4. YESU NA MJELEDI 2:13-22HISTORIA: Kwa Wayahudi, Hekalu palikuwa ni mahali muhimu zaidi duniani, hata muhimu zaidi kuliko nyumba zao wenyewe. Mfalme Sulemani alipokuwa amejenga hekalu la kwanza; Ezra wa pili. Hekalu la Yesu lilikuwa ni jengo kubwa lililofanikishwa na Mfalme Herode Mkuu. Baada ya kusulubiwa kwa Yesu Yerusalemu lilidumu kati ya miaka thelathini hadi arobaini.

1. Soma Mistari 14-16. Katika tabia za Yesu nini kinakushangaza zaidi??
 • Inachukua muda wa kutengeneza mjeledi wa kamba. Jinsi gani unadhani Yesu alionekanaje wakati akifanya kazi hii (15)?
 • Fikiria ni kelele za aina gani zilisikika hekaluni wakati huo kama ilivyoandikwa katika mstari wa 15.

  2. Kwanini hakuna mtu aliyemzuia Yesu wakati alipokuwa anapindua meza na akipepea fimbo yake?
 • Yesu alichukizwa hasa na nini?
  3. Je, unafikiri kwamba hata katika wakati wetu wenyewe hekalu la Mungu/kanisa linaweza kuwa mahali soko? Toa sababu.
 • Dhabihu zilitolewa katika hekalu ili wale waliotoa sadaka yao waaweze kusamehewa dhambi zao. Jinsi gani mfumo huu umekuwa ukipotoshwa kwa uhakika kwamba hayakuwa na mahusiano na kusudi la Mungu la awali?
  4. Kwa nini Mungu wa Biblia anachukia tafrija ambazo hufanyika tu kwa ajili ya kuonekana?
 • Kwa kufikiria ibada yako mwenyewe, sala, huduma nk, ni kwa kiasi gani ni kwa ajili ya kuonekana?
 • Kwa vitu gani hekalu ndani ya moyo wako litasafishwa na Yesu leo? (Unaweza kujibu kimoyomoyo)

  5. Kuna tofauti gani kati ya Hasira ya Yesu na Hasira yetu (16-17)?
  6. Katika kifungu hiki Yesu ameonesha sambamba kati ya hekalu na mwili wake mwenyewe (19-21). Kwa nini Mungu aliamua kuongeza hekalu moja zaidi katika dunia hii? (Kazi gani ya Hekalu ambayo Yesu alitimiza katika mwili wake wakati alipowambwa juu ya msalaba?)
  7. Fikiria sababu mbalimbali kwa nini Mungu aliweza kuwaruhusu Warumi kuharibu hekalu la Herode kati ya miaka thelathini au arobaini baada ya kusulubiwa kwa Yesu. (Kwa nini hekalu halikuhitajika tena pale Yerusalemu?)
  8. Mfano wa mwili wa Yesu kama hekalu sio tu kutaja sadaka yake msalabani lakini pia katika kanisa la Kikristo, hekalu lake duniani la sasa (1 Wakor.12: 27). Je, unafikiri kanisa katika siku zetu linahitaji matengenezo ya aina hiyo ambayoYesu aliweka juu ya kuunda hekalu la Yerusalemu? Toa sababu.
 • Ni katika hali gani lazima Kiongozi wa kanisa apeperushe mjeledi?

  HABARI NJEMA: Yesu amekuwa hekalu kwa ajili yako - hekalu ambapo dhambi zenu husafishwa. Na siyo hekalu tu lakini pia sadaka: Mwana kondoo wa Mungu azichukuaye dhambi za ulimwengu.


  ***

  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com