GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

1. YUSUFU BABA WA KAMBO WA MWANA WA MUNGU 1:18-25


Kiongozi anaweza kuelezea kwa kifupi.Luka 1:26-38 Kwa mujibu wa sheria ya Musa, waliokiuka sheria za ndoa waliadhibiwa kwa kupigwa mawe.Uhusiano wa kingono haukuruhusiwa kabla ya ndoa.Kumb 22.
Historia: Swali katika mabano liulizwe tu kama hakuna mtu aliyekwisha kulijibu hapo kabla.
1.Nini kilichomfanya Yusufu ahisi kwamba Maria alimdanganya (18-19)?
 • Unadhani ni nini ambacho kilikuwa kigumu zaidi kwa Yusufu?
 • Je unahisi Maria alimwambia Yusufu kuhusu ujio wa malaika? Kama siyo, kwanini? kama ndiyo kwanini Yosefu alimwamini Maria?
  2.Kwanini Yusufu hakupenda kulipiza kisasi kwa Maria pamoja na familia yake ingawa alikuwa na haki ya kufanya hivyo kisheria?
 • Unafikiri kwa jinsi gani Yusufu alimuamini Maria kutokana na maelezo katika mistari (18-19)
  3. Unadhani ni kwanini Mungu hakumtuma malaika kwa Yusufu siku ileile aliyomtuma kwa Maria(20) Kwanini upendo wa Yusufu ulipimwa kwa njia ngumu kiasi hicho?
  4.Kuzaliwa na bikira ina maana manii yaliingia kwenye kizazi cha Maria kutoka nje ya ulimwengu huu.Ni katika misingi ipi inamfanya Yusufu kuamini uzazi bikira ingawaje hapo kabla katika historia haijawahi kutokea kitu kama hicho.
 • Ni makala gani katika maandishi yetu inatuthibitishia kwamba kuzaliwa na bikira siyo habari ya kutunga?
  5.Kwa nini unafikiria kuzaliwa na bikira ni kwa wengi(wanatheolojia pia) mafundisho magumu kuamini?
 • Ni kwa jinsi gani imani katika kuzaliwa na bikira na dhana ya Mungu zinahusishwa pamoja?
  6.Kwa nini haikuwa rahisi kwa Yesu kuokoa watu wake kutenda dhambi ilihali alikuwa mtoto wa Yusufu na Maria?
 • Kumbuka dhambi uliyoitenda ambayo dhamira yako inakusuta.Kisha soma mstari wa 21 tena.Weka jina lako mwenyewe sehemu yenye maneno "watu wake" Je unapousoma huu mstari unaamini ni ya kwamba ni kweli?
  7.Je Yusufu alivumiliaje kutokumgusa mkewe mpendwa Maria ilihali waliishi katika nyumba moja (25)?
  8.Bila shaka kila mtu alidhani mtoto wa Maria alikuwa ni wa Yusufu.Je unafikiri Yusufu hakuieleza ukweli ili aonekane msafi kwa familia ya Maria?
 • Kwanini Mungu hakumchagua mtu mwingine awe baba wa kambo wa mwanaye?
  HABARI NJEMA: Hakika Yusufu alikufa kabla Yesu hajaanza huduma kwa uma, lakini alijua jambo muhimu kuhusu mwanawe huyo wa kambo:Angewaokoa watu wake akimjumuisha mwanaye wa kambo.


  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster