GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

8.AFISA WA KIGENI 8:5-13


Historia: Huyo alikuwa afisa wa Kirumi anayewakilisha majeshi ya utawala.Hakika watu waliuwawa kwa silaha.Dini ya askari wa Kirumi walifanya ibada ya Kaizari.kiongozi anatakiwa aelezee kwa ufupi mambo makuu kuhusu Abrahamu,Isaka na Yakobo.
1. Huyo afisa katika maandiko haya pengine alisikia mafundisho ya Mungu kutoka kwa mtumishi wake wa kiyahudi.Fikiria sababu nyingine ambazo kwanini afisa wa Kirumi amekuwa karibu na yeye(5-6)
2.Wayahudi hawakutembelea makazi ya wageni.kwa sababu iliwafanya najisi.Kulikuwa kuna sababu gani nyingine iliyokuwa katika akili ya Mroma kutokustahili kumpokea Yesu katika boma lale? (7-8)
3. Elezea imani ya huyo afisa wakati alipomsoggelea Yesu.
 • Unaamini ya kwamba shida zako zitaweza kutatuliwa kwa neno moja kutoka kwa Yesu (8) ?
  4. Ni kitu gani afisa alifikiria anacho kama Yesu?
 • Afisa alilionaje jeshi la Yesu lisiloonekana iliahali hakuna mtu yeyote angeweza kuliona?
 • Unaamini ya kwamba Yesu anaweza kuamuru malaika mmoja amsaidie mtu aliyemwomba kusaidiwa? Toa sababu.
  5. Injili inataja matukio mawili tu ya Yesu yanayowafurahisha imani ya watu. Kulikuwa na nini maalum kuhusu imani ya mroma(8-10) (Kuna tofauti gani kuamini miujiza na kuamini neno la Yesu?)
  6. Katika mstari wa 11 na 12 Yesu amesema inawezekana kuwa rahisi kwa mgeni,ambaye amekiri kutoka dini nyingine,amwamini zaidi ya hao ambayo wanaifahamu Biblia.Kwanini iwe hivyo?
 • Kitatumika kigezo kipi ili kuweza kutambua watakaoingia kwenye ufalme wa Mungu (mbinguni) na ambao watatupwa kwenye giza(kuzimu)?

  7. Mungu alikuwa amewapa ahadi zake kuhusu Masia na ardhi kwa Abrahamu,Isaka na Yakobo.Ni kwa jinsi gani imani ya hawa watu watatu inafanana na imani ya askari Mroma?
  8. Afisa hakuwa amejua kilichomtokea mtumishi wake.Unafikiria alitegemea kukuta nini nyumbani? (13)?
 • Yesu amesema maneno katika mstari wa 13 kwa ubinafi wa kileo..Utamjibu kitu gani?
  HABARI NJEMA: Yesu alitupwa nje ya ufalme wa Mungu,kwenye giza,kulipokuwa na kilio na kusaga meno (12).Kwa njia hii aliandaa kibali cha kwenda mbinguni kwa askari wa Kirumi na kwetu ambao hata hatukustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni.  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster