GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

MZIGO MWEPESI 11:28-30


Historia:Nira maana yake ni kipande cha mbao,ambacho kinaunganisha ngombe wawili ili waweze kuvuta kwa pamoja jembe,mzigo,n.k
1.Je ni nini baadhi ya mizigo ya kawaida ambayo watu wanabeba mabegani mwao siku hiizi?
 • Jaribu kufikiria mateso yako ya sasa hivi kama mzigo wa saruji.Ni mzigo mzito unaokadiriwa kuwa kilo 100.Bila kuupima nafikiria mzigo wako ni kiasi gani?
  2.Je ni jinsi gani mzigo wa mateso ni tofauti na mzigo wa dhambi(Mateso au dhamiri mbaya?)
  3.Fikiria maisha yako bila mzigo wowote.Nini kitakuwa kizuri au kibaya katika pande hizi mbili za maisha?
  4.Ni mtu wa aina gani unafikiria anaweza kukusaidia kubeba mzigo wako?
 • Inamaanisha nini kwa vitendo ukienda kwa Yesu na kukiri dhambi zako kwake?
  5.Yesu anamaanisha nini katika mstari wa 29?
 • Umepata pumziko la moyo wako?(Unaweza kujibi kimoyomoyo.)
 • Kwanini mtu mnyenyekevu tu ndiyo anayeweza kuutua mzigo wake? (Kwanini watu wengi wamekuwa na machungu wakati wa ubebaji mizigo yao?)
 • Tutakuwaje wanyenyekevu na wapole kama Yesu alivyokuwa?
  6.Maneno haya ya Jesus yanamaanisha nini: "Chukueni nira juu yenu"? (Nira ya Yesu ni nini? Inatofautianaje na mizigo yetu wenyewe?)
 • Jinsi gani hali yetu inabadilika kama tutabeba nira pamoja na Yesu?
  7.Yesu anamaanisha nini kwa kusema nira yake ni nyepesi na mzigo wake ni mwepesi(30)?
  8.Je watu hao walifanya nini pamoja na mizigo yao ambao hawakutaka kupelekwa kwa Yesu?
 • Kwanini hata Wakristo wengine daima hawapeleki mizigo yao kwa Yesu?
  9.Unafikiria mzigo wako utakuwa mzito kiasi gani ukijua hakuna hatia na pia hutakiwi kufikiria kuhusu kosa ni la nani?
 • Unafikiria mzigo wako utakuwa mzito kiasi gani iwapo utaamini ya kwamba Yesu atabadilisha matatizo yako yote yawe sawa bila wasiwasi?
  HABARI NJEMA: Kiongozi asome Yohana 19:17.Msalaba wa Yesu umebeba mizigo yetu yote;mateso na dhambi zetu.
  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster