GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

7. MANABII WA UWONGO 7:15-25


Historia: Manabii walikuwa ni watu ambao walitangaza neno la Mungu kwa watu wake.Tunaweza kutumia vigezo katika kifungu hiki kwa mtu yeyote ambaye anasimama mbele ya wengine kwa madai ya kutangaza neno la Mungu,bila kujali kama yeye ni mchungaji au msharika wa kawaida.
1.Jaribu kutafuta sababu nyingi kadiri iwezekanavyo kutokana na kifungu hiki kwanini ni vigumu kumwambia mtu kwamba wewe ni nabii wa uwongo.
 • Kwa mujibu wa kifungu hiki,manabii wa uwongo hufanya kazi zao ndani au nje ya kanisa.
  2. Unafikiriaje nabii wa uwongo,ambaye ni mbwa mwitu aliyevaa mavazi ya kondoo,kweli anafanya kazi ya kanisa?
 • Je walimu wa uwongo wanajua wazi ya kwamba wao ni mbwa mwitu walio katika mavazi ya kondoo? Toa sababu.
 • Ni matunda gani unaweza kuyaelezea endapo unabii ni ukweli au uwongo (16-20)? Toa baadhi ya mifano halisi.
  3. Katika siku hizi umesikia wapi mambo haya yakitokea kama yalivyoelezewa katika mstari wa 22 (unabii,kutoa mapepo na miujiza)?
 • Yesu anawakosolea nini hao watu, ambao hata wametenda miujiza mikubwa kwa jina lake?
 • Ni kwa kigezo gani kinatumika kutathmini watu ambao wanafanya miujiza katika makanisa ya kikristo?
  4. Je manabii wa uwongo wanachukuliwa kama lengo la dini?
 • Fikiria mtu ambaye anatembelea mikutano hiyo ambapo miujiza hutokea.Nini kinakuwa kimepungua kwenye imani yake?
  5. Ni nini tabia ya manabii wa uwongo dhidi ya dhambi (21,23)
 • Kwa nini manabii wa uwongo walitambua wenyewe ya kwamba wao ni watenda maovu?
  6. Fikiria jinsi manabii wa uwongo wanavyotumia jina la Yesu.Kwa makusudi gani hawatumii?
 • Kiongozi anaweza kusoma Warumi 10:13.Kuna tofauti gani kati ya manabii wa uwongo na watu wa Paulo ilivyoainishwa katika mstari hapo juu,kuhusu jinsi jina a yesu lilivyotumika?
  7. Ni kwa jinsi gani Yesu alijijua mwenyewe (23)?
 • Kwanini Yesu hakugundua ya kwamba hawa watu walitumia jina lake katika kutenda miujiza mikubwa?
 • Tunawezaje kujua leo kama Yesu atatukubali ama kutukataa siku ya mwisho?
  8. Ni ujumbe gani ambao manabii wa ukweli wanao kwa wale wenye dhambi,wapotevu ambao wamepoteza furaha yao duniani na ambaowanakabiliwa na kifo?
 • Ni kazi ya nani kwa ulimwengu wa leo kuwaonya Wakristo kuhusu manabii wa uwongo?
  HABARI NJEMA: Shetani hawezi kuwa kama mwanakondoo wa Mungu,Yesu,kwa sababu yeye hana majeraha yeyote katika mwili wake.Tatizo la manabii wa uwongo hawakubali dhambi zao na kwa sababu hiyo hawahitaji msalaba.Ndiyo maana hawaoni umuhimu wa kumtambua Yesu kama mwokozi wao.
  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster