GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

HUZUNI KUBWA NA IMANIKUBWA 15:21-28


Historia: Wakanaani walikuwa maadui wakubwa wa Wayahudi. Tiro na Sidoni ni miji iliyojengwa katika umbali wa 45-60 km kutoka Galilaya. Yesu hakutaka mtu kujua kuhusu safari hii ya nje ya nchi (Mark 7:24). Kiongozi anatakiwa kuwaambia ukweli kuhusu Mfalme Daudi (22).
1. Fikiria maisha ya kila siku ya mama huyu, hasa mahusiano yake na watu wengine. (binti yake, mume, watoto wengine, majirani nk)
 • Kwa nini mama labda alijishtaki mwenyewe?
 • Ni mama gani katika ulimwengu wa kileo mwenye huzuni kubwa moyoni mwake kama mwanamke huyu alivyofanya?
  2. Mwanamke Mkanaani tayari alijua kitu ambacho wengi wa Wayahudi hawakuwa na ufahamu wa: ya kwamba Yesu alikuwa Mwana wa Daudi (22). Jinsi gani unadhani alikuja kujua ukweli huu?
 • Kwa nini mama aliomba kwa ajili yake (22)?
  3. Yesu alichukua hatua gani tatu za mwanzo kumsaidia mam huyu? (23-26)?
 • Kawaida Yesu huwakaribisha watu wote wanaosumbuliwa na matatizo. Kwa nini hakumsaidia mwanamke huyu?
 • Ungefanya nini kama Yesu angetutendea sisi kama alivyomtendea huyu mwanamke?
  4.Wanafunzi walijisikiaje kuhusu mwanamke Mkaanani katika hali nzima?
  5.Jinsi gani mama Mkanaani alilalamika kwaYesu baada ya kukataliwa(23,25,27)?
  6. Je, unafikiria ni nini kilichotokea katika moyo wa Yesu wakati alipokuwa kimya mama akiteseka?
 • Kwa nini Yesu wakati mwingine huwa kimya wakati wakati tunapomlilia atusaidie?
 • Kwa nini ni lazima imani ya kila mmoja wetu kupimwa?
  7. Yesu alisifu imani ya watu wawili tu. Jaribu iwezekanavyo kutafuta sifa nyingi za imani kubwa katika mwanamke huyu (28).
  8. Kwa ujumla ni jinsi gani inakisiwa ya kwamba mtu anapata imani kubwa katika moyo wa mtu?
 • Kiongozi anapaswa kusoma Mark 7:30. Jinsi gani mama huyu mapagani alipata imani kubwa hata kabla ya kuona miujiza ikitokea?
 • Katika hali ya aina gani hali tunahitaji imani kubwa?
  9. Yesu alikuwa na madhumuni gani katika safari yake moja tuu nje ya nchi?
  HABARI NJEMA: Juu ya msalaba Yesu alimwamini Mungu licha ya ukimya wake elezea Zaburi 22: 1-2,24. Imani ya Yesu ilikuwa sawa na ile ya mwanamke Mkanaani katika hatua hii. Tofauti kubwa kati ya hali zao ni kwamba katika kesi ya Yesu Mungu alikuwa kimya kwa sababu ya hasira yake, si kwa sababu ya upendo wake.  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster