4. YESU KUJARIBIWA KATIKA DHAMBI 4:1-11


Historia: Shetani alimjaribu Hawa katika pepo hali iliyopelekea kuanguka dhambini.Kwa namna hiyo hiyo alimjaribu Mungu kipindi cha miaka 40 nyikani na kufanya kuanguka dhambini mara kwa mara.Shetani amejaribu kila mmoja wetu hali iliyopelekea kuanguka dhambini.yesu pia alijaribiwa kwa sababu alikuja kama binadamu na mwakilishi wa binadamu.
1.Fikiria unatakiwa kuwa jangwani kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu bila kuonana na mtu ,kula wala kunywa kitu chochote .Unafikiria ni hali gani itakuwa mbaya zaidi kwako?
 • Je unafikiria Yesu alikuwaje kimwili na kiroho baada ya kufunga kwa siku 40?
 • Ukijaribu majaribu yako na ya Yesu.Kuna tofauti gani?
  2.Mara nyingi tunafikiri ya kwamba Roho Mtakatifu ni kiongozi wa waaminio katika ukamilifu wa maisha.Kwanini basi alimuongoza Yesu ajaribiwe na ibilisi kule jangwani? (1)
 • Kwanni pia Roho Mtakatifu anatuongoza kwenye majaribu ambayo yanapelekea kujaribiwa na shetani?
  3.Jaribu la kwanza linahusu matumizi yetu ya MSINGI:njaa,kiu,mahitaji ya ngono ,usalama n.k (3-4).Kwanini ingekuwa dhambi kwa Yesu kubadili mawe kuwa mikate?
  4.Je unafikiria mwanadamu ataweza kuishi kwa neno la Mungu pekee bila mahitaji ya msingi kutimizwa? (4) Tafadhali jibu kwa uaminifu na kisha utoe sababu.
  5.Jaribu la pili linahusu uhusiano wetu na Mungu(5-7) Mungu angeudhihirishia nini ulimwengu kama angejirusha?
 • Ni kwa njia gani jaribu la pili linakuja maishani mwetu?
  6.Jaribu la tatu inahusu kitu katika imani yetu.Je shetani alisema ukweli katika mstari wa 9? Toa sababu.
 • Dunia ingepata nini kwa muda kama angefanya jinsi shetani alivyomwamuru?
 • Ni faida gani ya muda mfupi twaweza kupata iwapo tutapiga magoti na kusujudu mabwana wengine zaidi ya Mungu aliye hai?
  7.Ni nini ilikuwa silaha ya Yesu alipokuwa anapambana na Shetani?
 • Ni nini silaha yako unapokuwa unapambana na majaribu pamoja na dhambi?

 • 8.Yesu alishinda vita dhidi ya shetani.Kwanini aliadhibiwa adhabu ya kifo ambayo ingewapasa tu wale walioshindwa vita?
 • Angekuwa Mungu wa aina gani kama Yesu asingejaribiwa?
 • Ungekuwa ni aina gani ya mkristo kama usingejaribiwa?
  HABARI NJEMA: Kiongozi asome Waebrania 2:18


  ***

  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com