MBH JUU ya JONAH

1. BWANA ALITUMA MMISIONARI - 2 Wafalme 14:24-27 na Yona 1:1-3
2. MUNGU ALITUMA KIMBUNGA
3. MUNGU LITUMA UAMSHO
4. MUNGU ALITUMA MTANGONA AND BUU
5. ISHARA ZA YONA: MUNGU ALIMTUMA MWANAE

Print all lessons

? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com


1. BWANA ALITUMA MMISIONARI - 2 Wafalme 14:24-27 na Yona 1:1-3MANENO YA AWALI YA KITABU KIZIMA CHA YONA. (ichapishwe kwa kila mtu na kisomwe mwanzoni mwa masomo ya Biblia.)

 • Maisha ya Yona yalipishana kwa sehemu nay ale ya mfalme Jeroboam II wa Israel (793-753 KK). Ufalme wa Daudi na Suleimani ulikuwa umegawanyika mara mbili katika mwaka wa 930 KK: Yuda kusini na Israeli kaskazini. Yona aliishia Israeli. Alizaliwa katika kijiji cha Gath Hepher karibu na Nazareti. Hekalu lilikuwa katika Yuda lakini Waisarael hawakwenda huko na walianguka kabisa katika kuabudu miungu katika mwaka ule.
 • Ufalme wa Assyria ulikuepo Zaidi ya miaka elfu moja. Ulikuwa na miongo miwili, baadaye ili ilipishana na maisha ya Yona (900-612 BC). Kwa vile miaka mia moja kabla ya Yona, wafalme wa Assyria walizidisha vita, ambao walifahamika kwa ukali wao. Nchi zilizoshindwa ziliwalipa Waachemi na walilazimika kuwa katika utumwa wa waachemi. Israeli bado iliishi kama kma Nchi, lakini walilipa hela nyingi kwa ulinzi wa Waachemi.
 • Mji wa Nineveh ulikuwa mji mkuu wa Waachemi. Wana elimukale wamegundua ma kumi elfu ya maandishi katika mawe kutoka mabaki ya nyumba. Maelezo ya vita vya waachemi yana unyama ndani yake: miili iliyo katwa katwa, watu uchi walitupwa katika machongo ya miti na wakaachwa wameninginia kule, milima ya fufu la vichwa katika vizingiti vya milangu...

  2.Wafelme 14:24-27
  Tafuta Gath Hepher na mpaka kati ya Hamath na bahari ya chumvi kutoka ramani. Yeroboam katika mstari was 24 unataja Yeroboam I. Dhambi ya Yeroboam inataja sanamu mbili za ndama ambazo Yeroboam alisimamisha katika Bethel na Dan.
 • Je unawezaje kukadiria miaka arobaini ya Jeroboam II kama mfalme wa Israel?
 • Tukifikiria juu ya utawala wa Jeroboam , je hali ya Waisrael ambao waliomwamini na wala Yahweh na wala sio miungu mingine ilikuaje?
 • Je unafikiri watu wa Israeli walimthanije Yona kama nabii?
 • (KWA JAPANI TU: Je watu wa Japani wangalifikiaje juu ya Nabii ambaye alitabiliri kuwa kiziwa cha kingechukulia tena kuwa chini ya mikono ya Wajapani
 • na ilitendeka hivyo baadaye?)
  Yona 1:1-3
  Ninawi
 • Je chukumu la Yona lilitofautianaje nan a chukumu la awali kama nabii?
 • Kwa nini Bwana akumuamuru nabii wake kuhubiri dhidi ya kuabudu sanamu katika nchi yake lakini akataka kumtuma katika mbali kule Ninawi?
 • Je nini ilikuwa shabaha ya Mungu kumtuma mmisionary katika mji katiri katika dunia nzima ?
 • Je unafikiri nini juu ya ujumbe mabao Yona aliagizwa kutangaza katika Ninawi (2)?
 • Kwa Bwana hakuwashitusha wakaaji wa Ninawi kwa njia zingine kwa mfano kutma jeshi ya maadui katika milango yao? Kwa nini mmisionari?
 • Yona alijaribu kutafakari makaribisho atakayoyapata Ninawi. Ni nini kingefanyika kwa mmisionari mgeni katika mji ule katiri?
 • Je unafikiri Mungu aliataka kutimiza katika sfari hii ya umissionari a) katika nchi ya Mmisionari na b) katika Maisha ya Mmisionari?
  Vita
  Tafuta Ninawi, Japho na Tarshish kutoka ramani. Ninawi alikuwa karibu na mji wa Mosul ya Iraq ya leo. Tarshsish ulikuwa katika Hispani ya sasa
 • mwisho wa dunia katika kipindi kile. Japho ni Jaffa ya sasa.
  -Jaribu uwezavyo kupata sababu mbalimbali kwa nini Yona alitaka kutoroka kutoka kwa kazi aliyopewa na Mungu.
 • Hesabu kutoka ramani kuna kilometa ngapi kati ya Gath Hefer (Nazareth) na Ninawi kwa upande mmoja na katika ya Gath Hefer na Tarshish kwa upande mwingine. Ni sehemu gani ya sehemu hizi iko mbali sana.?
 • Je unafikiri nini: Je Yona alifikiri kweli kwamba angeweza kutoroka kutoka uso wa Bwana? Toa sababu zako.
 • Je Biblia inamaanisha nini inaposema (katika Kiebrania halisi) kwamba Yona alitaka "apate kujiepusha na uso wa BWANA" (3)?
 • Kadiria ni hela kiasi gani (ukilinganisha na mshahara wa mtu wa mwezi mmoja) Yona alihitaji kulipa nauri kwenda Tarshishi?
 • Je unafikiri Yona aliwambia familia yake nini alipokuwa naondoka kwenda Tarshish?
 • Je Yona alifikiri lini atarudi nyumbani?
  Matumizi
 • Je Mungu alikuita katika kazi gani na aliifanyeje?
 • Ni nani wakaaji wa Ninawi" ambao unahitaji kuwahubiria neno la Bwana?
 • Kama umewahi kutoroka kutoka mbele za Mungu tafadhali tuambie ilikuaje na ni kwa nini ilitendeka?
 • Tunawezaje kujizuia kutofanya kosa lile lile ambalo Yona alifanya?
  INJILI: Yesu tofauti na Yona alitoka mbinguni kwa hiari yake mwenyewe akawa Mmisionari kwa ulimwengu wote, alijua vizuri jinsi itakavyoenda. Baada ya kufufuka kwake alituma ujumbe huu kwa ulimwengu wote, pia miji yetu na bila mwaliko kutoka upande wetu. Hii inaonyesha jinsi gani Yesus anapenda kila mji duniani.

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  2. MUNGU ALITUMA KIMBUNGA  Yona 1:4-16
  YALIYOMO: Wakati ule kipindi cha kusafiri kwa Mashua kiisha mwezi wa Tisa katika Bahari ya mediterania; baada ya hapo dhoruba zilifanya kusafiri kuwa hatari. Katika Matendo ya Mitume tunasoma kuwa watu Zaidi ya 300 waliweza kusafiri katika Mashua kubwa (Matendo ya Mitume 27:37). Mashua kama hizo zilikuwa na ngurumo (13). "Bwana" ("Yahweh") ndo jina kamili la Mungu wa Waisrael (9, 14, 16).
  Mashambulizi ya Dhoruba
 • Unafikiri nini juu ya Bwana anapotumia majanga kama kama vile, (dhoruba,mtetemoko wa aridhi au Tsunami) kwa kuwaadhibu watu wau kumzuia mabii anayetoroka (4)?
 • Je unafikiri nini juu ya Mungu ambaye hawezi kuamuru maumbile ?
 • Je unapata dhana gani juu ya mabaria katika somo hili?
 • Tafuta kutoka somo mambo ambayo mabaharia walifanya ili kuweza kujiokoa. Ili waweze kuendelea ?
 • Je Yona aliogopa katika dhoruba au hakuwa? Je kwa nini unafikiri hivyo-toa sababau zako?
 • Ni nini kilimfanya Yona kulala usingizi sana kiasi kwamba hakuweza kuamka kipindi cha dhoruba?
 • Kutoka Injili tunajifunza kwamba Yesu pia alilala katiba katika dhoruba. Je kuna tofauti gani kati ya usingizia wake na ule wa Yona?
 • Je unafikiri Yona alifikiri nini wakati mabaharia waliamua kutatua tatizo kwa kura (7a)?
 • Kuna tofauti gani iliyoko kati ya ungamo la Yona na lile la Misha yake (9)?
 • Kwa nini Yona aliwaambia ukweli hali yake kwa mabaharia na wala hakuweza kudanganya (10)?
 • Je hatua ya mabahari juu ya ukiri wa Yona unaonyesha nini(8,10-11)?
 • Kwa nini Yona aliwaambia mabaharia wamtupe katika bahari badala yay eye mwenyewe kuruka (12)?
 • Je unafikiri Yona alikuwa na wazo gani aliposema maneno yaliyoa andikwa katika mstari wa 12?
 • Je Mabaharia hawakuwa tayari kutupa Yona mabarini japo walijua kuwa dhuruba ilikuwa kosa lake (13-14)?
 • Je unafikiri nini juu mstari wa 15?
 • Je Imani ya mabaria ilibadirika kwa wakati ule au ilibadirika kabisa (14, 16)? Toa sababu zako.
 • Je mabaria pengine walitoa ahadi gani kwa Munguwa Yona? Fikiri sababu mbali mbali (16)?

  Hitimisho
 • Je somo hili linasema nini juu ya Mkristo ambaye anajaribu kumtoroka Mungu kwa njia moja au nyingine?
 • Je Mungu anatumia mbinu gani/ jia leo hii kuwanaza watu kam Yona?
 • Angalia somo mara nyingine na jibu: Bwana anatumiaje hata mateso ya watoto wake kwa kusudi za ufalme wake?
 • Ni nini katika surah ii kinaguza moyo wako sana?
  INJILI: Katika mistari hii Yona ni mfano wa Yesu. Mwokozi wetu alikuwa tayari kutupwa katika ziwa ambalo lilikuwa na moto unayochomwa ili tungalihitaji kutupwa pale. Hivi ndivyo hazira ya Mungu juu ya dhambi zetu ili punguazwa.

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  4. MUNGU LITUMA UAMSHO  Yona 3
  HABARI YA AWALI: Mji wa Ninawi unatajwa mara tu baada ya gharika - na tayari ulikuwa unaitwa mji mkuu (Mwanzo.10:12). Utafiki wa miamba unaonyesha kwamba kulikuwa na wakaaji katika mji wa Ninawi mapema 4500 KK. Yona na watu wa mji ule walielewana kwa sababu Kiebrania na Accad ni lugha ambazo zinakaribiana.
  Majina na Wafalem watawala wa Assyrian yanafahamika, shukrania kwa vigai wa mawe. Lakini hatujui mwaka mabao Yona alienda Ninawi, hatuwezi kuwa na uhakika wa jina la mfame pia. Katikati ya karne ya 8 KK kulikuwa na wafalme wengine waliofuatana.
  Kuitwa kuwa mmisionari - mara nyingine tena!
 • Jaribu kufikiri hali ya kimwili ya Yona baada ya samaki kumtabika katika ukingo wa mshariki mwa bahari ya Mediterranean (2:11)?
 • Je Mungu ambaye Yona aliwmwamini alikuaje katika hali yake ya maisha ? Linganisha dhana hii ya Mungu ambayo alikuwa nayo kabla ya safari yake. (1:9; 2:10b na 4:2)?
 • Je Yona alipata wapi ujasiri wa Imani alikuwa nayo sasa kwa Mungu?
 • Je unafikiri ilikuwa rahisi kwa Yona kuwa mmsionari baada ya matukio kuliko awali?
 • Tazama ramani. Je ni kiasi gani cha kilometa ambacho alitembea? Je unafikiri inamchukua mda gani?
  Yona kuhubiri Sheria
 • Je unarikiri wana Inchi wenzako watafanya nini kama mtu Fulani ataanza kuhubiri katika barabara za mji mkuu: "Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa "?
 • Je utafanyeje ukisikia hubiri la namna hii katika Kanisa lako?
 • Je Yona aliwezaje kupata ujarisiri wa kuhubiri namna hii kwa Waasiria wakatiri?
 • Kwa nini Yona hakuweza kuelezea katika mahubiri yake jinsi alivyookolewa kutoka tumbo la nyangumi?
 • Kwa nini Mungu alitaka kuwaonya watu wa Ninawi (kinyume na, tuseme, Sodoma) kwamba janga halitahebukika?
 • Fikiria ni kwa nini wakaaji wa Ninawi hawakuweza kunyamazisha nabii mgeni?
 • Ni nini kinachikushangaza juu ya hatua ya mfalme kwa ujumbe wa Yona(6-9)?
 • Ni nini kilichomfanya mfalme atamani kuwa Mungu wa Yona nagekuwa na huruma kwa mji huu?

  Hatua za awali za uamsho
 • Ni nini kilichofanya ujumbe wa Yona kuwa na nguvu sana?
 • NI nini kingalifanyika kama Yona alitembea akipiga kelele: "Mungu anapenda watu wote wa dunia, ninyi mkiwa miongoni mwao"?
 • Kwa nini nia lazima sharia kuhubiriawa kabla ya uamsho kufika?
 • Tunaweza kupata wapi ujasiri kuhubiri kwa wenzetu sharia kali kama Yona alivyo hubiria Waninawi?
 • Yesu mwenyewe alisema kuwa yeye ni "mkuu kuliko Yona" (Mathayo12:41). Alimaanisha nini? (Tunarudi katika hili wakati mwingine.)
  Ishara ya kutisha?
 • Vigai wa mawe vya Waashuru vinataja mara na tena kuhusu " ishara ya kutisha" kutoka mwaka wa 763 - kupatwa mwezi. Hili ni kisio tu, ebu tufikiri kwamba hili lilitokea kabla ya kufika kw Yona Ninawili. Je unafikiri iliweza kudhuru vipi mawazo ya watu kule .
 • Je Yona alihitaji kwa ajili ya nini, kama ishara za hatari zilikuwa tayari zimewagopesha watu?

  INJILI: Kisa hiki kinaonyesha kuwa hakuna kisa chochote hapa duniani ambacho ni ambacho hakina matumaini wala mtu wala mji. Kama neno la Mungu linaweza kuvunja miyo ya Waashuru, linaweza kufanya kwa nchi yoyote au kwetu sisi wenyewe, au kwa mtu ambayo unahanghaika juu yake leo.

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  5. MUNGU ALITUMA MTANGONA AND BUU  Yona 4
  UTANGULIZI WA YALIYOMO: Katika mstari wa 2 Yona anasema ukiri wa Imani, ambao ni nukuu kutoka AK. Katika sehemu ile joto linaweza kupanda hadi selisiasi + 50, hasa wakati upepo unavuma kutoka upande wa jangwani. Lija ya haya, Yona aliamua kuka nje ya kuta za Ninawi zaidia ya mwezi mmoja. Mmea katika msataru wa 6 ulikuwa ule ambao unakuwa haraka Zaidi meta nne. Lakini hili halifanyiki kwa kipindi cha usiku mmoja bila muujiza wa Mungu.
  Bwana alibadilisha mipango yake
 • Fikiria njia tofauti tofauti kuwa Bwana alibadilisha mawazo yake juu na Ninawi (3:10-4:1)?
 • Je Yona angewezaje kupatanishwa kulingana na mstari Yona 3:10: "Atakaponena nabii kwa jina la BWANA, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena BWANA; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope." (Kumbu.18:22).
 • Na kama mtu Fulani ambaye anajiita nambii siku hizi anakosea. Kwa maoni yako je mtu huyu nageweza kufanya kama kisa cha Yona au yeye ni nabii wa uongo?
 • Mstari wa 4:2b unatwambiaje juu ya hali nzima/ hatima ya nhci hii na ile ya dunia nzima? Na kazi ya Missioni je?
  Mmisionari akashirika
 • Unafikiri ni kwa nini Bwana wakati mwingine anawaacha watoto wake wapata emajaribu baada ya mafanikio makubwa?
 • Ni nini hasa kilichomfanya Yona akamkashirikie Mungu (4:1-2)?
 • Je unafikiri hasira ya Yona inaeleweka na kusamehewa? Toa sababu zako.
 • Je Yona alitumia mbinu gani kukabiriana na hazira zake?
 • Yona alitaka kufa mara mbili katika malngo huu (4:3,8).Kwa nini alitaka kufa?
 • Je Yona angalijibu vipi maswali ya Mungu (4)?
 • Je unafikiri nini juu ya maelezo/ Hitifaki, kulingana na ambavyo Yona alichnganyikiwa kulinga na hali ya kisaikologia ?
 • Sura hii inasema nini juu ya hazira/mfadhahiko wa wafanyika kazi wa Kanisa/ mtu ambaye anamtumikia Mungu?
 • Kwa nino Yona alienda nje ya mji badala ya kwenda nyumbani (5)?
  Cha msingi
 • Ni nini Zaidi ya joto ambacho kilimfanya hali ya Yona kuwa kuwa ngumu alipokuwa akikaa jangwani ?
 • Yona nasemekana kusikia furaha mara moja tu katika simulizi hili zima katika mstari wa 6. Je ukweli huu unasema nini kumhusu?
 • Unaoneje njia ya Mungu kukbabiriana na YOna kulingana na msitari wa 6-7?
 • Bwana anauliza Yona kwa mara ya pili. Kwa nini (4,9)?
 • Linganisha Yona aliyekuwa katika tumobo la samaki na Yona aliyekaa jangwani. Kuna tofauti gani?
 • Yona ndiye Mmisionari wa pekee katika AK ambaye alitumwa kuwahubiria wapagani. NI kwa njia gani ambayo yeye ni mfano wa wamisionari wote?
  Hitimisho
 • Je mlango wa nne unasena nini juu ya hazira yako?
 • Kama umewahi kusijisikia kana kwamba Mungu anakuvuta kwa kuzudi, ni lini?
 • Ni kuzudi gani ambalo Mungu amekufanya ujisikie angalau vema?
 • Je mfanyikazi wa Kanisa atafanya nini akama atamkashirikia Mungu?
 • Je kuna faraja gani kwetu katika sura ya 4?
  Mwisho
 • Je mistari ya mwisho inatuonyesha nini juu ya tabia ya Mungu (10-11)?
 • Je kuna maana gani ya neno "mnyama" katika mstari wa 11?
 • Ni nini kilifanyika kwa Yona Mungu alipomzungumzia? Fikiria njia mbali mbali.
 • Je Wanaisraeli wa siku za Yona walisema nini waliposikia juu ya safari ya Yona kwenda Ninawi? Na Mfalme Yeroboam II je?
  INJILI: Kitabu cha Yona kinaishia na neema ya Mungu kwa wapagani. Tukitazama katika mistari ya Mwisho tunaweza kuelewa kwamba ni kwa nini alimtuma mwanae duniani. Yona alikuwa sawa alipofikiri kwamba Waashuru wangemeza Israel siku zile au za usoni. Uamsho wa Ninawi uliguza kizazi kimoja tu. Tangu mwaka wa 745 kuendelea, ufalme wa Waashuru ulipiga Israeli ya kaskazini kidogo kidogo. Miongo mine baada ya giza la mwezi (722) ilihabribu Samari na kuchukua mateka kabila tisa na hawakuweza kurudi.
  Mwisho siku ya kiama ya Ninawi ilifika pia. Katika mwaka wa 612 KK, Wabali waliteka mji na kuuteketeza hadi udongo. Makadilio ya Yona ya siku arobaini hayakutimia hadi baada ya miaka 150. Kwa karne nyingi hakuna aliyejua ilikuwa wapi. Si kabla ya 1840 ilipopatika chini ya jangwa karibu na Mosul. Ninawili ilionodka lakini kitabu cha Yona kipo bado. Kama vile Yesu alivyosema,: "Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe." (Luk.21:33).

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  6. ISHARA ZA YONA: MUNGU ALIMTUMA MWANAE  Math.12:38-41 na 16:1-4
  YALIYOMO YA MSINGI: Kastika lugha ya Biblia ishara inaweza kumaanisha mambo mawili: a) Kitu ambacho kinaendana na agano na kutibithisha kuwa mtu fulani au kundi la watu fulani ni wa upande wa Mnug (Sabato, Kutahiliwa, ubatiso). Au inaweza kumaanisha b) muujiza ambayo kwayo Mungu anaonyesha nguvu zake na muujiza ili watu waonen.
 • Kama kuna kipindi Fulani katika maisha yako ambaco ulitaka upate ishara kutoka kwa Mungu, ni kipindi gani?
 • Sema kwa maneno yako: Yesus anajaribu kusema nini kwa Mafarisayo kwa hotuba hizi mbili ndogo?
  Kizazi kilicholaaniwa na chenye usinzi
 • Je Yesu maoni ya Yesu juu ya ukweli wa uamshoa wa Ninawi (41)?
 • Linganisha hatua za watu wa Ninawi kwa kwa mahubiri ya Yona na Mafarisayo juu ya mahubiri ya Yesu. Mbona ni tofauti?
 • Kwa nini unafikiri hisia zetu katika nchi yetu kwa mafundisho ya Yesu ni kam hisia za Mafarisayo na si kama watu wa Ninawi?
 • Mafarisayo walikuwa wameona miujiza mingi ambayo Yesus alitenda. Kwa nini walitaka kuona ishara moja zaidi (12:38 na16:1)?
 • Ni ishara gani pengine inagalitibithisha kuwa Yesu ni mwana wa Mungu?
 • Kwa nini hata ufufuo wa Yesu hakuwazawishi Mafarisayo kuwa Yesu ni mwana wa Mungu?
 • Kwa nini Yesu anajiita kuwa mwenyewe "Kitu kiubwa kuliko Yona"?
  Ishara
 • Ni katika hali gani watu siku hizi utaka ishara, na ni ishara za namna gani wanadai na ni kutoka kwa nani?
 • Ni kwa nini ni hatari wakati mwingine kufanya maamuzi katika mambo makubwa kwa hali ya ishara?
 • Kuna tofauti gani katik ya "ishara ya Yona" na siahra ambazo watu wanataka kupata ili kuimsrisha Imani yao?
 • Je ni kwa njia ipi "ishara ya Yona" ina huruma za Mungu?
 • Je wenzetu wanwezaje kukutana na "ishara ya Yona"?
 • Ni kwa njia ipi ishara ya Yona kwa watu wa Ninawi ina uwepo wa Munug katika mji wao?
 • Ni kwa njia gani Safari ya Yona katika sakafu ya bahari ni mfano wa ubatiso wa Kikristo. Tazama pia Warumi 6:3-5?
 • Ni katika misingi gani tunaweza kuita meza ya Bwana kuwa "Ishara ya Yona""?
 • Kwa mara nyingine: kwa nini Biblia, ubatiso na Meza ya Bwana ni "Ishara ya Yona"?
 • Kwa nini hatuitaji ishara zingine kwa kuimarisha Imani yetu ila "Ishara ya Yona" (16:4)?
 • Kwa nini hukumu ya watu wa Magharibi itakuwa kali kuliko ile ya nchi za wapagani?
 • Tunawezajew kuzaidia kupeleka ishara ya Yona kwa watu wengine iwezavyo hapa ulimwenguni?

  INJILI: Ubatiso wa Kikristo unaambatanisha kifo na kufufuka kwa Yesu (Warumi.6:3-5). Meza ya Bwana inaambatanisha pia. Kifo na kufufufka kwa Yes undo vichwa vikuu katika Biblia nzima. Kama uliuliza kuwa ni jinsi gani utafahamu kuwa Yesu ni Mungu, jibu ni : Tazma ishara ya Yona. Ukiluliza jinsi utakavyofahamu kuwa Yesu anapenda watu wote, jibu ni: tazama ishara ya Yona. Hii ndio maana ishara hii moja inakutosha maishani mwako na hata bila ishara zingine.

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com