GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

1. Noa ALIJENGA SAFINA Mwanzo 6:5-22HABARI YA AWALI: Wakati katikati ya Adamu na Noa, mwanadamu aliishi bila sharia ya Mungu. Sheria tu ilikuwa "Amri kuu" ambayo inasema: Katika yote watendee wengine kama vile ungependa wengine wakutendee (Mathayo.7:12 alihitaji kusubiri mda mrefu watoto wakiume wazaliwe zaidi ya wanaume wengine. Tayari alikuwa na umri wa miaka 500 wakatika watoto watatu wa kiume walizaliwa (5:28-32).
6:5-7 na 11-12.
 • Je unafikiri maisha ya kila siku ya ulimwengu yalikuaje akama inavyoelzewa katika mistari ya 5,11 na12?
 • Linganisha kipindi cha Noa na kipindi chetu.
 • Je unafikiri Mungu ameonyeshwaje katika mistari ya 6-7?
 • Je unafikiri watu walikuwa wakatiri, kwa sababy hawakujua amri za Mungu au kwa sababu zingine?
 • Je Wakristo wanawezaje kuondoa wingi wa ukatiri katika siku zetu?
 • Kwa nini Mungu aliamua kuangamiza hata wanayama pamoja na wanadamu (7,13)?
  6:8-10. Katika mstari wa 9 kuna maneno mawili ya Kiebrania kumwelezea Noa : mtakatifu (tsaddik) na bila lawama (tamim). Utakatifu ni neno muhimu katika Biblia. Inamaanisha mtu ambaye amekubalika mbele za Mungu.
 • Soma kwa makini mistari 8-9 na jaribu kupiga picha katika mawazo yako uhusiano wa Noaa na Mungu na kwa majirani zake. Unaweza kusema nini juu yake?
 • Je Noa ni mtakatifu kwa sababu ya Imani yake au matendo yake? Toa sababu zako.
 • Ebu fikiria jinsi Noa aliweza kutunza Imani yake katika ukatiri ule.
 • Je unafikiri watu walifikiri nini juu ya Noa?
  6:13-16. Safina ilikuwa na ukubwa wa mikono 10000 (108000 square feet) katika mazimulizi tatu; ilikuwa kubwa kama vile tanki la mafuta la wakati huu. Kumbuka haya yalitokea kabla ya karne ya chuma. Katika kipindi cha Noa mtu angeweza kupata chuma kutoka kwa mawe na hilo tu.
 • Badilisha vipimo vya safina kwenda katika meta/futi. Je urefu, upana na kina ulihesabiwaje?
 • Je kulikuwa na tofauti gani kati ya meli na safina?
  6:17-22. Waandishi wengine wa agano la Kale wamefikiri mistari ya 5:32, 6:3, 7:6 kwamba Noa aliweza kujenga safina kwa miaka mia moja. Kama hili ni sawa basi hakuwa na watoto wakati alipoanza jenga safina. Lameki babake alikuwa bado hai;; alikufa miaka mitano kabla ya kumalizika safina.
 • Ebu fikiria hatua mbalimbali za ujenzi. Je Noa alipata shida gani hasa?
 • Unfikiri watu walisema nini juu ya mradi wa meli kubwa iliyojengwa katika nchi kavu.
 • Petero anamuita Noa "mtangazaji wa utakatifu" (2.Petero.2:5) na mwandishi wa Waebrania anatwambia kuwa ali "alihukumu ulimwengu kupitia kwa imani yake" (Waebrania 11:7). Hii inamaanisha kuwat Noa aliwahubiria watu wake akiwa anajenga safina. Inawezekanaje luwa hakuna aliye tubu kwa kipindi cham miaka mia moja ?
 • Je unafikiri baba yake Noa na ndugu zake walifikiri nini juu ya mradi huu wa kunjenga safina (5:28-30)?
 • Mke wa Noa je? Je alikumbana na shida gani?
 • Watoto wa Noa walizaliwa wakatika ujenzi wa safina ulikuwa unaendelea. Linganisha miaka yao ya awali na watoto wa lika yao?
 • Ebu fikiria wasichana ambao waliotoka katika familia ambazo si wacha Mungu lakini walikubaliana kuolewa na watoto wa kiume wa Noa. Ni nini kilichowafanya kufanya hivyo? Fikiria uwezekano mbalimbali.
  Hitimisho:
 • Je umepewa kazi gani na Mungu ambayo unahitaji kuwa mwaminifu kama Noa alivyofanya katika kujenga safina?
 • Tunawezaje kuvumilia matusi ya dunia inayotuzunguka pasipo kukata matumaini?

  INJILI:
  Noa alikuwa mtakatifu machoni pa Mungu na aliamini huruma za Mungu. Hakujenga safina ili aweze kuwa matakatifu lakini tayari alikuwa mtakatifu "akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani." (Waebrania 11:7).

  ***

  Version for printing    
  Downloads    
  Contact us    
  Webmaster