5. MFARISAYO NA NYOKA WA SHABA 3:1-16HISTORIA: Ingawa Nikodemo alikuwa ni mtaalamu katika masuala ya dini, yeye hata hivyo hakuingia ufalme wa Mungu, ambayo hayawezi kuonekana. Cha ajabu kwamba Nikodemo anakuja kujadili masuala haya na Yesu ambaye ni mdogo kuliko yeye, na hakuwa na elimu, wala kushika nafasi za juu za kijamii kama yeye mwenyewe. Nikodemo ni mwanachama wa baraza katika Israeli, aina ya mbunge.

1. Kwa uanayoyaona katika maandiko, Nikodemo alikuwa na uimara/udhafu gani? (Nini kinonesha kuhusu Nikodemo kutokukutana na Yesu twakati wa mchana bali usiku?)
 • Nikodemo alikuja kuongea nini na Yesu?

  2. Kwa nini Nikodemo hakuwa na uhakika wa wokovu,hata baada ya kumwamini Mungu katika maisha yake yote?
 • Kwa nini huenda sisi pia tunaweza kukosa uhakika wa wokovu?

  3. Kifuatacho tunaangalia jinsi Yesu alivyoelezea: “kuzaliwa mara ya pili". Ni nini kitabadilika endapo mtu atazaliwa mara ya pili (3-8)?
 • Inamaanisha nini kwamba ni lazima mtu azaliwe“kwa maji na Roho" (5)?

  4. Nikodemo alimuuliza Yesu: “Inawezaje kutokea (kuzaliwa mara ya pili)?" (9). Elezea kwa maneno yako kile Yesu alichomjibu (10-16).

  5. Wakati wa kuelezea kuzaliwa upya, Yesu alitumia mfano wa safari ya Israeli nyikani, tukio ambalo Mungu alimtuma nyoka na sumu kuwaadhibu kwa sababu ya dhambi zao. Baadaye, hata hivyo, Mungu aliwapa dawa: Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipomtazama yule nyoka wa shaba, ataishi. (Hesabu.21:4-9). Je,kuna uhusiano gani kati ya tukio hilo na kifo cha Yesu juu ya msalaba? Fikiria sababu nyingi iwezekanavyo (13-16).

  6. Watu hao waaminio walioamua kumtazama nyoka wa shaba waliamini nini?
 • Biblia inatuambia watu wengi walikufa siku hiyo. Kwa nini watu wote hawakuamini uponyaji ulioletwa na Mungu?
 • Tukio hili katika Agano la Kale linaelekeza kufanya nini kuhusiana na kuzaliwa mara ya pili?

  7. Katika Biblia , nyoka ni alama ya shetaniadui wa Mungu. Unafikiria ni kwanini Yesu aliamua kumtumia nyoka katika uponyaji?

  8. Mstari wa 16 unatufundisha nini kuhusu kuzaliwa mara ya pili?
  9. (Kama kuna muda umebaki:) Ni aina gani ya kutokuelewana umewahi kusikia kuhusiana na kuzaliwa upya? Jadili ukihusisha kifungu hiki.

  HABARI NJEMA: Mungu anatupenda, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.


  ***

  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com