GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

9. WITO KWA MATHAYO 9:9-13


Historia: Kwa Wayahudi wa wakati wa Yesu,kula pamoja ilikuwa ni ishara ya upendo.Watoza ushuru walikuwa wakionekana watu wenye imani haba kwa sababu hawakuwa waaminifu na masuala ya fedha.Mathayo alichukuliwa kama mtu ambaye aliandiak injili iliyozaa jina lake.
1.Fikiria maisha ya kila siku ya Mathayo,mtoza ushuru.Yapi aliyoyafanya yaliyokuwa mema na yapi yalikuwa mabaya?
  • Unafikiria uhusiano wa Mathayo na Mungu ulikuwaje ingali alikuwa mtoza ushuru?
  • Mathayo alitegemea Yesu aseme nini wakati alipoingia katika kibanda cha kukusanyia kodi?
    2. Kwa nini Yesu hakumuuliza Mathayo : "Unataka kuwa mwanafunzi wangu"?
  • Unadhani Mathayo alijisikiaje wakati mwalimu wake na mfanyakazi wa miujiza walivyomtaka kuwa mfuasi wake?
  • Kwa nini Yesu alimtaka mtoza ushuru awe mwanafunzi wake ilihali alijua watu wangeweza kumkosoa?
  • Kwa nini Yesu anataka wewe uwe mwanafunzi wake?
    3.Wenzake Mathayo walifikiria nini baada ya yeye kuondoka pasipo kupanga dawati lake?
  • Ni kwa jinsi gani Mathayo aliweza kuacha kazi yake ambayo ilikuwa inamuingizia kipato?
  • Mathayo alipata faida gani baada ya kuacha kazi iliyokuwa inamuingizia kipato?
  • Mungu anakwambia,labda ni mara yako ya kwanza,labda ni mara ya mia moja "Nifuate mimi!" Ungemjibu nini?
    4. Pamoja na Mathayo,baba wa nyumba ya waamwaminio Yesu,Unafikiria maisha ya mke na watoto yalibadilika?
  • Kwanini Mathayoalitaka kufanya sherehe kwa Yesu na wenzake(10)?

  • 5. Kuna makundi gani katika jamii yetu,watu wenye heshima ambao hawataki ushirikiano?
  • Kwanii Mungu alitaka kushirikiana na watu wa aina zote?
    6. Yesu anamaanisha nini katika mstari wa 12-13?
  • Ni katika kundi gani ambalo unajiona uko kati ya hayo mawili:mwenye afya au ugonjwa,msafi au mwenye dhambi?(unaweza kujibu kimoymoyo.)
  • Mwanga ulioupata katika maandiko haya,unafikiria umepata ugonjwa na dhambi maishani?
  • Kwa nini mara nyingine ni rahisi kutoa sadaka kwa Mungu zaidi ya kuonyesha wema kwa majirani?
    7.Kwa nini Yesu, "daktari", alitakiwa awe na moyo uliopondeka? Kwanini yeye aliye mwema anatakiwa kuhesabiwa miongoni mwa wenye dhambi?(linganisha Isaya 53:10-12)
    HABARI NJEMA: Yesu amekuwa sadaka kailifu kwa Mungu-ndiyo maana Yesu hakupendelea zawadi nyingine kutoka kwetu isipokuwa kutumia nguvu zetu kuokoa majirani zetu.











    ***

    Version for printing    
    Downloads    
    Contact us    
    Webmaster