26. MWANA MPOTEVU Luka 15:11-24


KUMBUKA: Nyumba katika Mashariki ya Kati kwa kawaida haiwezi kusimama yenyewe mlimani ila katika sehemu ambayo ína watu wengi vijijini karibu barabrani. Sehemu ya pekee ambayo inaruhusu kuona mbali ni juu ya paa ya nyumba. Kumbuka pia kwamba wanaume wenye heshima katika Mashariki ya Kati hawawezi kukimbia.
1. Kwa nini huyu kijana hakuridhika na maisha yake nyumbani hata ingwa alikuwa na nyumba nzuri na baba mwema?
 • Kama ungelikuwa katika nafasi ya baba je ungejibuje ombi la mwanao?
  2. Kwa nini Mungu hajaribu kumzuia mtu ambaye anataka kuondoka?
  3. Je una maoni gani juu ya maisha aliyoishia huyu kijana akiwa ngambo- alikuwa na furaha au hakuwa nayo?
 • Kwa nini watu wengi siku hizi wanapenda kushi maisha ya aina hiyo- kusafiri ngambo na pesa nyingi bila kujali ya kesho?
  4. Nguruwe ni mnyama ambao si msafi kulingana na Wayahudi. Je unafikiri huyu kijana alijisikiaje katika hali hii ambayo imesemwa katika mistari ya 14-16?
 • Je huyu kijana alikuwa na uchanguzi gani katika hali hii?
 • Je una uchaguzi gani katika hali yako ya sasa inapofika katika upande wa uhusiano wako na Mungu?
  5. Mistari ya 18-19 ina toba ya dhambi ya huyu kijana. Dhambi zake zilikuwa zipi dhidi ya mbinguni? Kwa nini alikiri dhambi zake kwanza?
 • Je alikuwa na dhambi gani mbele ya baba yake?
  6. Ni kwa njia gani huwa tunafikiri kama mwana mpotevu: " sistahili kuitwa mwana wa Mungu " (19)?
 • Ni lini mtu ansitahili kuitwa motto wa Mungu?
  7. Kwa nini kijana hakusema kwa baba yake yote aliyopanga kuyasema (18-19 na 21)?
  8. Je baba alikuwa anafanya nini miaka hii yote (20)?
 • Je unafikiri baba alimsamahe mwanae lini?
 • Ni lini kijana alinaza kuamini katika upendo wa baba yake?
  9. Je Yesu mwenyewe yuko upande gani katika mfano huu?

  HABARI NJEMA: Mfano wa mwana mpotevu unatufundisha kitu juu ya Yesu kwa namna nyingine. Yesu pia aliondoka nyumbani na kutoka kwa baba yake ila kwa sababu zingine: kutimiza mapenzi ya baba yake.Na bado, aliporudi nyumbani katika mwisho wa maisha yake,hakupata makaribisho jinsi aliyopokea mwana mpotevu. Kwa kweli ilifanyika kinyume: Kwa kusema mlango ulipamishwa usoni mwake. Kwa nini?  ***

  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com