27. MWANA MPOTEVU MWINGINE Luka 15:25-32


1. Kwa nini Kijana wa kwanza hakutoka nyumbani kama vile alivtofanya yule mdogo?
 • Huyu mtu alitamani nini kuliko vyote?
 • Kwa nini hakukua na furaha yeyote katika huyu mtoto wa kiume wa kwanza?
  2. Kwa nini mtoto mvulana wa kwanza hakujihesabu kuwa mtumwa kuliko kuwa mridhi (12b, 29, 31)?
 • Kwa nini huyu kaka hakuamini maneno ya babake?
  3. Ni kwa njia gani umejisikia kuwa umefanya kazi ya Mungu bila kupata "hata mbuzi" kama zawadi (29)?
  4. Mtoto wa kwanza alimhabisha baba yake mbele ya kijiji chote kwa kutkataa kufika katika katika karamu. Je unafikiri ni sababu gani hakumpenda baba yake?
 • Jadili kwa mjibu wa mfano huu: Kama hatumpendi Mungu ni sababu gani hasa?
  5. Mtoto wa kwanza alijidanganya kwa kufikiria kuwa alitimiza amri za baba (29). Ni nini mapenzi ya baba kuhusu mwanae?
 • Ni kwa njia gani ahta waumini waaminifu wanaweza kwenda kinyume na Mungu bila kufahamu?
  6. Katika mfano wa Yesu, karamu huashiria mbinguni. Ni nani kulinga na mfano huu anaenda mbinguni na Yule asiye?
  7. Kwa nini Yesus anaonekana kuingia mfano huu ukiwa katikati (32)?
  8. Ebu fikiria hali ambayo ilitenda aubuhi iliyofuata wakati hawa ndugu wawili walienda kufanya kazi shambani - je hisia zao zilitofautianaje?
  9. Je Yesu mwenyewe yuko wapi katika mfano huu?
  HABARI NJEMA: Yesu alikuwa na haki ya urithi sawa na Yule kijana mkubwa alivyokuwa nayo lakini aliacha haki zake. " ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba." (Wafilippi 2:6-8). Kwa njia hiyo Yesu aliwaokowa watu kama vile ndugu mkubwa, ambaye wamefungwa katika utumwa wao. Yesu atawaweka huru - uwapo tu watakubali urithi wa bure.


  ***

  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com