29. KUMI WAPONYWA, MMOJA KAOKOKA Luka 17:11-19


KUMBUKA: Wakati wa Yesu, wakoma waliishi wakitenganishwa kutoka kwa watu wengine. Kama mtu alifikiri kuwa ameponywa alihitaji kujionyesha kwa makuhani (Walawi 13-14). Agano la lote linataja mara kama mara mbili au tatu tu za miujiza ya namna hiyo. Viongozi wanaweza kutazama katika ensaiklopidia juu ya ukoma. Kwa Wasamaria, Wayahudi wakiwadharau kwa kuwa walikuwa wageni na wakapagani.
1. Fikiria siku hawa watu kumi walipogundua kuwa walikuwa wamepata ukoma. NI mawazo ya aina gani yalikuwa katika akili zao kuhusu siku za maisha yao ya usoni kwao wenyewenyewe na familia zao?
(
 • Unaona mfanano gani kati ya ukoma na wakati wa Yesu na kupata UKIMWI leo?)
  2. Je unafikiri ni mambo gani ambayo yalijitokeza katika maisha ya hawa wagonjwa ambao walitengwa?
  3. Je hawa wakoma walitarajia Yesu awafanyie nini- tazama maombi yao katika mstari wa 13?
  4. Mpaka kati ya Samari na Galilaya ni umbali wa 50-60 kilometa kutoka miji ambayo makuhani walikaa. Fikiria sababu mbali mbali kwa nini Yesu hakuwaponya hawa wanaume papo hapo, badala yake akawatuma mbali sana?
 • Ni nini kiliwafanya hawa wanaume kuanza safari ndefu, hata ingawa hawakuwa wameponywa bado?
 • Je unaweza kuwaita hawa wanaume kumi kuwa waaminio au wasio amini mara tu walipoanza safari yao?
  5. Makuhani wa Wakiyahudi hawakutaka kuwa na uhusiano wowote na Wasamaria. Kwa nini Msamaria mmoja alinanza safari na hawa Wayahudi?
  6. Fikiria sababu mbalimbali kwa nini hawa Wayahudi hawakuweza kurudi kwa Yesus ili kumshukuru?
 • Kwa nini Msamaria alirudi kumshukuru Mungu?
  7. Kwa nini alisikitishwa juu wale tisa ambao hawakurudi kwake?
 • Je unafikiri umeweza kumkashirisha Yesu kwa tabia kama zile zile za hawa wanaume tisa walivyoonyesha?
  8. "Imani yako imekuponya" inaweza kutafsiriwa "Imani yako imekuokoa" . Kwa nini alipenda kusema maneno haya kwa Msamaria?
  9. Kuna tofauti gani kati ya Imani inayotafuta uponyaji na Imani inayotafuta Yesu mwenyewe?
 • Kwa nini "Imani ya uponyaji" haiwaokoi watu waliyo nayo?
  10. Je miaka ya kutengwa na aibu ilimaanisha nini kwa hawa Wayahudi tisa, wakati walifikiri juu yao baadaye?
 • Je miaka ya ugonjwa ilimaanisha nini kwa Msamaria?

  HABARI NJEMA: Yesus aliweza kusikia hali ya kutengwa na aibu msalabani jinsi vile wale wakoma walivyojisikia: " Alidharauliwa na kukataliwa na watu;Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko;Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. 4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu,Amejitwika huzuni zetu;Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa,Amepigwa na Mungu, na kuteswa." (Is.53¬:3-4). Hiyo ndiyo gharama ambayo Yesu alilipa kwa muujiza huu.


  ***

  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com