15. JINA MBINGUNI Luka 10:17-20


TAZAMA: Kwa taarifa ya msingi, soma mstari wa.1 na 9. Mstari huu unazungumza juu ya hali ya maana sana halio ya uamsho wa Galilaya - Je itachukua mwendo gani? Kwa ajili ya swali ya 9
  • tazama Mwanzo .3:15.
    1. Je unafikiri kutatendeka nini kama watu katika Makanisa yetu walikuwa na nguvu kama ya hawa 70 walikuwa nayo?
  • Kwa nini hawa 70 walitoa taarifa moja hasa ya huduma yao kwa Yesu?
    2. Kwa nini watu wanafurahia mamlaka na uwezo?
  • Wanafunzi wake walifurahi juu ya mafanikio yao, kwa nini Yesu hakufurahi pamoja nao?
    3. Kuna tofauti gani kati ya furaha juu ya huduma na furaha juu ya jina lake kuandika katika kitabu cha mbinguni?
  • Kwa nini ni rahisi kufurahia juu ya vitu vya dunia kuliko mambo ya mbinguni?
    4. Je wanafunzi walihubiri kwa wale ambao wanafurahi juu ya kutoa mapepo?
  • Je wanafunzi wanafundisha nini juu ya wale ambao wanafurahi juu ya majina yao kuandikwa mbinguni?
    5. Je nini kifanyike ili kujifunza kufrahia juu ya majina yetu kuandikwa mbinguni?
    6. Ni lini na jinsi gani majina yetu yanawezaje kuandikwa mbinguni?
    7. Ni lini na ni wapi umesikia mambo kama hayo yalitotajwa katika mstari 19 yametendeka?
  • Ni katika hali gani unaweza kuwa na ujasiri kukanyaga nyoka na ngeu?
    8. Kwa nini kitu chochote au mtu yeyote hawezi kudhuru wanafunzi wa Yesu (19)?
  • Je nini ambaco unaogopa kinaweza kudhuru wapendwa wako?
  • Kulingana na somo hili, ni mambo gani ambayo hatuhitaji kuogopa?
  • Ni mambo gani ambayo tunahitaji kuogopa?
    9. Japo wengi wa wanafunzi wa Yesu walifia dini, ni jinsi gani ni wazi kuwa walishinda nguvu za adui?
  • Ni kwa nini Yule nyoka wa zamani (Ibilisi) alikubaliwa kupiga kisigino cha Yesu juu ya msalaba?
    10. Je somo hili linasema nini juu ya huduma yetu?
  • Je somo hili linasema nini juu ya "Nguvu ya uinjilisti"? (Kama hujui neno hilo unaweza kuacha kujibu swali.)

    HABARI NJEMA: Biblia inatuambia kuwa wale ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima mbinguni: " Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. " (Rev.20:15). Kwa sababu Yesu hakutaka litendeke kwetu aliomba kama Musa alivyofanya: " Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao - na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika. " (Kutoka.32:32).


    ***

    ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com