GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

MFALME APANDA MJINI KWAKE 21: 1-11Historia: Watu walikuwa wakisubiri ishara ambayo ingethibitisha kama Yesu alikuwa mfalme au la - na punda alikuwa ni ishara, walitoa unabii kwa Zakaria (9: 9). Kwa kweli, Yesu alikuwa mwana wa Mfalme Daudi katika kizazi cha 30.
1. KUINGIA KWA USHINDI
 • Je, watu walitegemea nini mfalme baada ya kuingia kwa ushindi katika mji mkuu?
 • Ingekuwaje kama kitu chochote kingekuwa tofauti na matarajo ya wanafunzi kwa Yesu katika kile umati ungefanya?
 • Angalia kwa makini katika mwendelezo wa mtiririko, ilivyotokea wakati Yesu alipokuwa anakaribia Yerusalemu kwa mara ya mwisho. Ni nani aliyeandaa ukaribisho? Yote yalianzaje? Kwa nini watu walitandaza mavazi yao barabarani? Kwa nini mji mzima ulishtushwa?

  2. MFALME
 • Kwa nini Yesu alipokuwa anakwendaYerusalemu alipanda juu ya punda, na siyo juu ya farasi?
 • Watu wangejuaje ya kwamba Yesu alikuwa ni mwana wa Daudi? (linganisha.20: 31)
 • Yesu alikuwa na tabia gani ya Kifalme?
 • Kwa nini kwa ghafla watu wote hawakuwa na hofu ya kumwita Yesu Mfalme, ingawa vikosi nya majeshi ya Warumi hawakutaka kusikia mambo kama hayo?
 • Hadi hatua hii Yesu ameficha siri kwamba alikuwa mfalme. Kwa nini sasa aitumie kwa manufaa?
 • Kuna tofauti gani kati ya wafalme wa dunia hii na Yesu katika hali hii?
 • Kwa nini Yesu alitakiwa afe kama mfalme?


  3. WATU
 • Je, unafikiri Yesu alikuwa na furaha umaarufu wake kufichwa ghafla? Toa sababu.
 • Unadhani ilikuwa asilimia ngapi watu waliokuwa wakipiga kelele, "Msulubishe!" Baada ya siku tano?
 • Kwa nini hakusimama mtu yeyote katika umati huu na kumtetea Yesu alipokuwa akinyanyaswa?
 • Jinsi gani unaweza kuishi, kama utasimama peke yako na zako ambao wanakupinga?
  4. HOSANNA (maana yake, " Bwana tuokoe / tusaidie!")
 • Kilio cha watu katika mstari wa 9 kinaelezea nini? Cf. maana ya "Hosana".
 • Kwa nini ni sahihi zaidi kupiga kelele, "Nisaidie!" Kwa Mfalme Yesu kuliko "Heko!"
 • Ni nini kinachoshangaza kuhusu mstari wa 11?
 • Tukio hili lina madhara gani juu ya mustakabali wa Yesu hapo baadaye?
  5. WEWE NA MIMI
 • Mambo gani yalikufanya ulie, "Hosanna, nisaidie!" Siku za hivi karibuni / wakati wa ujio huu?
 • Kwa nini hii kilio maandalizi bora kwa ajili ya Krismasi?
  HABARI NJEMA: Soma mstari wa 5 kwa mara nyingine tena na kuweka jina Lako mwenyewe katika nafasi ya "Binti Sayuni".  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster