6. MAJI YALIYO HAI 4:5-19MSINGI: Wasamaria walikuwa watu wa damu mchanganyiko na ilikuwa inaonekana hivyo kwa Wayahudi. Kama mwanamke huyu alikuwa katika miaka ya thelathini mwanzoni wakati huo, maana yake ni kwamba yeye alikuwa amebadilisha mpenzi wake angalau kila mwaka mmoja.
1. Kwa nini unafikiri mwanamke huyu alikwenda kuchota maji saa sita mchana na si baada ya jua kutua kama ilivyokuwa desturi kwa wanawake wengine katika Sikari? (Unadhani mwanamke huyu waliona wakati kwenda vizuri peke yake kila siku?)
 • Ni nani alimsindikiza mwanamke huyu?
 • Unafikiria alikuwa na matumaini gani na woga gani kuhusu hatma yake ya baadaye?
  1. Ni kipi kigumu: kuacha wapenzi watano mmoja baada ya mwingine, au kuachwa mara tano? Toa sababu.
 • Unafikiria ilikuwaje kuanza mahusiano mapya kwa mara ya sita, na alikuwa ameshaoa?
 • Alijaribuje kuhalalisha kwamba aliibiwa baba wa watoto wake huko kijijini?

  2. Unadhani mwanamke alijisikiaje/ kuhusu mwanaume kwa ujumla/ kuhusu upendo?
  3. Wanaume Wayahudi waliepuka kuongea na wanawake katika maeneo ya uma na hawakufanya hivyo moja kwa moja.Kwanini Yesu hakuwa na hofu kukosoa fununu hizo?
 • Kwanini Yesu alianza mazungumzo kwa kuanza kuomba msaaada kutoka kwa Yule mwanamke (7)?
  4. Ni kwa njia gani mwanamke anaweza kutokuelewa maneno ya Mungu katika mstari wa 10?
 • Baadaye ni nini kilimfanya mwanamke asikie kiu?
 • Una kiu gani zaidi katika maisha yako? (Unaweza kuJibu kimoyomoyo.)

  5. Soma maneno katika mstari wa 14 jinsi maneno ya Yesu yanavyoongea na wewe. Maneno haya yanamaanisha nini kwako katika hali yako ya sasa?
 • Ni mtu wa aina gani ambaye ana kisima chake chenye maji yaliyo hai na katika moyo wake?
  6. Kwa nini Yesu kujibu ombi la wanawake kwa kusema: “Nenda, nenda ukamwite mume wako uje naye" (15-16)?
 • Nini kingetokea endapo angetangaza mstari wa 18 moja kwa moja kwa mwanamke bila kubadili maneno katika mstari wa16 hadi 17?
 • Kwanini Yesu alitaka kutuonyesha dhambi zetu kabla hajatupa maji yaliyo hai?

  7. Je unadhani mwanamke huyu alijisikiaje baada ya kugundua ya kwambaYesu historia ya maisha yake yote?
 • Mwanamke alielewaje badala ya kujali mambo yake, Yesu alimjali yeye?
  8. Majadiliano yafuatayo, Yesu alimfunulia mwanamke kwamba alikuwa Masihi – ukweli kwamba alificha siri kwa watu wengine wengi. Kwa nini unafikiria alifanya hivyo (25-26)?
  9. Angalia mstari 28 hadi 30. Ilisababisha matokeo gani kivitendo katika maisha ya mwanamke huyu aliyepokea maji yaliyo hai kutoka kwa Yesu? (Mtazamo wa dhambi zake ulibadilikaje? Vipi kuhusu uhusiano wake na kijiji?)

  HABARI NJEMA: Yesu alilia msalabani: “Nina kiu!" (19:28). mmiliki wa kisima cha maji yaliyo hai alikuwa na uzoefu wa makali kiu ya mwili na roho. Ndicho alicholipa kwa maji yaliyo hai ambayo kwake ni sadaka kwetu hata leo.


  ***

  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com