12. MWANAMKE ALIYE SAMAHEWA MENGI Luka 7:36-50


KUMBUKA: Katika utamaduni huu, mwanamke hakutakikana kuonyesha nywele yake hadharani. Mstari wa 44-46 inasimulia jinsi wageni waheshimiwa walikaribishwa nyumbani.
1. Je Mfarisayo Simioni alifikiri nini juu ya Yesu ambaye alimkaribisha nyumani kwake (36, 39, 44-46)?
  • Je unafikiri kwa nini Simioni alikaribisha nyumbani kwake hivyo?
    2. Kila mtu alimfahamu huyu huyu mwanamke kwa sababu alikuwa kahama wa Mjini (37). Ebu jaribu kufikiria juu ya mwanamke huyu alipokuwa anakuwa- Ni nini labda kilimfanya awe kahaba? Fikiria juu ya wezekano mbali mbali.
  • Je mwanamke huyu alikuwa na uzoefu gani kuhusu kupendwa?
    3. Chupa ya marimari iliyojaa marhamu ilikuwa ghali sana. Fikiria sababu mbalimbali kwa nini huyu mwanamke aliweka akiba hela na akanunua chupa ya marimari?
    4. Kwa nini huyu mwanamke alitaka kukutana na Yesu kwa kwa hali na mali? Bila shaka likuwa na ufahamu kuwa asingalipata makaribisho yoyote katika nyumba ya Mfarisayo!
  • Ni nini kilimfanya mwanamke kuamini kuwa Yesu asingalimkataa?
    5. Kwa nini huyu mwanamke alitaka kumgusa Yesu?
  • Nini kitafanyika kama tutaguzwa na mtu Fulani au kitu ambacho hatupendi?
  • Nini kilitendeka Yule mwanamke alipomgusa Yesu?
    6. Ni nini kilimfanya mwanamke alie sana hadi miguu ya Yesu ikaloana?
    7. Je unafikiri ni nini kilikucha kwanza hasa katika hali ya huyu mwanamke: imani yake katika Yesus au upendo wake kwake? Toa sababu zako kutokana na somo hili.
  • Kama wakati Fulani ulisikia kuwa ulimpenda Yesus kwa moyo wako wote, ni katika tukio gani?
    8. Katika mistari ya 41-42 Yesu anatoa mfano wa mkopeshaji. (Dinari mia tano ni sawa sawa na mshahara wa mwaka mmoja na nusu. Dinari hamsini ni sawa sawa na mashahara wa mwezi mmoja.) Dhamni inafaninishwa na deni.. Je Yesu alitaka kumfundisha Simioni kwa mfano huu?
  • Ni dhambi gani za Simioni ambazo Yesu anamaanisha katika mfano huu?
    9. Je ni nini kilitendeka na deni la dhambi ambalo mwanamke alikuwa nayo alimdeni Mungu?
  • Ni nini kilitendeka na deni la dhambi ambalo Simioni alikuwa nayo kwa Mungu?
  • Kwa nini Simioni hakumpenda Yesu?

    10. Yesu ambaye anajua kabisa dhmabi zako zote, anasema kwako sasa maneno ambayo yameandikwa katiika mstari wa 48 na 50. Utamjibu nini?



    ***

    ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com