikitiko yetu tayari -Kwa nini anapenda kuyasikia kutoka vinywa veytu?
  3. Je imani ya hao wanaume wawili ilibadilikaje baada ya kifo cha Yesu (19-21)?
 • Kwa nini hawa watu wawili hakuamini yale mbayo wanawake na wengine waliwambia juu ya kufufuka (22-24)?
  4. Je kuna tofauti gani kati ya tafsiri Yesu anayoitoa juu ya kifo chake na ile Kleopa na rafiki yake walitoa (19-21 na 25-27)?
  5. Kwa nini Kleopa hakuelewa kutoka Moses na Manabii (k.m. Biblia) kwamba ilikuwa lazima Kirsto kutezeka na kufa?
  6. Kwa nini Yesu alijifanya kana kwamba anawapita kwenda mbali (28)?
  7. Kwa nini hawa wanaume wawili hawakutambua Yesu alikuwa nani hadi alipomega mkate?
  8. Ni nini kilichowafanya hao wanaume wawili kutembea umbali wa kilometa 11 kurudi Yerusalemu katika giza?
  9. Katika siku zetu watu wengi ambao wanajiita Wakristo hawamini kufufuka kwa mwili kwa Yesu. Ni Mungu wa aina gani hawa watu wanaamini?
 • Ni kwa nini mtu hawezi kuwa Mkristo kama aamini kufufuka kwa mwili kwa Yesu Kristo?
  HABARI NJEMA: Yesu alimega mkate katika nyumba ya Kleopa kwa mikono yake iliyokuwa na alama. Hawa wanaume waili wangalimtambua Yeus kwa alama ya vidonda. Tunaweza kukutana na Kristo mfufuka kwa njia sawa na ile kila mara tunaposhiriki katika meza ya Bwana.


  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster