GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

UVUMILIVU WA ADHA 10:16-31


1.Unadhani ni kwa kiasi gani Wakristo ni watu wa chini na hata kupata mateso katika jamii yetu?
 • Wakristo wanashutumiwa zaidi kwa lipi katika jamii yetu?
  2.Nini kitatokea kwa kondoo aliye katikati ya mbwa mwitu (16)?
 • Yesu alimaanisha nini aliposema atawatuma wanafunzi wake kama kondoo waliozungukuwa na mbwa mwitu?
 • Ni kwanini mtu anafananishwa na nyoka alivyo mjanja au mwerevu kama njiwa?
  3. Ni kwa uhalifu gani wanafunzi wa Yesu walihusishwa walipoletwa kwenye majaribu (17-22)?
 • Kama ungejua kwamba ungetiwa hatiani kwa sababu ya imani yako,unafikiria ungweza kuogopa la kusema? (19-20)
  4. Ni katika aina gani ya jamii ambayo wanafamilia wanafanya mambo yalivyoelezwa katika mstari wa 21?
 • Ni nini kinafanya mtu abaki katika imani hata watu wengine wasipokubaliana naye (22)?
 • Unafikiria utaishije kama siku moja ungeteswa kwa sababu ya imani yako?
  5. Tunaweza kuutumia mstari wa 23 katika ulimwengu wa kileo?
  6. Nini maana ya mwanafunzi ambaye mwalimu wake alishavumilia mateso sawaa na yake (24-25)?
  7. Fikiria watu wawili walioko katika mateso.Mmoja wao anajua uwongo utajulikana na ukweli utashinda mwishoni.Mwingine hana uhakika juu ya hilo.Itakuwa hali gani kati ya wawili hao (26)?
  8. Tafuta sababu nyingi uwezavyo kwa nii Mkristo asiogope mateso(26-31).
 • Mkristo anatakiwa afanye nini hata akiwa katika kipindi cha mateso(27)?
  9. Katika mstari wa 28,Yesu alimtuma mungu kwa shetani?
 • Jinsi gani mienendo ya Mkristo amnaye anahofia ya kwamba hakuna mwingine zaidi ya Mungu katika kipindi cha mateso?Vipi kuhusu Mkristo ambaye anamwogopa shetani?
 • Kwa mujibu wa aya ya 28,ni janga gani katika maisha ya mwanadamu?
  10.Yesu anaamini hata Mkristo anaweza kuuwawa na maadui zake(28).ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia mstari wa 29-31 kwa maisha ya mashahidi kwa mfano Yohana mbatizaji?
 • Kwa nini ni vigumu kuteketeza kanisa la Kikristo kwa kutumia mateso?
 • Katika mstari wa 30-31 Yesu anaongea na wewe.Wanamaanisha nini kwako katika hali yako y amuda huu?
  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster