31. NANI MWENYE HAKI? Luka 18:9-14


KUMBUKA: Mfano wa Mfarisayo na mtosha ushuru Hekaluni ni mafundisho ya msingi ya Yesu juu ya Mafundisho ya dini ya kuhesabiwa haki. Mafundisho haya yahajibu swali: Ni nani anayeweza kuwa salama na Mungu na kuweza kwenda mbinguni.? Kumbuka kwamba neon Mfarisayo havikuweza kuingia katika akili za watu kuwa wanafiki wanaojitakia haki, ila mtu ambaye anamwamini na kumwogopa Mungu kweli. Wafarisayo walikuwa upande wa masikini pia. Watosha ushuru kwa upande mwingine walikuwa wasaliti wan chi ya baba yao na waliwanyonya masikini.
1. Ni nini kinaonyesha kwamba hawa wanaume wote walimwamini Mungu?
 • Kwa Wayahudi Hekaluilikuwa ni sehemu ya upatanisho na ni sehemu ambayo waliweza kukutana na Mungu. Jadili: Ni kwa sababu gani Mfarisayo katika somo letu waliweza kwenda Hekaluni?
 • Kwa sababy gani huyu Mtosha Ushuru aliweza kwenda Hekaluni?
  2. Mfarisayo walishukuruni kwa lipi - tazama ombi lake.
 • Kwa nini Mfarisayo hakuweza kutaja chochote ambacho Mungu alimtendea?
 • Je Mfarisayo alikuwa na mafundisha gani ya dini juu ya kuhesabiwa haki? (Tazama ujumbe ulioko mwanzoni.)
  3. Ni wakati gani kama umewahi kuomba kama yule Mfarisayo katika mfano huu? ( Jibu moyoni mwako.)
 • Kitenzi katika lugha ya Kiyuyani katika ombi la Mtosha ushuru una maan ifwatayayo: "Mungu, unihurumie kwa sababu ya kafara ambazo zinatolewa katika hekalu hii." Je mafundisho ya dini ya huyu mtosha ushuru yalikuwa yapi?
  4. Ni kwa njia gani tunaweza kufanana na Mfarisayo katika mfano huu?
 • Dhambi za Mfarisayo zilikuwa nini dhidi ya Mungu na jirani?
 • Kwa nini Mfarisayo hakutambua hata dhambi moja yake?
  5. Imani ya Mfarisayo ilikuwa imara kuliko ile ya mtosha ushuru. Kwa nini imani yao uongo huwa ina nguvu kuliko imani ya kweli?
  6. Ni nani ambaye alijua kuwa miongoni mwa hawa wawili alikuwa mwenye haki walipoondoka Hekaluni? (Singatia somo!)
 • Kwa nini Yesu hakumaliza mfano wake kwa kusema: "Na baada hayo, mtosha ushuru aliweza kufidia wale ambao aliwanyanganya pesa, na kubadilika kuwa mtu mwema."?
  7. Mfarisayo bila shaka aliweza kuharibu maisha ya watu wengi. Ni nini kilifanyika kwa hukumu angalipata kutoka kwa Mungu kwa sababu ya dhambi zake?
  8. Je mwenye kuhesabiwa haki ana changia nini katika kuhesabiwa haki?
 • Je Mungu ana nafasi ipi katika kuhesabiwa haki?
 • Je kafara ina nafasi gani katika kuhesabiwa haki?
  HABARI NJEMA: Kafara ailiyotolewa Hekaluni ni picha ya kifo cha Yesu. Kwa kweli Mtosha ushuru aliomba msamaha kwa ajili ya kafara ya Yesu. Dhambi zake zilihesabiwa kwa Yesu wakati huohuo alipewa haki ya Yesu.


  ***

  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com