GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

MAPAMBANO KULE GETHSEMANE 26:36-46


Historia: Katika Biblia kikombe kwa maana nyingine ni kikombe kilichojaa ghadhabu ya Mungu, ambayo mwenye dhambi ana gugumia chini (39).
1. Wakati ambao huna furaha, unataka watu wangapi wawe karibu na wewe? (Kwa nini Yesu hakutaka kwenda Gethsemane peke yake?)
 • Wanafunzi hawa watatu wote walikuwa ni wavuvi ambao walikuwa wakifanya kazi mara nyingi wakati wa usiku. Kwa nini hawakuweza kukaa macho kwa saa moja?
  2. Hii ni moja tu na ni wakati ambapo Yesu alizungumzia maumivu yake mwenyewe na huzuni (38). Nini hasa kilikuwa kichungu kwa ajili yake katika hali hii?
 • Kama wewe mwenyewe ulishawahi kuzidiwa na huzuni kiasi cha kufa, ilikutokea katika hali gani?
  3. Watu wengi wameshakutana na vifo vyao pasipo kuonyesha hofu yoyote. Kwanini siyo Yesu? (Iweje kama Yesu angekufa bila kuonyesha hofu yoyote, tabia yake gani imekuwa ishara kwetu?)
 • Ni nini kiinachofanya mtu muongo kuinamisha kichwa chini (39)?
  4. Kwanini Yesu hakuwaomba wanafunzi wake wamwombee (40-41)?
 • Ni aina gani ya majaribu ambayo Yesu aliyazungumzia katika mstari wa 41?
  5. Angalia maombi ya Yesu katika mstari wa 39. Je Yesu alikuwa na mapenzi sawa kama Baba yake wakati huo?
 • Kwa nini sehemu ya kwanza ya sala hii ni muhimu? Kwa nini sehemu ya pili pia ni muhimu?
 • Kitatokea kitu ganikwetu, kama tutaomba sehemu ya pili ya sala hiyo?
  6. Jinsi gani maombi ya Yesu yalibadilika alipoomba kwa mara ya pili (39,42)?
 • Kwa nini Yesu hakuacha baada ya kusali mara moja au mara mbili (39,42,44)?
  7. Je ,atarajio ya Yesu yalibadilika alipokuwa anasali? Kama ni hivyo, kwa njia gani?
 • Je, unafikiri unaweza kumuombeaa mtu unayempenda kuliko wote akuache, kama ni lazima? Toa sababu..
 • Ingekuwaje kwetu kama Yesu angekataa kunywa kikombe cha hasira ya Mungu?
  8. Unapata hisia gani kuhusu habari za Yesu katika mistari 45-46 ikilinganishwa na jinsi alivyokuwa hapo kabla? (Kwa mtulivu sana kutoka hatua hii juu ya hadi kifo chake?)
  9. Ni nini kingetokea kama Yesu angeishia juu ya msalaba bila mapambano haya?
 • Kwa nini ni muhimu kwamba sisi pia tuwe na Gethsemane yetu wenyewe kabla ya Golgotha?
  HABARI NJEMA: Yesu alikuwa ametikiswa kwa sababu alijua kwamba uhusiano wake wa karibu na baba yake itakuwa ungesita wakati huo. Hatutakiwi kunywa kikombe cha ghadhabu ya Mungu kwa sababu Yesu alikunywa kwa ajili yetu.


  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster