KIJITABU CHA MAFUNDISHO YA BIBLIA KUHUSU HABARI NJEMA (kwa Afrika)

Beginners
1. YESU ANAKUTANA NA MTUMISHI WA SERIKALI MDANGANYIFU (Mt 9:9 -14)
2. YESU ANAKUTANA NA MTU ALIYEPOOZA (Mk 2:1 - 12)
3. YESU ANAKUTANA NA KAHABA (Luka 7:36 - 50)
4. YESU ANAKUTANA NA TAJIRI (Mk 10:17 - 27)
5. MAFUNDISHO YA YESU: MWANA MPOTEVU (Lk 15:11 - 24)
6. MAFUNDISHO ZAIDI YA YESU: MWANA MPOTEVU MWINGINE (Lk 15:25 - 32)
7. MAFUNDISHO ZAIDI YA YESU: JIRANI YANGU NI NANI? (Lk 10:25 - 37)
8. WAKATI TENDO LISILOWEZEKANA LINATENDEKA (Mk 5:21 - 24 na 35 - 43)
9. MWANAMKE ALIYETOKWA DAMU (Mk 5:25 - 34)
10. . "EFATHA" - FUNGUKA (Mk 7:31 - 37)
11. . MUUMINI ANAYEAMINI SHINGO UPANDE (Mk 9:14 - 29)
12. . KILIO CHA KIPOFU MWOMBAJI (Mk 10:46 - 52)
13. . UPENDO HAUTAWEZA KUSHINDWA (Mk 14:1 - 9)
14. . KICHEKO KIITWACHO HUKUMU YA YESU (Mk 15:1 - 15)
15. . YESU ANAKUTANA NA WAHALIFU WAWILI (Lk 23:32 - 43)
16. . KUFUFUKA KUSIKOAMINIKA (Mk 16:1 - 8)
17. . YESU ANAKUTANA NA MWANAFUNZI MWENYE MASHAKA (Yn 20:19 - 29)

Print all lessons

? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com


1. YESU ANAKUTANA NA MTUMISHI WA SERIKALI MDANGANYIFU (Mt 9:9 -14)
TAARIFA MUHIMU: Kula pamoja kulikuwa ishara ya urafiki miongoni mwa Wayahudi wakati wa Yesu. Watu wa dini waliwadharau watoza ushuru kwa sababu walikusanya ushuru kwa sababu ya wanajeshi wakaaji wa Warumi. (MONGOLIA). Hawa ni sawa na Wamongolia wanaoishi upande wa Uchina ilhali Mongolia ilikuwa chini ya utawala wao. Isitoshe, watosha ushuru waliwatosha watu ushuru kupita kiasi na waliyachukua masalio. Mathayo alikuwa amefundishwa kuhusu Amri Kumi katika Biblia. Kwa mfano: Usiibe! Mfarisayo alikuwa kiongozi wa kidini.

1. Je, mtu anaweza kuwa mwenye furaha kama hana pesa za kumwezesha kuishi kwa starehe?
 • Yafikirie maisha ya Mathayo, mtosha ushuru. Ni mambo gani ambayo hayakuwa mazuri katika maisha yake licha ya mshahara wake mkubwa?

 • Mathayo aliweza kufikiria nini kuhusu Mungu na Amri zake alipokuwa anaifanya kazi yake kama mtosha ushuru?

 • Kwa nini ni kawaida kwa watu kuzichukua pesa na vitu vinginevyo visivyokuwa vyao wakati huu wetu?

  2. Mathayo alitarajia Yesu aseme nini alipoingia ofisini mwake?

 • Kwa nini Yesu alimwuliza Mathayo: "Ungependa kuwa mfuasi wangu?"

 • Mathayo alifikiria nini wakati kiongozi mashuhuri wa kidini alipomwuliza ajiunge na wafuasi wake?

 • Kwa nini Yesu alitaka kuwa na mtosha ushuru mmoja miongoni mwa wanafunzi wake ingawa alijua kuwa angekosolewa kwa kufanya hivyo?

  3. Wenzi wa Mathayo walifikiria nini alipoiacha kazi yake ghafla bila hata kuviondoa vitu vyake kutoka katika dawati lake?

 • Nini kilichomtia moyo Mathayo kuiacha kazi yake nzuri na mapato ya mara kwa mara?

  4. Mathayo alipokea nini badala ya vitu alivyovipoteza alipomfuata Yesu?

 • Maisha ya mke na watoto wake yalibadilikaje wakati aliyewapatia riziki yao ya kila siku alikuwa mfuasi wa Yesu?

 • Kwa nini Mathayo alitaka kuipanga karamu ya chakula ambapo aliwaalika Yesu na wenzi wake wa zamani (10)?

  5. Ni akina nani katika jamii yetu ambao watu wa heshima hawataki kuchangamana nao (11)?

 • Kwa nini Yesu alitaka kuchangamana na watu wa kila aina?

  6. Kwa nini Mafarisayo hawakumkosoa Yesu moja kwa moja bila kuogopa na badala yake waliwakosoa wanafunzi wake (11)?

  7. Yesu alimaanisha nini katika haya ya 12 - 13?

 • Unastahili kuwa wapi kati ya vikundi hivi viwili: cha haki au cha wenye dhambi? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

  8. Baadaye Mathayo hata aliuandika wasifu wa Yesu: Injili ya Mathayo. Unafikiri alisikitika kwa kuviacha vitu vyote na kumfuata Yesu? toa sababu zako.

  9. MASWALI YA HABARI NJEMA: Sasa Yesu anakuambia mambo haya mawili: "Nifuate!" na "Sikuja kuwaita watu wema bali wenye dhambi." Unamjibu nini?

 • (Kwa kila mshirika kujibu): Ni jambo gani muhimu zaidi ulilojifunza kutokana na haya Mafundisho ya Biblia?


  ***  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  2. YESU ANAKUTANA NA MTU ALIYEPOOZA (Mk 2:1 - 12)  TAARIFA MUHIMU: Nyakati za Yesu, nyumba zilijengwa kwa mawe ya chokaa na vigae na zilikuwa na mapaa bapa. Kulikuwa na ngazi nje ya nyumba zilizoelekea paani. Kawaida, mtu hupooza akiwa na umri wa makamu au zaidi kwa sababu ya utokaji wa damu katika ubongo. Mtu aliyepooza hawezi kutembea wala kuongea. Mwana wa Adamu ni jina alilolitumia Yesu alipojizungumzia mwenyewe.

  1. Unafikiri mtu anaweza kufurahi iwapo amelala kitandani mwake akiwa haongei wala hatembei?

 • Ni malezi ya aina gani aliyoyahitaji mtu huyu katika maisha yake ya kila siku?

 • Yafikirie maisha ya kila siku ya mlezi wa mtu huyu?

  2. Wayahudi wote walimwamini Mungu nyakati hizo. Mtu huyu alifikiria nini kuhusu Mungu na imani baada ya kupooza?

  3. Katika aya ya 5 tunaweza kuona kuwa mtu huyu alikuwa na dhambi katika dhamiri yake.

  Ni dhambi za aina gani ambazo mtu anaweza kuzifanya anapokuwa hawezi kutembea au kuongea?

 • Kwa maoni yako: je, uchungu na ugonjwa vinaweza kutubadilisha ili tuwe binadamu wema au tuwe binadamu wabaya zaidi?

  4. Shida ya kumsafirisha mtu aliyepooza kwa blanketi kupitia mjini ni ipi?

 • Kwa nini watu wengine hawakutoka nje ya nyumba ili wamruhusu huyu mtu maskini apelekwe kwa Yesu (4)?

 • Kwa nini marafiki zake wanne hawakurudi nyumbani baada ya kugundua kuwa ilikuwa vigumu kwao kuingia kupitia mlangoni?

  5. Watu hawa wanne walikuwa na uhusiano upi na mtu huyu aliyepooza? Fikiria uwezekano mbali mbali (3).

 • Ni hadhari zipi zilizochukuliwa mtu huyu alipopelekwa juu ya paani? (Itazame taarifa muhimu kuhusu jinsi nyumba ilivyojengwa).

 • Ni vifaa gani vilivyohitajika ili kuweza kulivunja paa la nyumba? Watu hawa wanne walivipata wapi?

 • Ni maoni yapi yaliyosikika kutoka chumbani kutoka paa la nyumba lilipokuwa linavunjwa?

  6. Wanaume wanne walikuwa wamemleta rafiki yao kwa Yesu ili aweze kuponywa. Kwa nini Yesu alimsamehe dhambi zake kwanza (5)?

 • Kwa nini Yesu aliufuata utaratibu huu: kwanza kusamehe dhambi halafu kuuponya ugonjwa?

 • Ilimaanisha nini kwa mtu huyu aliyepooza kwamba alisamehewa dhambi zake zote alizokuwa amezifanya hapo awali?

  7. Ifikirie hali ambayo unamwendea Yesu na kumwuliza akusuluhishie shida yako kubwa zaidi. Iwapo atakujibu: "Mwanangu/binti yangu, dhambi zako zimesamehewa." Je utafurahi au utahuzunika?

 • Iwapo ungeweza kuchagua, ungechagua nini: dhamiri nzuri au suluhisho la shida yako kubwa zaidi?

 • Mtazamo wa mtu aliyepooza ulibadilikaje kuhusu ugonjwa wake alipogundua kuwa angeenda mbinguni mwishowe?

  8. Katika aya ya 5, Yesu hazungumzii kuhusu imani ya mtu aliyepooza bali ile ya marafiki zake. Ni wazi kuwa mtu huyu mwenyewe hakuwa na imani yoyote kabla ya kukutana na Yesu. Itaje aya ambapo unafikiri kuwa alianza kumwamini Yesu.

 • Kwa nini walimu wa sheria hawakuamini kuwa Yesu angeweza kuwasamehe watu dhambi zao (7 - 8)?

  9. Yajibu maswali ambayo Yesu anayauliza katika aya ya 9.

 • Ilimgharimu nini Yesu kumtibu mgonjwa huyu? Ilimgharimu nini kumsamehe dhambi zake?
 • Ungefikiria nini kuhusu Yesu kama ungekuwa umeshuhudia kwa macho yako yale yanayoelezewa katika aya ya 10-12?

  10. MASWALI YA HABARI NJEMA: Iwapo moyo wako unakushtaki kwa kosa ulilolitenda, sikiliza akwambiayo Yesu: "Mwanangu/binti yangu, dhambi zako zimesamehewa!" Ili kuigharamia ahadi yake, ilimpasa Yesu afe msalabani. Ahadi yake ina maana gani kwako leo? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

 • (Kwa kila mshiriki kujibu): Ni jambo gani muhimu zaidi ulilojifunza kutokana na haya mafundisho?

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  3. YESU ANAKUTANA NA KAHABA (Luka 7:36 - 50)  TAARIFA MUHIMU: Aya ya 44-46 zinaelezea jinsi mgeni mashuhuri alivyopokewa nyakati za Yesu. Watu walikula wakiwa wameketi sakafuni; hiyo ndiyo sababu miguu michafu ya jirani ingemfanya mtu aipoteze hamu yake ya chakula. Kumbuka kuwa katika desturi za Wayahudi, mwanamke hakuzionyesha nywele zake mbele za wageni. Maana ya Mfarisayo ni muumini wa dhati wa Mungu. Simoni si yule aliyekuwa mwanafunzi wa Yesu.

  1. Kwa maoni yako, kahaba anaweza kuishi maisha ya furaha? Zitoe sababu zako.

 • Watu wote katika mji huo walimjua mwanamke huyu aliyeuuza mwili wake wenyewe. Ufikirie uwezekano mbali mbali uliomfanya msichana huyu kuwa kahaba.

  2. Ni maadili gani yaliyokuwa muhimu katika maisha ya Simoni Mfarisayo?

 • Kwa nini Simoni hakumwuliza mmoja wa watumishi wake aioshe miguu ya Yesu; isitoshe, alikuwa amemwalika Yesu kuwa mgeni wake (36, 44 - 46).

 • Ni sababu zipi zilizokuwa zimemfanya Simoni amwalike Yesu kwake kwa chakula? Ufikirie uwezekano mbali mbali (36).

  3. Mwanamke anayezungumziwa aliwezaje kupenyeza hadi katika nyumba ya Simoni na hadi katika chumba cha kulia chakula? Ufikirie uwezekano mbali mbali.

 • Marimari yenye marhamu yalikuwa ya bei ghali. Mwanamke huyu aliyapataje marimari haya au alikuwa ameyanunua kwa sababu gani? Zifikirie sababu mbali mbali.

  4. Kwa nini mwanamke huyu alitaka sana kukutana na Yesu hadi akathubutu kuingia katika nyumba ya Mfarisayo, akijua wazi wazi kuwa angeshindwa?

 • Nyakati hizo watu wa dini hawakuchangamana na watenda dhambi. Ni nini kilichomfanya mwanamke huyu awe na matumaini kuwa Yesu angekuwa tofauti?

  5. Kwa nini mwanamke huyu alitaka kumgusa Yesu (38)?

 • Ni nini kinachofanyika iwapo panya, nyoka au mtu tunayemchukia anatugusa?

 • Mwanamke huyu alikuwa na uamuzi gani kutokana na ukweli kwamba Yesu hakuuogopa mguso wake?

  6. Kisia lini mara ya mwisho ambapo mwanamke huyu alikuwa amelia.

 • Ni machozi ya kiasi gani yanayohitajika ili mtu aweze kuiosha miguu ya mtu mwingine?

 • Ni nini kilichomfanya mwanamke huyu alie sana hadi miguu ya Yesu ikaloa?

 • Kwa nini mwanamke huyu hakuikausha miguu ya Yesu kwa skafu au pindo la nguo yake badala ya nywele zake?
 • Mwanamke huyu hakulinena hata neno moja wakati wa chakula; je, tabia zake zilionyesha nini?

  7. Katika aya ya 41 - 42, Yesu anautoa mfano mfupi kuhusu mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili. Mkopeshaji ni Mungu lakini Yesu anamsema nani anapowazungumzia hawa wadaiwa waiwili?

 • Yesu anazifananisha dhambi na deni. Deni la dinari 500 linalingana na mshahara wa mtu wa kawaida kwa mwaka mmoja na nusu. Deni la dinari 50 linalingana na mshahara wa mwezi mmoja na nusu. Hizi zingekuwa kiasi gani cha pesa katika sarafu zetu?

 • Hebu tuchukulie kuwa kila dhambi uliyoifanya inalingana na deni, tuseme yuro 10 50/shilingi 1,000. Unamwia Mungu pesa kiasi gani kufikia sasa? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

  8. Kwa nini Simoni alimdharau Yesu na mwanamke yule?

 • Kwa nini ni rahisi kuziona dhambi za wengine kuliko zetu?

  9. Lipi lililotokea kwanza: Mwanamke huyu aliamini kwanza kuwa dhambi zake zilikuwa zimesamehewa au alimpenda Yesu kwanza ndipo dhambi zake zikasamehewa? Zitoe sababu zako kutoka aya za 42 - 43, 47.

 • Nani aliyelipa deni ambalo mwanamke huyu alimwia Mungu?

 • Ni nini kilichotokea kwa deni ambalo Simoni alimwia Mungu?

 • Yesu aliyalipa madeni ya watu wote kwa sarafu gani?

  10. MASWALI YA HABARI NJEMA: Yesu anazijua dhambi zako zote lakini licha yake anakwambia: "Umesamehewa dhambi zako zote. Imani yako imekuokoa. Nenda kwa amani!" (Aya ya 48 na 50). Ni yeye tu aliye na haki ya kuyasema maneno haya kwa sababu alilipia- deni ya dhambi zako kwa damu yake. Unamjibu nini? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

 • (Kwa kila mshirika kujibu): Ni jambo gani muhimu zaidi ulilojifunza kutokana na haya mafundisho?

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  4. YESU ANAKUTANA NA TAJIRI (Mk 10:17 - 27)  TAARIFA MUHIMU: Tawasifu zingine za Yesu zinatuambia kuwa azungumziwaye katika kifungu hiki alikuwa kijana na bado alikuwa mbunge (mjumbe wa baraza kuu). (Mt 19:22 na Lk 18:18). Mtu huyu alijua kutoka Biblia kuwa baada ya kifo chake angeurithi uzima wa milele au angeingia jahanamu. Kumbuka kuwa katika desturi za jamii hii, mwanaume hakumkimbilia au hakumpigia magoti mwanaume mwenzake.

  1.Unafikiriaje: mwanadamu anaweza kuwa na furaha bila kujua kitakachotendeka kwake baada ya kifo chake?

 • Ni nini kilichomfanya huyu kijana mbunge kuzionyesha tabia hizi zisizokuwa za kawaida za kumkimbilia na kumpigia magoti Yesu (17)?
 • Je, mtu huyu alimchukulia Yesu kama Mungu au kama mtu mwenye busara isiyokuwa ya kawaida (17b - 18)?

  2. Kwa nini mtu huyu hakuwa na hakika dhidi ya wokovu wake ingawa alikuwa amezitunza Amri za Mungu maishani mwake?

 • Kwa nini daima hatuna hakika ya kwenda mbinguni baada ya kifo chetu?

 • Unafikiri mtu anaweza kuwa na hakika ya kwenda mbinguni baada ya kifo chake? Zitoe sababu zako.

  3. Ni amri ipi iliyo ngumu kuiweka ambayo Yesu anaitaja hapa (19)?

 • Wanasiasa wengi hujaribiwa kuwa fisadi katika mambo ya pesa na ngono. Mtu huyu aliwezaje kuhepukana na majaribu haya yote (20)?

 • Kumbuka kwamba kulingana na Yesu, amri hizi lazima ziwekwe sio tu kwa matendo bali pia kwa maneno na mawazo. Je, unafikiri kijana huyu alifaulu kufanya hivyo (19 - 20)?

 • Kwa kweli ungeyasema maneno sawa na yale aliyoyasema kijana huyu katika aya ya 20?

  4. Kijana huyu mwanasiasa alipungukiwa kitu kimoja. Ifupishe aya ya 21 na useme kitu alichokuwa amepungukiwa.
  5. Yesu anaitaja hazina ya mbinguni katika aya ya 21. Mtu anawezaje kujiwekea hazina mbinguni?

 • Kuna tofauti gani kati ya hazina ya mbinguni na hazina ya ulimwenguni?

 • Ni vitu gani ambavyo vijana wa nyakati hizi zetu wanavitukuza kama "hazina" yenye thamani kubwa zaidi?

 • Ni nani au ni nini hazina yako nzuri kuliko zote? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

  6. Labda kijana huyu alikuwa na familia au wazazi wazee ambao aliowatunza. Ni nini kingetokea kama angekuwa amemfuata Yesu katika aya ya 21?

 • Jifikirie mwenyewe kuwa katika hali aliyokuwa nayo kijana mwanasiasa huyu. Ungeamini kuwa Mungu angeweza kuitunza familia yako hata baada ya wewe kuiacha nyumba yako na mali zako zote?

 • Je, unaweza kufikiria kuziacha hazina zako za ulimwenguni iwapo kufanya hivyo kungekuwezesha kwenda mbinguni? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

  7. Kulingana na aya ya 21, Yesu alimpenda huyu kijana mwanasiasa. Kwa nini basi aliyasema maneno hayo magumu yaliyomfanya aondoke?

  8. Baada ya kugundua kuwa hasingaliweza kuyatimiza yale Yesu alimtaka ayafanye, ni nini kingine ambacho mtu huyu angekifanya kuliko kumwacha Yesu (22)?

 • Labda Yesu angeweza kujibu nini kama mtu huyu angeungama kwake: "Nisamehe kwa kupenda mali kuliko wewe!"
  9. Yafikirie maisha ya kijana huyu kuanzia sasa na kuendelea: Alikuwa na furaha? Alifikiria nini kuhusu kifo chake?

 • Lilinganishe jibu ambalo Yesu alimpa kijana huyu na jibu alilompa Petero (aya ya 21 na 27). Je, kimsingi jibu lake lililingana au lilikuwa tofauti?

 • Ni nani atakayekwenda mbinguni baada ya kifo chake?


  10. MASWALI YA HABARI NJEMA: "Kwake Mungu mambo yote yanawezekana" ina maana kuwa: Yesu aliiacha hazina yake mbinguni na akaja humu ulimwenguni kuteswa na kufa ili uweze kukipata kibali cha kuingilia mbinguni. Kosa kubwa alilolifanya kijana huyu ni kumwacha Yesu. Je wewe utafanya nini? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

 • (Kwa kila mshirika kujibu): Ni jambo gani muhimu sana ulilojifunza kutokana na mafundisho ya kifungu hiki wakati huu?

  ***

  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  5. MAFUNDISHO YA YESU: MWANA MPOTEVU (Lk 15:11 - 24)  TAARIFA MUHIMU: Hadithi iliyotolewa na Yesu inaitwa mfano. Urithi haukupokewa wakati baba alikuwa angali hai. Nyakati za Yesu, nyumba haikusimama peke yake kilimani bali ilijengwa kijijini karibu na barabara nyembamba. Pahali pa pekee ambapo ungeweza kusimama ili uone nje ya kijiji palikuwa juu ya paa la nyumba (20). Jinsi tulivyokwisha kusema awali, wamaume hawakuwakimbilia wanaume wenzao katika sehemu hizo za ulimwengu.

  1. Kijana anaweza kufurahi iwapo wazazi wake watauwekea uhuru wake mipaka?
 • Kwa nini mwana mdogo hakuwa na furaha ingawa alikuwa na makao mazuri na baba mwema?

 • Ungekuwa katika nafasi ya baba, ungemjibu mwanao nini kuhusu ombi lake (12a)?

  2. Kwa nini baba aliyaficha masikitiko na mahangaiko yake ingawa alifahamu vizuri kile ambacho kingetokea iwapo angemruhusu mwanawe atoke (12b)?

 • Katika mfano huu, Baba ni Mungu. Kijana anaweza kuwa mtu ambaye amemwacha Mungu baada ya kumwamini au baada ya kubatizwa kwa jina lake. Kwa nini Mungu hamzuii mwanawe anayemwacha?

  3. Kwa nini vijana wengi wa siku hizi wanavutiwa na maisha mtindo ya kijana huyu - wanapokuwa ng’ambo peke yao bila wajibu wala pesa nyingi za matumizi?

 • Kijana huyu alizitumiaje pesa za babake: tazame aya ya 13 na 30.

 • Kwa nini kijana huyu hakupata marafiki wa kweli ambao wangebaki naye hata baada ya kuishiwa?

  4. Nguruwe alichukiliwa kuwa mnyama mchafu miongoni mwa Wayahudi. Kijana huyu alifikiria nini alipoitafuta kazi ya kuwalisha nguruwe (14 - 15)?

 • Kwa nini kijana huyu hakuruhusiwa hata kukila chakula cha nguruwe ili kujishibisha (16)?

  5. Ni nini kilichomfanya kijana huyu "kujirudi" badala ya kujinyonga alipokuwa katika hali hiyo ya kuikata tamaa (17)?

 • Katika aya ya 18-19, utalipata ungamo alilolipanga kijana huyu kumwambia babake. Dhambi zake kwa babake zilikuwa zipi?

 • Ni dhambi zipi ambazo mwana huyu alikuwa amezifanya "dhidi ya mbinguni" (18)?

 • Ni dhambi zipi ambazo umezifanya: a) dhidi ya mbinguni na b) dhidi ya wazazi? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)
  6. Kwa nini kijan huyu hakutarajia kumwuliza babake amkubali kama mwanawe (19)?

 • Kwa kawaida ni watu wa aina gani wanaofikiria kuwa hawastahili kuitwa wana wa Mungu (19)?

  7. Baba aliweza kufikiria nini alipomwona mwanawe akiikokota miguu yake barabarani kurudi kijijini akiwa hana viatu na isitoshe alivalia matambara (20)?

 • Ni nini kilichomfanya baba amtambue mwanawe kutoka mbali (20)? (Tazama taarifa muhimu.)

 • Unafikiri baba alikuwa akifanya nini miaka hii yote mwanawe alipokuwa mbali naye (20)?

  8. Kwa nini mwana huyu hakumwambia babake mambo yote aliyokuwa ameyapanga kumwambia (18b - 19 na 21)?

 • Maneno na tabia za baba zilimwambia nini mwana huyu (22 - 23)?

 • Baba alimsamehea mwanawe lini? Taja aya.

 • Ni lini mwana huyu alianza kuuamini upendo na msamaha wa babake? Taja aya.

 • Maneno ya baba yalimaanisha nini katika aya ya 24?

  9. Upendo wa Mungu unatofautianaje na ule wa wanadamu?

 • Mfano huu unafundisha nini kuhusu ubadilikaji?


  10. MASWALI YA HABARI NJEMA: "Mwanangu alikuwa amekufa, kumbe yu hai." Pia Yesu aliiacha nyumba ya Baba yake na akaja humu ulimwenguni si kwa kuyaasi mapenzi ya Baba yake bali kuyatimiza. Wakati wa kurudi nyumbani, mlango wa mbinguni ulifungwa usoni pake na ilimbidi alie: "Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?"Kwa nini kijana alikaribishwa namna ambavyo Yesu angekaribishwa katika mfano huu? Na kwa nini Yesu alikataliwa namna ambavyo mwana huyu angekuwa amekataliwa?

 • (Kwa kila mshirika kujibu): Ni jambo gani muhimu sana ulilojifunza kutokana na mafundisho ya kifungu hiki wakati huu?

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  6. MAFUNDISHO ZAIDI YA YESU: MWANA MPOTEVU MWINGINE (Lk 15:25 - 32)  TAARIFA MUHIMU: Kusema kweli, baba alikuwa ameiacha nusu ya mali yake kwa mwanawe mkubwa wakati kijana mdogo aliupokea urithi wake (aya ya 12). Halikuwa kosa la baba kwa mwanawe kutoyaamini maneno yake.

  1. Kijana anaweza kufurahi iwapo anahisi kuwa wazazi wake hawampendi?

 • Kwa nini kijana mkubwa hakutoka nyumbani aende katika nchi za mbali na nduguye, iwapo alikuwa hayafurahii maisha yake nyumbani?
 • Unafikiri kijana mkubwa alikitamani kitu gani kuliko kitu chochote katika maisha yake?

  2. Kwa nini mwana mkubwa alijiona mwenyewe kama mtumwa ingawa babake alikuwa amemwahidi nusu ya mali yake (12b, 29, 31)?
 • Iwapo baba katika mfano huu ni Mungu na kijana mdogo ni mtu aliyetengana na imani yake ya Kikristo, unafikiri kijana mkubwa anamwakilisha nani?

 • Je unafikiri baba huyu aliwatendea wanawe haki?

 • Je unafikiri daima Mungu hututendea sisi watu wake haki?

  3. Kijana mkubwa alikuwa akifikiria nini alipokuwa akifanya kazi shambani kila siku?
 • Iwapo umejihisi sawa na alivyojihisi mwana huyu katika aya ya 29 - 30, ni katika hali gani hayo yalitokea?

 • Ni sababu gani halisi ambayo ilimfanya kijana mkubwa kutowafanyia marafiki zake sherehe (29)?

 • Baba angechukuliaje iwapo kijana mkubwa angekuwa amemchinja mbuzi, kondoo au ndama na kusherehekea na marafiki zake (30 - 31)?

  4. Ni sababu gani kubwa iliyomfanya kijana mkubwa kuwa na hasira katika hali hii (27 - 28)?

 • Kijana mdogo alikuwa amemwaibisha babake mbele ya kijiji kizima na sasa kijana mkubwa anafanya vivyo hivyo? Kwa nini babake hakukasirika?

 • Unaipata picha gani kumhusu huyu baba katika aya za 28b na 31 - 32?

 • Unaipata picha gani kumhusu Mungu katika aya za 28b, 31 - 32?
  5. Kwa nini kijana mkubwa hakumpenda babake ingawa daima baba alikuwa mwema kwake?
 • Jadilianeni katika msingi wa mfano huu: Ni sababu gani inayoweza kutufanya tusimpende Mungu?

  6. Kijana mkubwa alifikiria kuwa daima aliyatimiza mapenzi ya babake (29). Baba alitarajia nini kutoka kwa mwanawe kuliko vyote?
 • Ni nini kituonyeshacho kuwa kijana mkubwa kamwe hakumpenda nduguye mdogo (30)?
 • Kijana mkubwa alimpenda nani?
  7. Kwa nini Yesu aliukatisha mfano wake bila kutuambia iwapo Kijana mkubwa alihudhuria sherehe au la (28, 32)?
  8. Katika mfano wa Yesu, daima karamu inamaanisha mbinguni. Kulingana na mfano huu, ni nani atakayeingia mbinguni mwishowe?

 • Litakuwa kosa la nani ikiwa mtu fulani hataingia mbinguni kulingana na mfano huu?

  9. Ifikirie hali ambapo vijana hawa wawili walikwenda shambani asubuhi iliyofuatia. Hali ya ndugu mkubwa ingekuwaje na ya ndugu mdogo je?

 • Watu wote duniani wanafanana na ndugu mkubwa au mdogo katika mfano huu. Unafikiri unafanana na yupi? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

  10. MASWALI YA HABARI NJEMA: Yesu anakwambia: "Vyote vilivyo vyangu ni vyako." Msalabani, alikuweka mahali mbinguni. Alikupatia urithi huu siku ile ulibatizwa. Ndugu mkubwa hakuiamini ahadi hii lakini aliushughulikia urithi wake kama mtumwa. Je, unaamini kuwa utaupokea urithi wako wa mbinguni bure au unajaribu kuupokea kwa matendo yako mema? Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

 • (Kwa kila mshiriki kujibu): Ni jambo gani muhimu sana ulilojifunza kutokana na haya Mafundisho ya Biblia?
  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  7. MAFUNDISHO ZAIDI YA YESU: JIRANI YANGU NI NANI? (Lk 10:25 - 37)  TAARIFA MUHIMU: Barabara iliyopitia mlimani kati ya Yerusalemu na Yeriko ilikuwa ya umbali wa kilomita 30 na ilikuwa hatari sana kwa sababu ya majambazi wa barabara kuu waliowavizia wasafiri. Maana ya Mlawi ni mtu aliyefanya kazi hekaluni kama mhudumu wa ofisi. Nyakati za Yesu, Wayahudi walichukiana sana na Wasamaria walioishi katika nchi moja nao. (Uchukue mfano kutoka katika nchi yako. KENYA: Ni rahisi kuuelewa mfano huu iwapo unafikiria kuwa watu wengine wote katika hadithi hii ni Wakenya isipokuwa Msamaria - ni mfuasi wa "Mungiki". UGANDA: Ni rahisi kuuelewa mfano huu iwapo unafikiria kuwa watu wengine wote katika hadithi hii ni Waganda isipokuwa Msamaria - ni mfuasi wa Yusufu Kony wa Jeshi la upiinzani la Bwana"LRA".)

  1. Mtu anaweza kufurahi iwapo hajali kabisa jinsi wenzake watesekavyo lakini anajifikiria tu mwenyewe na familia yake?

 • Ni mara ngapi unazitoa pesa zako kwa ajili ya kuwasaidia wenye haja?

  2. Katika mafundisho yetu yaliyotangulia, tulijifunza kuhusu mwanasiasa mmoja aliyemuuliza Yesu swali sawa na aliloliuliza mwalimu wa sheria katika hiki kifungu. Njia ya kwendea mbinguni ni ipi kulingana na anachokisema Yesu katika hiki kifungu (25 - 27)?

 • Uwezekano wako wa kwenda mbinguni ni upi iwapo masharti ni yale anaoatoa Yesu katika aya ya 27?

  3. Yesu anautoa mfano wa mtu aliyepigwa na genge la majambazi na akaachwa akiwa mahututi. Yafikirie mawazo ya majeruhi huyu alipokuwa amelala kando ya barabara saa baada ya saa (30).
 • Je, mke na watoto wake walikuwa wakifikiria nini wakati hakuwasili nyumbani mda ule aliokuwa amewaahidi?

  4. Kulikuwa na hatari gani kwa wapita njia kumsaidia majeruhi huyu?

 • Kuhani na Mlawi walikuwa njiani kwenda kuutekeleza wajibu wao wa kidini hekaluni. Unafikiri watu hawa wawili wangefanya nini iwapo majeruhi angekuwa mtoto wao wenyewe?
 • Zifikirie sababu nyingi uwezavyo zilizowafanya hawa watu wawili kukataa kumsaidia mwathiriwa wa uhalifu huu (31 - 32).

 • Unafikiria mwenywe ungefanya nini iwapo ungempata mtu akiwa katika hali hiyo?

  5. Je, Kuhani na Mlawi waliifafanuaje amri ya upendo waliyokuwa wamefundishwa tangu walipokuwa watoto? Utazame aya ya 27.

 • Ungefikiria nini kuhusu mtu aliyesema hivi: "Ninampenda Mungu kwa moyo wangu wote lakini kwa bahati mbaya sina nafasi ya kuwasaidia watu wengine."

  6. Iwapo Msamaria angepita na ampate Myahudi majeruhi, angeziteteaje tabia zake? Itazame taarifa muhimu.

 • Ni jinsi gani ambavyo Msamaria alifanya zaidi ya kile ambacho yeyote angekitarajia katika hali hii (33 - 35)?

  7. Dinari mbili zilikuwa sawa na mshahara wa kazi za siku mbili, kumaanisha sehemu moja kwa kumi na tatu ya wastani ya mshahara wa mwezi mmoja. Kwa kiasi hicho cha pesa, mtu angeishi hotelini kwa miezi miwili. Dinari mbili zingekuwa sawa na pesa ngapi katika sarafu zetu?

 • Zifikirie sababu mbalimbali zilizomfanya Msamaria akitoe kiasi hicho cha pesa kwa mtu asiyemjua (35).
 • Kwa maoni yako, ni asilimia ngapi ya amri ya upendo aliyoitimiza Msamaria huyu msafiri? Itazame aya ya 27.

  8. Yesu alimaanisha nini juu ya jirani?

 • Ni majirani wapi wa karibu na wa mbali unaopaswa kuwasaidia?

  9. Ungeulizwa kuichagua nafasi katika mfano huu, ni nafasi ipi ambayo ingekufaa zaidi: ya majeruhi, jambazi wa barabara kuu, kuhani, Mlawi au mwenye hoteli? Zitoe sababu zako za kuichagua nafasi hiyo.

 • Ni kwa njia zipi Yesu anafanana na Msamaria katika mfano huu?
 • Yesu anamfananaje Myahudi majeruhi?
 • Yesu aliitayarisha njia nyingine ya kwendea mbinguni isipokuwa ile inayoelezewa katika aya ya 27. Ni njia ipi hiyo?

  10. MASWALI YA HABARI NJEMA: "Nenda ukafanye vivyo hivyo", Yesu akasema - na akaenda na akafanya hivyo mwenyewe. Hata kama watu wote wamekupita bila kuzijali huzuni zako, hawezi kufanya hivyo. Sasa anasimama karibu nawe na anataka kuvifunga vidonda vya moyo wako. Unamjibu nini? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

 • (Kwa kila mshiriki kujibu): Ni jambo gani muhimu zaidi ulilojifunza kutokana na haya Mafundisho ya Biblia?

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  8. WAKATI TENDO LISILOWEZEKANA LINATENDEKA (Mk 5:21 - 24 na 35 - 43)  TAARIFA MUHIMU: Kwa kawaida, mkuu wa sinagogi alichaguliwa kutoka miongoni mwa watu walioheshimika mjini. Watawala wa sinagogi wengine wote katika injili zote nne walikuwa wapinzani wa Yesu isipokuwa Yairo. Mtu huyu alikuwa na binti wa pekee tu (Lk 8:42).

  1. Yafikirie maisha ya kila siku ya familia hii ndogo baada ya mtoto waliyemngojea kwa muda mrefu kuzaliwa. (Wazazi walihisije walipogundua kuwa mtoto alikuwa msichana na si mvulana? Ni ndoto gani walizokuwa nazo katika maisha ya baadaye ya binti yao?)

  2. Ni nini kinachoweza kutokea kwa uhusiano baina ya wazazi na mtoto wao anapokuwa mgonjwa? Zifikirie sababu tafauti tofauti.

 • Yairo alifikiria nini kuhusu Mungu binti yake alipokuwa mgonjwa?

  3. Kwa nini Yairo aliamua kuutaka msaada kutoka kwa mtu ambaye marafiki zake wote walimchukia?

 • Yairo alihisi nini kuhusu Yesu wakati huu kutokana na alivyomhutubia (22 - 23)?

  4. Fikiria alivyohisi baba alipoipokea habari mbaya kutoka nyumbani (35).

 • Iwapo umewahi kuhisi kuwa unamsumbua Yesu, hayo yalitokea lini?

  5. Kwa nini Yesu alimwambia Yairo asiogope ingawa jambo baya sana lilikuwa limetokea kwake (36)?

 • Inawezekana kuwa Yairo aliamini nini hata baada ya bintiye kufa?

 • Yairo angekuwa amefanya nini kama hangekuwa amemwamini Yesu?

  6. Ni nini unachokiogopa sana ulimwenguni? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)
 • Ungefanya nini kama Yesu angekwambia usiogope wakati jambo baya zaidi limetendeka kwako?

 • Yesu anakuambia leo, "Usiogope, amini tu". Maneno haya yana maana gani katika hali yako ya sasa?

  7. Mkewe Yairo alimwona bintiye akifa wakati mumewe alipokuwa hayuko nyumbani. Hali yake ya kiakili ilikuwaje wakati Yesu na mumewe waliwasili nyumbani?

 • Mipango ya mazishi ilikuwa ikiendelea Yesu alipowasili katika nyumba ya Yairo (38). Yesu alitaka kuwaambia wageni nini kulingana na maneno yake yapatikanayo katika aya ya 39?

  8. Soma kwa makini jinsi Yesu alivyomfufua msichana kutoka kwa wafu (41 - 43). Ni maelezo ya kina yepi unayoyapata kuwa muhimu?

  9. Kwa nini Yesu aliyatoa maagizo makali kwa watu wasimwambie yeyote kuhusu muujiza huu ingawa lingekuwa tangazo zuri kwa mahubiri yake (43)?

  10. Tukio hili lilikuwa na athari gani kwa msichana huyu mwenyewe? Liliathiri vipi maisha yake ya baadaye?

 • Maisha ya wazazi yalibadilikaje baada ya tukio hili?
 • Unafikiri familia hii ilifikiria nini kuhusu uvumi wa kufa na kufufuka kwa Yesu waliousikia baada ya mambo hayo kutokea?

  11. HABARI NJEMA: "Usiogope, amini tu" Yesu anasema kwa kinywa chake: "Niachie haya. Ninaweza kuyashughulikia." Yesu mwenyewe alikiogopa kitu kimoja tu, yaani kutenganishwa na Baba yake wa Mbinguni. Aliogopa sana hadi akatokwa jasho la damu huko Gethisemane. Kwa njia hii alituonyesha kuwa kutenganishwa na Mungu (yaani: jahanamu) ndicho kitu cha pekee tupaswacho kukiogopa. Misiba mingine yote anaiweza na itaweza kubadilika ikawa baraka katika maisha ya wale wamwaminio.

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  9. MWANAMKE ALIYETOKWA DAMU (Mk 5:25 - 34)  TAARIFA MUHIMU: Kulingana na Sheria za Musa za kidini, mwanamke alichukuliwa kuwa mchafu wakati wake wa hedhi. Hakuna aliyeruhusiwa kumgusa au kukigusa chochote alichokuwa amekigusa. Aidha hakuruhusiwa kuingia hekaluni akiwa katika hali hiyo (Walawi 15). (KUMBUKA: Ukihisi kuwa ugonjwa kama huu hauwezi kujadiliwa katika jamii yako, unaweza kukiacha kifungu hiki na uendelee na vingine.)

  1. Labda mwanamke huyu alikuwa na miaka thelathini au arobaini na alianza kuwa mgonjwa akiwa na umri mdogo kabisa. Ugonjwa huu ulikuwa na matokeo gani katika maisha yake ya kijamii (25)? (Ulikuwa na matokeo gani kama alikuwa ameolewa/alikuwa hajaolewa?

 • Utokwaji na damu ulikuwa na matokeo gani katika hali yake ya kimwili?
 • Ugonjwa kama huo huwa na athari gani katika kujistahi kwa mtu?

  2. Mwanamke huyu alifikiria nini kuhusu Mungu baada ya kuupata ugonjwa kama huu katika miaka yake ya ujana?
 • Uhusiano wake na Mungu ulibadilikaje wakati wa ugonjwa wake wa miaka mingi?

  3. Katika aya ya 26, inasemekana kuwa mwanamke huyu alikuwa tajiri hapo awali. Zifikirie njia mbalimbali zilizompatia pesa na kwanza zilikusudiwa kwa nini.

  4. Tunaweza kufikiria kuwa matabibu (wanajinakolojia) wa nyakati hizo hawakuwa mabingwa sana. Kwa nini ilikuwa muhimu kwake kuwa tayari kuyapata matibabu kama hayo na hata kuzitumia pesa zake zote kwa "madaktari" kama hao (26)?

 • Mwanamke huyu alihisije kuhusu madaktari na waponyaji wa kila aina wakati huu wa maisha yake (26 - 28)?

  5. Je, inawezekanaje kuwa mwanamke huyu aliyekuwa amevunjwa moyo na waponyaji wengine alikuwa na hakika kuwa kuigusa tu nguo ya Yesu kungemponya (27 - 28)?

 • Una hakika kama mwanamke huyu kuwa Yesu anaweza kuzitatua shida zako mbaya zaidi? Kwa nini? Kwa nini huna uhakika?

  6. Kwa nini mwanamke huyu hakumuuliza Yesu msaada jinsi wagonjwa wengine walivyofanya (28 - 29)?

 • Kwa nini mwanamke huyu alikuchagua kugusa kama njia ya kumponya?

  7. Yesu angewezaje kujua kwa uangalifu kuwa mtu fulani ameigusa nguo yake (30 - 31)?
 • Kwa nini Yesu hakumwacha mwanamke huyu aende nyumbani bila kuzungumza naye (30 -32)?

  8. Unafikiri mwanamke huyu alihisije alipolisikia swali la Yesu katika aya ya 30?
 • Mwanamke huyu alikiona nini machoni mwa Yesu wakati Yesu aligeuka na kumwangalia usoni moja kwa moja (32)?

  9. Mwanamke huyu hakutarajia kulisema hata neno moja kwa Yesu na baadaye aliishia kumwambia hadithi nzima. Unafikiri alimwambia nini kwa kweli (33)?

 • Je, umewahi kumwambia Yesu ukweli mtupu kuhusu maisha yako kwa maneno mengi sana?

  10. Aya ya 34 unaweza kutafsiriwa kwa njia mbili: "Imani yako imekuponya." Au: "Imani yako imekuokoa." Kwa nini Yesu alitaka kuyasema maneno haya hasa kwa mwanamke huyu?
 • Kwa nini Yesu alimwita mwanamke huyu bintiye ingawa labda walikaribiana katika umri (34)?

  11. HABARI NJEMA: Yesu pia alikuwa mchafu kidini damu yake ilipomwagika alipochapwa mijeledi na aliposulubiwa. Kila mmoja aliyemgusa alikuwa mchafu. Hii ndiyo gharama aliyoilipa Yesu kwa kumwokoa huyu mwanamke - na kwa kukuokoa wewe!

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  10. "EFATHA" - FUNGUKA (Mk 7:31 - 37)  TAARIFA MUHIMU: Mtu katika kifungu hiki hakika alikuwa kiziwi tangu mwanzo wa utoto wake. Kwa sababu hiyo, alishindwa kuwasiliana na watu wengine. (Nyakati hizo bado hakukuwa na lugha ya bubu inayotumika sana.) Isaya alikuwa ametabiri miaka 700 iliyotangulia kuwa Masihi angewafanya viziwi kusikia na mabubu kusema (37, linganisha na Isa 35:5).

  1. Zifikirie aina za sauti unazozisikia mchana kutwa. Unafikiri ni nini kingekuwa shida zaidi kwako kama hukuwa na uwezo wa kusikia chochote?

  2. Fikiria maisha ya utotoni ya mtu huyu jinsi yalivyokuwa. (Ni uwezo gani uliokuwepo ambao wazazi wake waliutumia kumfunza mtoto wao ili kumkinga dhidi ya hatari, kumfanya aifanye kazi n.k.? Ni uhusiano wa aina gani aliokuwa nao na wenzi wake? Unafikiri kujistahi kwake kulikuwaje?)

  3. Yalinganishe maisha ya kiziwi huyu na maisha ya wenzi wake alipokuwa mtu mzima.
 • Labda mtu huyu pia alikuwa ameitembelea sinagogi au hekalu mara chache. Unafikiri aliyaelewa mangapi kuhusu Mungu asiyeonekana?

  4. Je watu waliomleta kwa Yesu walikuwa na nia gani? Ufikirie uwezekano mbalimbali (31 - 32).
 • Iwapo ni wewe uliyetaka kumleta kiziwi huyu kwa Yesu, ungemwelezeaje mahali mlikuwa mnampeleka na kwa nini?

  5. Kwa nini Yesu hakumponya kiziwi huyu kulingana na jinsi marafiki zake walivyomwuliza 32 -34)?
 • Kwa nini mtu huyu hakukataa na badala yake alimfuata Rabi ambaye hakumjua (33)?
 • Kwa nini Yesu alitaka kumpeleka kiziwi huyu kando, mbali kutoka kwa umati (33)?

  6. Unafikiri kiziwi huyu aliyaelewa mangapi miongoni mwa ishara nne za Yesu za lugha ya bubu katika aya ya 33 - 34? (Ni nini Yesu alitaka kukiwasilisha kwa kiziwi huyu alipoyagusa masikio yake - ulimi wake - alipotazama mbinguni - aliposhusha pumzi kwa nguvu kabla ya kumponya?)

 • Unafikiri ni kwa nini Marko aliliandika neno la kuponya la Yesu kwa Kiaramaiki cha asili katika injili yake (34)?

  7. Ni mambo gani yanayokuzuia kuyasikia yale watu wengine wanajaribu kukwambia hata kama uwezo wako wa kusikia ni mzuri sana?

 • Yesu anasimama mbele yako sasa na anakwambia: "Efatha!" - "Funguka!" Anamaanisha nini - fikiria kuhusu mawasiliano yako na watu wengine. (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

  8. Kwa kawaida inamchukua mtoto miaka mitatu kujifunza maneno muhimu zaidi ya lugha. Inawezekanaje kuwa kiziwi huyu alizipata habari hizo mara moja tu (35)?

  9. Kila muujiza wa Yesu unatufundisha jambo fulani juu ya mbinguni. Tunajifunza nini kuhusu mbinguni katika tukio hili?

  10. Kwa nini watu waliendelea kuongea kuhusu muujiza huu ingawa Yesu alikuwa amewaagiza wasiseme chochote (36)?
 • Yesu angependelea watu wawaambie wenzao nini kumhusu?
 • Unafikiriaje: kuna faida kwa kanisa la Kikristo la nyakati hizi zetu kuitangaza miujiza katika vyombo vya habari?

  11. HABARI NJEMA: Mawasiliano ya kina baina ya Yesu na Mungu yalikatishwa Yesu aliponing’inia msalabani na Mungu aliyafunga masikio yake kwa kilio chake. Mungu huwasikia tu wenye haki na wakati huo Yesu alikuwa mwenye dhambi kuliko wengine wote sio kwa sababu ya dhambi zake mwenyewe bali dhambi zetu. Kunyamaza kwa Mungu kulikuwa gharama aliyoilipa Yesu kwa kuyaanzisha tena mawasiliano kati yetu wenye dhambi na Mungu wetu mwenye haki.

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  11. MUUMINI ANAYEAMINI SHINGO UPANDE (Mk 9:14 - 29)  TAARIFA MUHIMU: Mtu aliye na pepo mbaya husemekana kuwa amepagawa. Hii ni hali tofauti na kuwa na ugonjwa wa akili au kifafa n.k. Pepo mbaya hawezi kumwingia mtu anayemwamini Yesu na aliyebatizwa kwa jina lake kwa sababu Roho Mtakatifu tayari anaishi moyoni mwake. Kulingana na Luka, kijana katika kifungu hiki alikuwa mtoto wa pekee wa wazazi wake (Lk 9:38).

  1. Yafikirie maisha ya kila siku ya baba huyu yalivyokuwa tangu mwanawe alipopagawa na upepo mwovu (17 - 18, 20 - 22). (Ufikirie uhusiano kati yake na mkewe ulivyokuwa, yeye na watoto wake wengine, yeye na majirani na yeye na Mungu. Hofu yake ilikuwa nini kuhusu maisha ya baadaye ya familia yake? Ni majaribio gani aliyokuwa ameyafanya ili kumfanya mwanawe aponywe?)

 • Yalinganishe maisha ya kijana huyu na ya wenzi wake (17 - 18, 20 - 22).

  2. Shida kubwa sana kwa baba huyu ilikuwa ipi kulingana na hali inayoelezewa katika aya ya 14 - 18?

  3. Yesu alikuwa anawazungumzia akina nani alipokizungumzia kizazi kisichoamini alichokipata kuwa kigumu sana kukivumilia (19)?

 • Kwa nini ilikuwa vigumu kwa Yesu kuvumilia kutoamini kwa watu katika hali hii (19)?
 • Je, unafikiri Yesu angekiitaje kizazi hiki chetu?

  4. Kwa nini baba alijijumuisha katika kilio cha mwanawe ili kutaka msaada: "Tuhurumie na tusaidie!" (22)?

  5. Katika aya ya 23, Yesu anaonekana akiidai imani thabiti kutoka kwa baba. Kwa nini alifanya hivyo?

 • Ungehisije iwapo mtu angedai imani kamili kutoka kwako wakati ungekuwa na mfadhaiko ?

  6. Baba alikiamini nini na alikishuku nini alipokuwa akiipaaza sauti ya ombi lake katika aya ya 24?

 • Ulikiamini nini na ulikishuku nini ulipoulilia msaada wa Yesu mara ya mwisho kuhusu shida za wapendwa wako?

  7. Je, kilio hiki cha msaada kilithibitisha kuwa tayari baba alikuwa na imani ya wokovu au la (24)? Toe sababu zako.

 • Unafikiri baba alikuwa muumini wa Yesu lini? Ujadili uwezekano mbali mbali.

  8. Kwa nini Yesu aliisaidia familia hii ingawa baba wala mwanawe hakuwa na imani thabiti (25)?
 • Ni kwa imani ya nani muujiza huu ulifanyika?
 • Ni kiasi gani cha imani kingehitajika ndipo Yesu aweze kuwasaidia wapendwa walio katika mateso?

  9. Inaelekea kuwa baba alifikiria kuwa mwanawe tayari alikuwa amekufa alipolala chini kama maiti (26). Kwa nini aliupata uzoefu huu wa mateso sana kabla ya Yesu kumsaidia. (Baba angekosa kujifunza nini kama angesaidiwa na Yesu papo hapo?)
 • Kwa nini mara kwa mara Yesu anaturuhusu tufikie hali ya kuikata tamaa kabla ya yeye kuingilia kati?

  10. "Yesu alimshika mkono na akamsimamisha" (27). Liweke jina la mtu unayesumbuliwa naye katika sentensi hii. Aya ya 27 inakwambia nini unapoisoma jinsi ilivyo?

  11. HABARI NJEMA: Hata wakati watu waovu na pepo wabaya walimtesa Yesu, bado aliuamini uwezo na upendo wa Baba yake wa Mbinguni kwa imani thabiti. Kwa sababu ya imani yake kamili, sisi pia tunaweza kuupokea msaada wake licha ya mashaka yetu.

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  12. KILIO CHA KIPOFU MWOMBAJI (Mk 10:46 - 52)  TAARIFA MUHIMU: Tunavyofahamu, Yesu alitembelea Yeriko mara moja tu. Alifanya hivyo wakati wa safari yake ya mwisho ya kwenda Yerusalemu. Yesu alikuwa wa kizazi cha Daudi moja kwa moja. Mungu alikuwa amemwaahidi mfalme huyu kuwa mwanawe angekikalia kiti cha enzi cha Israeli milele (2 Sam 7:12 - 16). Warumi waliokuwa wanaitawala nchi hiyo nyakati hizo, hawakumvumilia yeyote aliyewataja wafalme waliopita na waliokuwepo. Yesu alizungumziwa kama mwana wa Daudi mara moja tu kabla ya tukio hili na aliyefanya hivyo wakati huo alikuwa mgeni (Mt 15:22).

  1. Ni nini kingekuwa kigumu sana kwako iwapo ungekuwa unajipatia riziki ya kila siku kwa uombaji?
 • Furaha na huzuni za kila siku za kipofu huyu mwombaji zilikuwa zipi?

  2. Hata kipofu anaweza kujifunza nini anapokuwa ameketi kando ya barabara kila mwaka iwapo ana masikio mazuri?
 • Wakati wa miaka mitatu ya mahubiri ya hadharani ya Yesu, Bartimayo alisikia jinsi alivyokuwa anatembelea sehemu zingine. Kwa nini hakuyataka matibabu, kwa mfano, mji wa Yerusalemu ulikuwa na umbali wa kilomita 30 mahali Yesu alienda kila mara nyakati za sikukuu za kidini?

  3. Bartimayo alishindwa kufanya nini Yesu alipofika katika mji wake hatimaye (46)?
 • Ni mpango gani Bartimayo alikuwa nao tayari wa kuwasiliana na Yesu wakati angekuja Yeriko mwishowe?

  4. Bartimayo angewezaje kujua kuwa Yesu alikuwa mwana wa Mfalme Daudi (47)?
 • Kwa nini Bartimayo hakuwaogopa Warumi bali alimsalimia Yesu kama mwana wa mfalme atakayerithi ufalme au mfalme kwa sauti ya juu sana (47)?

  5. Kwa nini watu walijaribu kumnyamazisha Bartimayo? Yatafute majibu mengi uwezavyo (48).
 • Kwa nini yeyote hakumshika Bartimayo mkono na kumwongoza hadi kwa Yesu (48)?

  6. Ni vipi na kwa nini Bartimayo alikibadilisha kilio chake? Ilinganishe kwa makini aya ya 47 na ya 48.
 • Yesu alizionyesha hisia gani kwa cheo cha mfalme (49 - 51)?

  7. Unafikiri Bartimayo alihisi vipi watu walipomwambia kuwa Yesu alikuwa anamwita (49 - 50)?
 • Labda Bartimayo alikuwa amelitunza vizuri joho lake lililokuwa godoro na tandiko lake usiku. Kwa nini hakulitupa ghafla (50)?

  8. Kwa nini Yesu alimwuliza Bartimayo swali wazi kama hilo (51)?
 • Yesu anakuuliza swali lilo hilo sasa (51). Tafakali mjibu kwa uaminifu. (Unaweza kufanya hivyo kimoyomoyo.)

  9. Yesu aliyaponyaje macho ya huyu mtu (52)?
 • Aya ya 52 inaweza kutafsiriwa kwa njia mbili:"Imani yako imekuponya" au "Imani yako imekuokoa." Kwa nini Yesu alitaka kuyasema maneno haya kwa Bartimayo katika hali hii?

  10. Bartimayo alimfuata Yesu barabarani labda hadi Yerusalemu (52b). Siku iliyofuatia, kila mtu alikuwa akimwamkua Yesu kama "mwana wa Daudi" alipokuwa anaingia mjini (Mk 11:9 - 10). Wajibu wa Bartimayo ulikuwa upi katika yote haya?
 • Baada ya wiki tu, Bartimayo alimshuhudia mfadhili wake akisulubiwa msalabani. Unafikiri alifahamu nini kuhusu kilichomfanya Yesu afe?

  ***

  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  13. UPENDO HAUTAWEZA KUSHINDWA (Mk 14:1 - 9)  TAARIFA MUHIMU: Kiongozi aelezee kwa kifupi mistari ifwatayo inatufunza nini kuhusu Maria wa Bethania. Lk 10:38 - 42, Yn 11 na Yn 12:1 - 11. (Maria huyu asichanganywe na mamake Yesu au mwanamke anayezungumziwa katika (Lk 7:36 - 50). Wazazi wa Martha, Maria na Lazaro dhahiri walikuwa wamekufa. Waliwaachia mabinti zao pesa za kutumia labda wakati wangeolewa au za kuwasaidia wakati za uzeeni. Juma la mwisho ya maisha ya Yesu ulimwenguni ilikuwa inaanza tu.
  1. Ni zawadi gani ungependa kumpa rafiki yako iwapo ungejua kuwa angekufa?
 • Yesu anayataja maziko yake hapa (1 - 2, 8)? Unafikiri Maria, tofauti na wanafunzi, alitambua kuwa angekufa karibuni? Toe sababu zako.

  2. Ili kuyanunua marashi ya nardo, ungekilipa kiasi cha pesa ambacho kingelingana na wastani ya mshahara ambao mfanyakazi angeupokea kwa mwaka mzima (3). Hii ndiyo sababu tone moja moja tu la mafuta haya lilitumika. Chupa hii ingeuzwa kiasi gani cha pesa ukilinganisha na sarafu zetu leo?

 • Kwa kawaida inachukua muda gani kuziweka pesa zinazoweza kulingana na mshahara wa mwaka mmoja?
 • Maria alipoyanunua marashi haya ghali, alikuwa akifikiria nini kuhusu mahari yake au malipo yake ya uzeeni?

  3. Kwa nini Maria aliyamwaga mafuta yote katika kichwa cha Yesu badala ya matone machache tu (3 - 4)?
 • Maneno "Masiya" na "Kristo" yana maana ya "aliyepakwa mafuta". Wafalme wa Wayahudi kawaida walikuwa wanapakwa mafuta mwanzoni mwa kazi zao. Kwa nini Yesu hakupakwa mafuta hadi muda mfupi tu kabla ya maziko yake?

  4. Maria alikuwa ameitumia akiba yake yote kwa chupa ya marashi. Ni sehemu gani ya kumkosoa iliyomuudhi zaidi (4 - 5)?
 • Mshahara wa mwaka mmoja ungetumiwaje kuwafaidi maskini wa mji (5)? Ufikirie uwezekano tofauti tofauti.

  5. Yesu alimtetea Maria kwa njia mbalimbali zipi (6 - 9)?
 • Unafikiri Yesu angekwambia alivyomwambia Maria: "Yeye amefanya alivyoweza" (8)?
 • Ungemfanyia Yesu nini kutoka sasa na kuendelea?

  6. Tendo la Maria na tendo la Yesu yanafananaje (kifo chake msalabani, k.m. “injili" katika aya ya 9)?
 • Unafikiri ni "hasara" gani iliyo kubwa: kwamba Maria aliyamwaga marashi yake ghali kwa ajili ya Yesu au kwamba Yesu aliimwaga damu yake kwa ajili ya Maria?

  7. Ni jambo gani lililo la kipekee sana litakalokumbukwa milele katika tabia za Maria (9)?
 • Ni kumbukumbu gani ungependa kuiacha utakapokufa?

  8. Unafikiri Maria alihisi vipi baadaye kuhusu pesa "alizozipoteza" kwa ajili ya Yesu siku hiyo?
 • Maria alijifunzaje kumpenda Yesu sana?
 • Tunawezaje kujifunza kumpenda Yesu jinsi Maria alivyompenda?

  9. HABARI NJEMA: Maria alikuwa amejifunza kumpenda Yesu kwa kumsikiliza. Hiyo ndiyo sababu pia aliweza kumhudumia wakati uliofaa. Kwanza, Maria alikuwa ameamini kusamehewa kwa dhambi zake na imani hii yake ndiyo iliyomfanya akitoe kila alichokuwa nacho kwa Bwana. Ilikuwa ni kwa sababu yake Yesu alitembea akiwa na harufu ya marashi ya nardo kila mahali nyakati za siku zake za mwisho ulimwenguni.

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  14. KICHEKO KIITWACHO HUKUMU YA YESU (Mk 15:1 - 15)  TAARIFA MUHIMU: Kuna maswali mengi sana katika somo hili ambayo huwezi kuyauliza yote katika kipindi cha saa moja. Wachague wahusika wawili au watatu kutoka kikundi kwa majadiliano yenu. Au badala yake kigawe kikundi chako cha Mafundisho ya Biblia katika vikundi vya washirika 2 au 3. Kila kikundi kijadiliane kuhusu wahusika wawili au watatu na kisha kishiriki matokeo yake na vingine.

  1. PONTIO PILATO
  Kama gavana wa Yuda mwaka wa 26 - 36 BK, aliwawakilisha wanajeshi watawala wa Himaya ya Warumi na aliwajibika kwa Mfame Tiberia mwenyewe. Pilato hakutaka mfalme ausikie uvumi wowote kuhusu maasi ya Wayahudi. Ilikuwa haki yake kuitangaza adhabu ya kifo au kuinyima.

  Aya ya 1 - 15

 • Ni mawazo yapi unayoyapata kuhusu tabia za Pilato na maadili yake?
 • Unafikiria nini kuhusu jaji anayeyauliza mawsali kama yale yanayoulizwa katika aya ya 12 na ya 14 wakati wa hukumu?
 • Kwa nini Pilato hakuutumia uwezo wake na badala yake aliwaruhusu wengine wamtolee uamuzi?
 • Unafikiri Pilato alifikiria nini kuhusu Yesu? (Kwa nini alimwita Yesu "Mfalme wa Wayahudi" mara mbili? (linganisha aya ya 9 na ya 12.)
 • Walinganishe hawa watu wawili: Gavana wa Kirumi na Mfalme wa Wayahudi. Kuna tofauti za kuvutia zipi kati yao katika hali hii?
 • Ni nani aliyeisuluhisha kesi hii rasmi mwishoni?
 • Unafikiri Pilato alihisije alipomtoa Yesu achapwe mijeledi na asulubiwe (15)?
 • Unafikiri Pilato alijaribuje kuituliza dhamiri yake maishani mwake?
 • Kama ungekuwa katika hali ya Pilato asubuhi ile ungeiamuaje kesi hii?

  2. BARABA
  Mwuaji na kiongozi wa uasi kisiasa, jina lake linamaanisha mwana wa baba.  Aya ya 6 - 15
 • Yafikirie maisha ya utoto, ya ujana na ya utu uzima ya mtu huyu. Ni nini labda kilichomfanya Baraba kuwa mwanamapinduzi na mwuaji?

 • Iwapo hali zako zingekuwa tofauti, unafikiri mwenyewe ungekuwa mwuaji? Kwa nini? Kwa nini hungekuwa?

 • Unafikiri ni mawazo gani yalizokuwa zinaendelea akilini mwa Baraba wakati siku ya kuuawa kwake ilipokuwa inakaribia? (Unafikiri alijuta kwa lolote?)

 • Unafikiri Baraba alienda kumwona mtu aliyesulubiwa msalabani badala yake?
 • Ni kwa njia gani sote tunafananishwa na Baraba katika mahusiano yetu na Yesu?

  3. MAKUHANI WAKUU
  Kwa kawaida kulikuwa na kuhani mkuu mmoja kila wakati lakini katika hali hii, kulikuwa na wawili: Kayafa, kuhani mkuu halisi katika mwaka wa 18 - 36 BK na baba mkwe, Anasi aliyeyashikilia mamlaka awali. Anasi bado aliutumia ushawishi wake kupitia kwa mkwe wake.

  Aya ya 1 - 15
 • Unafikiri ni nini kuhani mkuu alikichukulia kuwa wito mkuu maishani?
 • Kwa nini Kayafa na Anasi walimwonea Yesu wivu?
 • Kwa nini makuhani wakuu hawakuitambua nia yao?
 • Ni uvunjaji sheria upi uliokuwa mbaya zaidi: hukumu ya kifo isiyo haki iliyotekelezwa na makuhani wakuu au mauaji aliyokuwa ameyatekeleza Baraba wakati wa uasi?

 • Ni nini kinachoweza kumfanya mtu wa dini sana kuwa chombo cha ibilisi?
 • Unafikiri unawafanana makuhani wakuu kwa njia yoyote? Iwapo unawafanana, ni kwa njia gani?

  4. UMATI
 • Walipiga kelele, "Hosana" kwa Yesu Jumapili iliyokuwa imetangulia. Sasa wanapaaza sauti: "Msulubishe!" Lazima kulikuwa na wengine miongoni mwa umati huu waliokuwa wamesaidiwa na Yesu.

  Aya ya 8 - 15

 • Kwa nini umati ulimtaka muuaji hatari aachiliwe huru?
 • Watu waliwezaje kukubali kumshambulia mfadhili wao? (Kwa nini kulikosekana hata sauti ya mtu moja iliyomtetea Yesu dhidi ya hila za haki katika hali hii?)
 • Je, ungefanya nini kama ungekuwa miongoni mwa umati asubuhi hiyo?
 • Unafikiri tendo kama hili lingetokea katika nchi yako wakati huu? Toe sababu zako?
 • Aya hii kinatufundisha nini kuhusu uzuri na ubaya wa demokrasia?

  5. YESU
  Anaisema sentensi moja tu wakati wa hukumu nzima (2). Kwa upande mwingine, ananyamaza.

  Aya ya 1 - 15

 • Kufikia wakati huu, Yesu alikuwa amelikataa jina lolote isipokuwa "Mwana wa Mtu". Kwa nini sasa anakubali hadharani kuwa yeye ni mfalme wa Wayahudi (2)?
 • Kwa nini Yesu hajitetei mwenyewe?
 • Mlinganishe Yesu na watu wengine katika kifungu hiki. Je, anatofautianaje nao? (Ni nini kinachomfanya Yesu astaajabiwe hasa unapoizingatia hali yake?)
 • Unafikiri Yesu alihisi nini dhidi ya wale watu wote waliomzunguka na waliokuwa na hamu ya kuimwaga damu?
 • Ni nani aliyeamua kesi ya Yesu wakati wa hukumu yake: Pilato, Mungu au shetani?

  ***

  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  15. YESU ANAKUTANA NA WAHALIFU WAWILI (Lk 23:32 - 43)  TAARIFA MUHIMU: Katika Himaya ya Kirumi kusulubiwa kulitumika tu kwa uhalifu mbaya zaidi. Basi tunaweza kuchukulia kuwa watu hawa wawili walikuwa wahalifu wajuzi ambao labda walikuwa wamewaua watu kwa sababu ya pesa. (Masiha au Kristo) kilikuwa cheo cha mfalme aliyengojewa na Wayahudi tangu nyakati za Agano la Kale.

  1. Mtu anayewapiga wengine kwa ngumi au kwa ulimi wake anaweza kuwa na furaha?
 • Kwa nini vijana wengi wa nyakati hizi zetu hukimbilia vurugu na hufurahia kuwafanyia ghasia wengine?

  2. Zifikirie sababu mbalimbali zilizowafanya hawa watu wawili wakimbilie vurugu katika ujana wao.
 • Labda ni nani angeweza kuwakomesha hawa wawili kabla ya wao kuwa wabaya kupindukia?
 • Daima unaweza kuzibadilisha tabia zako unapofahamu kuwa zinakudhuru wewe na wengine?
  3. Wahalifu hawa wawili wangezichunguza tabia za Yesu kutokana na kukaribiana naye kuliko mtu mwingine yeyote. Ni maneno na matendo yapi yaliyoweza kuwashangaza zaidi (34 - 38)?
 • Kwa nini Yesu alitaka kuwatetea wale waliomtesa mbele ya Baba yake wa mbinguni (34)?
 • Unaweza kumwombea adui mbaya kuliko wote: "Mungu, msamehe. Hakujua ni vipi alivyonitendea vibaya" (34).

  4. Tafuta kutoka aya kwa nini umati, watawala, wanajeshi wa Kirumi na mmoja wa wahalifu walimpigia Yesu ukelele (34b - 39).
 • Hawa watu walimdhihaki Yesu kwa sababu gani (35 - 39)?
 • Kwa nini mmoja wa marafiki zake Yesu hakumtetea?
 • Je, ungesema na ungefanya nini kama ungekuwa unasimama chini ya msalaba?

  5. Ni nini kilichomfanya mmoja wa wahalifu kulifikia hitimisho kuwa Yesu alikuwa mfalme na alikuwa na ufalme wake mwenyewe (37 - 38, 42)?

 • Mlinganishe Yesu msalabani na wafalme wengine wa ulimwengu huu. Kuna tofauti zipi za kuvutia zaidi kati yao?

 • Ni nini kilichomfanya mmoja wa wahalifu ahitimishe kuwa Yesu hakuwa tu mfalme bali alikuwa Mungu pia (40 - 41)?

  6. Wahalifu wengi hawakubali kabisa kuwa walikuwa wameyatenda maovu yoyote. Ni nini kilichomfanya mmoja wa wahalifu akubali kuwa hukumu ya kifo ilikuwa adhabu halali kwa uhalifu wake (41)?

 • Kwa nini mhalifu yule mwingine hakuikubali hatia yake hata katika hali hii?
 • Ni nani kati ya hawa wahalifu wawili unayemwelewa vyema: yule aliyeikubali hatia yake au yule aliyeikana?

  7. Aya ya 42 ina ombi fupi sana: "Unikumbuke!" Kwa nini ni muhimu kwetu binadamu kuwa mtu fulani tunayempenda anatukumbuka tunapokuwa matesoni?
 • Kwa nini mhalifu huyu hakuuliza moja kwa moja aruhusiwe kuuingia ufalme wa Yesu?

  8. Mhalifu huyu alikuwa amefikiria nini alipolisikia jibu laYesu (43)?
 • Kwa nini Yesu alimruhusu mwuaji katili kuingia Paradiso (mbinguni)?
 • Ni wakati upi, kulingana na maoni yako, ambapo mhalifu huyu alianza kumwamini Yesu? Taja aya.

  9. Zifikirie saa za mwisho za mhalifu aliyekuwa muumini wa Yesu. Alikuwa mwenye furaha au alikuwa mwenye huzuni saa hizo?

 • Labda mamake, mkewe au mtoto wa aliyekuwa mhalifu alikuwa anasimama chini ya msalaba. Ni kumbukumbu ipi aliyoiacha kwa familia yake?
 • Ni ushuhuda upi aliouacha mhalifu huyu kwa vizazi vijavyo vitakavyozisoma habari zake katika Biblia?

  10. HABARI NJEMA: Milango ya Paradiso ilifunguliwa mbele ya mhalifu lakini badala yake ilimpasa Yesu mwenyewe kuiingia kupitia milango ya jahanamu. Unataka kuliomba ombi sawa na la mhalifu huyu? "Yesu, unikumbuke!" Kama unaweza, atakupa jibu sawa: "Siku moja utakuwa nami Paradiso." (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)
 • (Kwa kila mwana kikundi kujibu): Ni jambo gani muhimu zaidi ulilojifunza katika haya Mafundisho ya Biblia?
  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  16. KUFUFUKA KUSIKOAMINIKA (Mk 16:1 - 8)


  TAARIFA MUHIMU: Kulingana na desturi za kale, Marko alikuwa mkalimani wa Petero; na injili yake ilihusu maisha ya Yesu jinsi yalivyoonekana machoni pa Petero. Mojawapo ya dhamira katika injili hii ni ukosefu wa imani ya mwanafunzi huyu. Ingawa Yesu alikuwa amekitabiri kifo na ufufuo wake mara tatu tayari, wanafunzi wake walikuwa wazito sana kumwamini. Kumbuka kuwa mwili wa Yesu ulikuwa umepakwa mafuta tayari siku ile aliyokufa.

  1. Kwa nini wanawake kutoka Galilaya walisisitiza kulitembelea kaburi licha ya jiwe na askari ambao (kulingana na Mathayo) walikuwa wakilichunga kaburi (1 - 3)?

  2. Tayari wanawake walikuwa wameshuhudia mwili wa Yesu ulioshughulikiwa vibaya ukipakwa mafuta siku mbili zilizotangulia. Kwa nini unafikiri walitaka kuupaka mafuta tena?
 • Unafikiri ungependa kuuona na kuugusa mwili wa mpendwa wako katika hali hiyo?
 • Ni Yohana tu aliyeshuhudia kifo cha Yesu; wengine walikuwa wametoweka kutoka mahali hapo. Kwa nini hawakuja sasa kulitembelea kaburi la Bwana wao? (Unafikiri kuna tofauti kati ya wanawake na wanaume kuhusu tukio hili? Kama ipo, tofauti ni ipi?)

  3. Iwapo wanawake waliamini katika ufufuo kulingana na utabiri wa Yesu, unafikiri wangetendaje Jumapili hiyo asubuhi (1 - 4)?

  4. Wanawake walifikiria nini walipoyasikia maneno ya malaika (6 - 7)?
 • Ni nini kilichowaogofya sana wanawake (8)?

  5. Kwa nini Yesu aliwachagua wanawake kuwa mashahidi wa ufufuo wake licha ya kuwa hawakukubaliwa kuwa mashahidi katika mahakama wakati huo (7, 10)?

  6. Ni vipi na ni lini imani ya ufufuo wa Yesu ilianza mioyoni mwa wanawake hawa?

  7. Petero alimkana Bwana wake siku mbili zilizokuwa zimetangulia. Ilimaanisha nini kwake Yesu alipomtumia salamu maalumu (7)?

  8. Kuna chochote maishani mwako kinachoonekana kutowezekana kwako kama maiti kufufuka tena? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

 • Ungejibu nini kama Yesu angekukemea kwa kuikosa imani jinsi alivyowakemea wanafunzi wake katika aya ya 14?

  9. Kuna tofauti gani baina ya ufufuo wa mwili (unaofundishwa tu katika imani ya Kikristo) na kuishi milele kwa roho (ambako ni imani ya kawaida katika dini nyingi)?

  10. Kama ufufuo wa mwili haungekuwepo, Ukristo ungewapa nini wanadamu?
 • Chukulia kwamba mtu fulani aliyaamini mafundisho yote ya Kikristo isipokuwa ufufuo wa mwili. Kwa nini hatungemwita Mkristo?

  11. HABARI NJEMA: Hatimaye wanafunzi walipothibitisha kuwa kweli Yesu alikuwa amefufuka kimwili kutoka kwa wafu, waliwaendea mashahidi wake thabiti. Wengi wao walikufa kama wafiadini wakikataa kuiacha imani yao kwa vyovyote vile. Walijua kuwa Yesu angekuwa nao milele katika ulimwengu huu na ule ujao.

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  17. YESU ANAKUTANA NA MWANAFUNZI MWENYE MASHAKA (Yn 20:19 - 29)  TAARIFA MUHIMU: Thomaso alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na wawili wa Yesu. Labda alikuwa na ndugu pacha kwa sababu jina lake linamaanisha "pacha".

  1. Mwanadamu anaweza kuwa na maisha mema katika ulimwengu huu bila kuamini kuwa mwili wake utafufuka kutoka kaburini siku ya mwisho?
 • Ni tabia nzuri zipi zipatikanazo katika nafsi ya mtu kama Thomaso? Tabia mbaya ni zipi?
 • Unafikiri ni kwa nini Yesu alimchagua mtu kama huyu kuwa mmoja wa wanafunzi wake?

  2. Wanafunzi walifikiria nini kuhusu Yesu asubuhi na mchana wa Jumapili ya Pasaka?
 • Kwa nini wanafunzi hawakuamini katika ufufuo wa Yesu?

 • Yafikirie maelezo mbalimbali kuhusu pahali ambapo Thomaso angekuwa ameenda Jumapili jioni alipokuwa hayupo pamoja na wanafunzi wengine kumi (24).

 • Kwa nini Yesu aliyefufuka aliwaamkua wanafunzi wake kwa kusema, "Amani iwe nanyi" (21, 26)

  3. Ufufuo ulikuwa umetabiriwa na manabii wa Agano la Kale na Yesu mwenyewe. Sasa marafiki wa dhati wa Thomaso walimhakikishia kuwa walikuwa wamemwona Yesu kwa macho yao yenyewe. Kwa nini Thomaso hakuamini katika ufufuo wa Yesu hata baada ya kuusikia ushuhuda huu wote (25a)?

 • Kama ungekuwa katika hali ya Thomaso, unafikiri ungeuamini ufufuo? Toa sababu zako.

  4. Unafikiri Thomaso alijihisi vipi juma lililofuata miongoni mwa marafiki zake walioshangilia?

 • Ni nini kilichomfanya Thomaso kukaa na marafiki zake badala ya kujiendea zake juma hilo hiyo?

 • Je, ni nini kingetokea kwa Thomaso iwapo angekiacha kikundi cha wanafunzi wakati huu?

 • Ni nini kitakachotokea kwetu iwapo tutauacha ushirika wa Kikristo tunapokuwa na mashaka kuhusu mafundisho ya dini ya kimsingi ya Kikristo?

  6. Kwa nini Thomaso alitaka kumgusa Yesu kabla ya kuamini katika ufufuo wake (25b)?
  7.
 • Unafikiri Thomaso alihisi vipi alipoyasikia maneno yake mwenyewe kutoka kinywani mwa Yesu (25 - 27)?

  6. Ni maelezo yapi ya kinaganaga yanayotuonyesha kuwa Yesu alikuwa si ziwi wala pepo (27)?
 • Unafikiri kwa kweli Thomaso aliviweka vidole vyake katika makovu ya mikononi na ubavuni mwa Yesu?

  7. Thomaso alikuwa mtu wa kwanza katika Agano Jipya kumwita Yesu Mungu sio tu Mwana wa Mungu (28). Kwa nini Wakristo wote ulimwenguni wanaamini kuwa Yesu ni Mungu?

  8. Yesu anamtaja nani katika aya ya 29?
 • Kwa nini ni muhimu kuuamini msaada wa Mungu kabla ya kuupokea?
  9. Kulingana na kifungu hiki, Yesu anamtendeaje mtu anayependa kumwamini lakini hawezi?
 • Ungemjibu nini mtu aliyesema kwako: "Ninamwamini Yesu lakini siamini katika ufufuo wake wa mwili"?
 • Kwa nini imani yote ya Kikristo inaporomoka iwapo mwili wa Yesu haukufufuka kutoka kaburini?

  10. MASWALI YA HABARI NJEMA: Thomaso alisema kwa Yesu: "Bwana wangu na Mungu wangu!" Unaweza kulifanya ungamo sawa kwa Yesu leo? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)
 • (Kwa kila mwana kikundi kujibu): Ni jambo gani muhimu zaidi ulilojifunza kutokana na haya Mafundisho ya Biblia?

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com