GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

5. MAHUBIRI KUTOKA MLIMA SINAI 5:21-32


Historia: Kama Musa alivyowapa watu wake sheria ya Mungu kutoka mlima Sinai,ndivyo alivyofanya Yesu "Musa mpya ".Katika amri ya zamani Yesu aliongeza ufahamu mpya.
1. Hasira inahusishwaje na mauaji? (21-22)
 • Umewahi kuitwa "mwema kwa ajili ya kitu " au "mjinga" Ulijisikiaje?
 • Je inamwathirije mtoto akiendelea kuitwa "asiyefaa" au" mjinga"?
  2. Je utajipa adhabu gani kwa dhambi iliyoongelewa katika mstari (21-22)
 • Ungetoa adhabu gani kwa watu ambao wangetenda dhambi kwa ndugu zako?
  3.Kwa nini ni lazima kupatana na watu wengine kabla ya kutekeleza wajibu wetu wa kidini? (23-24)
 • Kwanini yesu hakupendelea makosa ya walalamikaji lakini aliwaamuru wamfuatao wachukue hatua za kuwezesha kupatikana kwa ndugu yao?(23 - 25)
 • Nini kitatokea endapo kwenye familia/shule/eneo la kazi kama utafuata na kutekeleza maagizo ya Yesu katika mistari hii?
  4. Mungu angesema "Kaka yako akikukosea sahau na usiweke moyoni kabisa! "Je ni rahisi kwako kufuata maagizo zaidi ya yaliyotolewa?
 • Nini kitatokea kwa mtu ambaye hasamehi wamkoseao?
 • Ni nani aliyemtenda dhambi Yesu unataka kusamehe leo? Unaweza kujibu kwenye moyo wako
  5. Kwa nini Yesu anafikiria dhambi iliyotendwa na mtu kifikra kwamba ni yakweli? (27-28)?
 • Fikiria hali ambayo macho yako na mikono yako inakushawishi kutenda dhambi, ni kwa njia gani utaweza kuidhibiti hali hiyo? (29-30)?
  6.Je ni nini hasa Yesu alifundisha kuhusu talaka(31-32)? Zingatia maandiko!
 • Fikiria hali inavyokuwa pale mwanandoa anapopenda mtu mwingine.Yapaswa kufanya juhudi gani kama wakosaji wakiamua kufuata maagizo ya Yesu?
  7. Kuna tofauti gani kati ya mafundisho ya Yesu kuhusu ndoa na jinsi watu wanavyofikiria katika ulimwengu wa kileo?
  8. Ungeelezeaje kifungu hiki kwa mtu aliyekiri kuwa tayari kuishi kama amri zinavyoelekeza? Vipi kuhusu mtu aliyekata tamaa kwa kukosa uwezo wa kuishi kwa mujibu wao?
  HABARI NJEMA: Yesu aiadhibiwa kwa adhabu zote zilizoorodheshwa kwenye kifungu hiki kutokana na hukumu ya moto wa Jehanamu.Alitakiwa kulipa hata senti yake ya mwisho ili kulipa madeni yetu-deni tunalodaiwa na Mungu ni kutokufuata amri zake.(Linganisha na mstari wa 26)


  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster