GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

HABARI NJEMA KWA MASKINI 11:1-6Historia: Yohana mbatizaji, kwa sasa miaka 30 imepita alikuwa ni mwanaume aliyembatiza yesu na akashuhudia jinsi roho mtakatifu alishuka kutoka juu mbinguni.Katika jibu lake kwa Yohana,Yesu anamnukuu nabii Isaya(Isaya 35:5,6 na 61:1) Kiongozi anatakiwa kusoma aya hizi.
1. Yohana mbatizaji alifungwa kwa kumkosoa Mfalme Herode kwa uasherati wake.Ni nini kilimuumiza zaidi kwa kitendo cha kufungwa kwake?
 • Yohana alipokutana na Yesu kwa mara ya kwanza,alisema "Tazama mwanakondoo wa Mungu,aliyechukua dhambi za dunia"(Yohana 1:29). Ni nini kilichomfanya awe na mashaka imani yake ya awali?
  2.Yohana atatoa hitimisho gani kuhusu maisha yake mwenyewe kama itakuwa wazi kuwa Yesu kwa wakati huo hakuwa kristo?
 • Kama ulishawahi kuwa na wasiwasi kwamba Yesu ni Mungu au laa.Ni hali gani itakutokea?
  3.Alipotuma wanafunzi wake kwa Yesu,Unafikiria Yohana alitegemea ujio wake wa kumtoa gerezanikiniujiza? (2-3) Toa sababu.
 • Kwanini Yesu hakumtembelea Yohana alipokuwa gerezani?
  4.Kwa nini Yesu hakujibu swali la Yohana:Ndiyo ni mimi.Hutakiwi kusubiri kwa mtu mwingine yeyote? (Kwanini yesu alitaka kujibu kwa kunakili katika maandiko kutoka katika agano la kale?)
 • Utajisikiaje kama utapata mstari wa Biblia kutoka kwa rafiki yako wakati wa huzuni?
 • Wakati wa kumnukuu isaya,kwanini yesu aliiruka ahadi kuhusu Masia kuwakomboa wafungwa?
  5.Ni maneno gani ya Yesu ambayo Yohana angeweza kuyatumia?
 • Habari njema maana yake ni msamaha wa dhambi(5). Kwa dhambi gani Yohana aliifanya iliyohitaji msamaha wa Mungu katika hali ile?
 • Kwanini mara nyingi Mungu hufanya waumini wake kama maskini kama Yohana mbatizaji alipokuwa gerezani?
  6.Maneno ya Mungu katika mstari wa 6 yanamaanisha nini?
 • Kwa mujibu wa kifungu hiki,tunatakiwa tufanye nini tunapokuwa na mashaka kwa jinsi Yesu anavyowatendea wapendwa wetu na sisi wenyewe?
  7.Je unafikiria Yohana alilipokeaje jibu kutoka kwa yesu? (Je alipata amani moyoni mwake kabla hajafa?)
 • Yohana alikuwa muumini wa kwei katika maisha yake yote.Unadhani imani yake ilibadilikaje wakati akiwasiliana na Yesu kwa mara ya mwisho?
  8.Yohana alifikiria nini kuhusu maisha na kifo pale ambapo Herode alipokuja kumkata kichwa?
  HABARI NJEMA: Yesu alisema kwamba alikuja kuhubiri habari njema kwa maskini ili kuwaponya waliovunjika moyo,kuwatangazia uhuru mateka..kuwafariji wotewanaoomboleza.(Isaya 61:1-2) yesu anakuja pia kwako leo kufanya hayo yote -kupitia neno lake.  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster