GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

MBINGU NA NCHI ZITAPITA 24:29-44


Historia: Kuna nadharia nyingi miongoni mwa Wakristo ya kwamba ni utaratibu upi mambo yatatokea wakati Yesu atakapokuja tena katika dunia hii. Katika utafiti huu wa Biblia hatujadili utaratibu wa mambo bali mambo yao wenyewe. Kiongozi anatakiwa kuelezea kwa ufupi kuhusu Nuhu na wakati wake. (37-39, linganisha.Mwanzo.6-7)
1.Kama ukisikia Yesu atarudi leo utajisikiaje?
 • Kuna tofauti gani kati ya kumsubiri Yesu na kungoja kifo?
  2. Ni aina gani ya mabadiliko yatatokea kabla ya kuja kwa Yesu? Jaribu kueleza mambo haya kwa maneno ya kisasa (29). (Nini kinaweza kusababisha giza duniani? Kumbuka pia wakati wa Nuhu.)
 • Ni mategemeo gani yalitarajiwa ambayo hadi sasa hayajatokea?
  3. Ni kwa jinsi gani ujio wa kwanza wa Yesu unatofautina na ule wa pili? Jaribu kupata tofauti kadiri iwezekanavyo (30).
 • Mataifa yote yataomboleza kitu gani wakati Yesu akija tena (30)?
  4. Nini kitatokea kwa Wakristo wakati Yesu atakapokuja tena (31)?
 • Je, ungependa kuwa hai wakati matukio ya mstari wa 31 yatakapotokea? Toa sababu zako.
  5. Je, Yesu alitaka kusema kuhusu nini wakati wa kuwapo kwake kupitia mfano mdogo wa mtini (32-34)? (Je, unafikiri mfano huu anaongea kuhusu Israel ya kileo? Kama ni hivyo, kwajinsi gani?)
  6. Maneno ya Yesu yanamaanisha nini (= Biblia) kwa Wakristo wa kizazi kilichopita (35)
 • Inamaanisha ninii kwako kwamba kuna mambo katika dunia hii ambayo hayatapita kamwe?
  7. Kwanini siku ya kurudi tena ni siri hata kwa Yesu mwenyewe (36)?
 • Maisha yako yatabadilikaje ukijua siku ambayo Yesu atakuja tena?
  8. Jinsi gani rika la Nuhu linafanana na watu wa kileo (38-39)? (Walikuwa wanapendelea nini na hawakupendelea nini?)
  9. Je mistari 40-41 ina maanisha nini? Linganisha wakati wa Nuhu na mstari 31.
 • Fikiria jinsi dunia bila ingekuwa leo kama i mambo yaliyotabiriwa katika mistari hii yatatimia(40-41).
  10. Ni kwa nani ujio wa Yesu unakuwa kama mwizi anavunja nyumba yake (43-44)? Kwa nani itakavyokuwa kama alitamani kukutana na rafiki mpendwa?
 • Je mistari 42 na 44 unatushauri tufanye nini kivitendo?
 • Jinsi gani ujio wa mara ya pili wa Yesu kuwa faraja kwa ajili yetu, badala ya mawazo ya kutisha?  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster