GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

2. WATU WENYE BUSARA KUTOKA MASHARIKI 2:1-12


Historia: Wayahudi wengi waliishi Uajemi(Zamani ilijulikana Babeli) hata baada ya uhamisho ulipomalizika mapema miaka 500.Watu wenye hekima walikuwa ni wachawi na wana anga na walikuwa na dini tofauti ya ile ya Wayahudi.Umbali kutoka Uajemi hadi Palestina ilikadiriwa kuwa kilometa 1000 hadi 1500.
1.Safari ya watu wenye busara ilichukua muda gani,iwapo ngamia alitembea kilometa 30 kwa siku?
 • Je unadhani wakuu,wanawake na majirani waliichukuliaje safari hii?
  2.Je unafikiria ni kwanini watu wenye busara walitaka kumwabudu Mfalme wa Wayahudi badala ya kumwabudu Mfalme wao ?
 • Kwanini watu wenye busara walitaka kutoa zawadi za thamani kwa Mfalme mpya wa Wayahudi?
  3.Wayahudi hawakuwa na Mfalme kwa muda wa miaka 600.Herode alikuwa tu ni kibaraka wa Warumi.Kwanini Herode na watu wote wa Yerusalemu walisikitika waliposikia habari ya kuzaliwa mfalme mpya(3)?
 • Herode aliamini nini(4,16).(Aliamini nini kuhusiana na cheo chake -Biblia-masihi-mpango wa Mungu.
  4.Ni kutokea hatua ipi hadi ipi nyota iliwaongoza watu wenye busara angalia mstari wa 2 na wa 9
 • Kwanini Mungu hakuiruhusu nyota iwaongoze watu wenye busara moja kwa moja hadi Bethlehemu-kwanini wapitie Yerusalemu ? (Kwanini ilikuwa ni muhimu kwa watu wenye busara kuhusishwa na neno la Mungu?)
 • Ni aina gani ya nyota Mungu ameituma kwenye maisha yako kukuongoza kumjua Yesu?
  5.Wababeli walijenga mnara wa Babeli wakaiba safu ya agano na pia walibomoa hekalu.Watu wenye busara walikuwa wanao. Kwa nini Mugu aliwaongoza maadui kuwa wa kwanza kumwabudu mwanawe kama mfalme?
  6.Wakati wakisikia uvumi wa kuzaliwa mfalme mpya Bethlehemu,umbali wa kilometa kumi na mbili,kwanini hakuna Myerusalemu yeyote kumwabudu kule?
  7.Ni kwa njia gani mfalme mpya pengine alikuwa tofauti na waliyofikiria kabla?
 • Ni nini kipo katika imani ya watu wenye busara kama mfano?
  8.Watu wenye hekima walitoa zawadi kwa mtoto Yesu.Je wao walifaidika nini kutoka kwake?
 • Kwanini zawadi hizo zilihitajika kwa familia ya Yusufu(13)?
 • Utampa nini Yesu kama zawadi ya kuzaliwa kwa mwaka huu?
  9.Unafikiriaje maisha ya hawa watu wenye busara baada ya kurejea Uajemi katikati ya wapagani na dini za kipagani?

  HABARI NJEMA: Mara nyingi katika maisha yake Yesu hakupewa heshima ya Kifalme.Watu wenye busara walimwabudu katika maisha yake na Pilato Gavana wa Kirumi aliandika cheo chake juu ya msalaba.Yesu alikuwa ni mfalme pekee aliyewaalika hata maadui zake waje kuabudu.  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster