GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

6.USIOGOPE 6:25-34


Historia: Neno haki (33) maana yake ni usafi kamili wa maneno na matendo.Watu wema tu ndiyo watakaokwenda mbinguni.
1.Kwa kutumia maneno yako mwenyewe elezea mambo ambayo Yesu alitukataza katika kifungu hiki.
 • Ni vitu gani kati ya vilivyoorodheshwa vinakupa hofu zaidi?
 • Maisha yako ya hofu yamebadilikaje baada ya kusoma kifungu hiki?
  2.Je ni nini kitatokea katika familia yako iwapo mwanafamilia mmoja atakuwa na hofu ya pesa,afya na maisha ya baadaye?
 • Je hofu inaifanyia nini miili yetu?
  3.Je hofu na ukosefu wa imani vinashabihiana?
 • Je tutapunguzaje kiwango cha hofu na ukosefu wa imani katika maisha yetu?
  4.Tafuta ahadi zote Yeu alizowapa wanafunzi wake katika kifungu hiki.
 • Ni ahadi gani ambayo ni rahisi kwako kuamini? Ni ipi ambayo ni ngumu kuamini?
  5.Soma kifungu cha 31-35.Ni kitu gani unahitaji zaidi kwa leo(Unaweza kujibu moyoni)
 • Je waamini ya kwamba Baba wa mbingunianajua mahitaji yako ya leo? Toa sababu.
  6.Inamaanisha nini kwa vitendo kutafuta kwanza ufalme wa Mungu? (33)
 • Kwa nini watu wanatafuta kwanza furaha zao badala ya kuanza na ufalme wa Mungu?
 • Unatafuta nini kwanza? (Unaweza ukajibu moyoni)
  7.Inamaanisha nini kivitendo kuutafuta wema wa Mungu ,na siyo wema wa mtu (33b)?
 • Kama una uzoefu ambao umepelekea kutafuta haki yao mwenyewe kwa kutafuta haki ya Mungu,tafadhali badilishana uzoefu na wengine.
  8. Mstari wa 34 una maana gani?
 • Fikiria kipindi ambacho ulikuwa na wasiwasi kuhusu jambo fulani kwa siku zako zijazo.Ni nii unapaswa kufanya badala ya kuwa na hofu?

 • Unaijua hali yako kwa sasa Yesu bado anaongea juu yako mistari 33-34.je utamjibu nini?
  HABARI NJEMA: Daima Yesu aliuweka ufalme wa Mungu kuwa muhimu kuliko vitu vingine vyote.Na bado hakupewa moja ya mambo mema yaliyoahidiwa katika kifungu hiki lakini ni msalaba.Yesu alibeba adhabu ya msalaba na woga wa kutokumwamini Mungu.Ndiyo maana anaweza kupokea hata wenye imani haba.


  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster