GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

NGANO NA MAGUGU 13:24-30 na 36-43


Historia: Magugu ni majani mabaya ambayo huota yenyewe mahali palipopandwa mazao.Magugu haya huonekana kama ngano inapokuwa changa.Kwa sababu magugu haya yana sumu hayatakiwi shambani.
1.MFANO (24-30)
 • Kuna tofauti gani kati ya shamba lenye ngano pekee na lenye ngano na magugu?
 • Mtu anayepanda magugu kwa jiran yake ana nia gani?
 • Utachukuiaje kama mtu ataiharibu kazi yako kwa namna hiyo?
 • Ni nini kinachoshangaza jinsi mhudumu wa shamba alivyokabiliana na hujuma (28-30)?
 • Kwanini kila sehemu ya ngano ni muhimu kwa mkulima(29)?
 • Kuna uhusiano gani kati ya mbegu na tunda linalotokana na mbegu hiyo?
  2.TAFSIRI YA MIFANO (36-43) Kumbuka ya kwamba neno shamba lina maana mbili;ulimwengu(38),ufalme wa mwana wa Adam(41) ambalo ni kanisa la Kristo.
 • Mwanzoni Yesu aliita neno la Mungu mbegu.Kwanini sasa anawaita watu mbegu(38)?
 • Nani anaotesha watu na ni kwa namna gani (37,39)?
 • Je mfano huu unatufundisha nini kuhusu shetani anavyofanya kazi?
 • Shetani alikuwa na malengo gani alipomweka mwanawe ndani ya kanisa la Kikristo maeneo yote?
 • Muonekano wa usharika wa Mungu ukoje,kama hakuna matapeli ?
 • Kwanini hatuwezi daima kujua ambaye ni mwana wa Mungu na ambaye ni shetani?
 • Kwa nini ni hawaruhusiwi kutupa "wana wa Ibilisi" nje ya kanisa kabla ya hukumu ya mwisho?
 • Tumia ujumbe wa mfano huu katika ushirika wako mwenyewe Kikristo.
 • Unaweza kufikiria wewe ni mbegu ya aina gani;ngano au magugu? (Unaweza kujibu kimoyomoyo)
  kimoyomoyo.)
 • Kwa mujibu wa mfano huu, unafikiri inawezekana kwamba mtu ni nusu ngano, nusu magugu? Toa sababu.
 • Mwisho wa dunia utakuwa kama nini(41-43)?
 • Je Mungu anategemea mavuno ya aina gani katika ulimwengu huu?

  3. UADILIFU (43)
 • Kwa nini mara nyingi Yesu hutumia neno "haki" katika tafsiri ya mfano wake?
 • Kiongozi anapaswa kusoma Warumi 4: 5Tutakuwaje wenye haki?`

  4.MUHTASARI WA MASWALI
 • Tofauti ya msingi kati muumini wa kweli na mzushi ni ipi?
 • Unafikiri Yesu anataka kusema na wewe binafsi kupitia mfano huu?

  HABARI NJEMA: Ingawa alikuwa ngano bora alikuwa milele katika dunia hii,Yesu alivutwa na kutupwa katika tanuru la moto kama gugu.Ndiyo maana sasa anaweza kubadili magugu kuwa ngano na kuyavuna katika ufalme wa Mungu.


  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster