MBH JUU ya NOAH

1. Noa ALIJENGA SAFINA Mwanzo 6:5-22
2. GHARIKA Mwanzo 7
3. MWANZO MPYA Mwanzo 8
4. AGANO LA Noa NA DHAMBI YA Noa Mwanzo 9

Print all lessons

? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com


1. Noa ALIJENGA SAFINA Mwanzo 6:5-22



HABARI YA AWALI: Wakati katikati ya Adamu na Noa, mwanadamu aliishi bila sharia ya Mungu. Sheria tu ilikuwa "Amri kuu" ambayo inasema: Katika yote watendee wengine kama vile ungependa wengine wakutendee (Mathayo.7:12 alihitaji kusubiri mda mrefu watoto wakiume wazaliwe zaidi ya wanaume wengine. Tayari alikuwa na umri wa miaka 500 wakatika watoto watatu wa kiume walizaliwa (5:28-32).
6:5-7 na 11-12.
 • Je unafikiri maisha ya kila siku ya ulimwengu yalikuaje akama inavyoelzewa katika mistari ya 5,11 na12?
 • Linganisha kipindi cha Noa na kipindi chetu.
 • Je unafikiri Mungu ameonyeshwaje katika mistari ya 6-7?
 • Je unafikiri watu walikuwa wakatiri, kwa sababy hawakujua amri za Mungu au kwa sababu zingine?
 • Je Wakristo wanawezaje kuondoa wingi wa ukatiri katika siku zetu?
 • Kwa nini Mungu aliamua kuangamiza hata wanayama pamoja na wanadamu (7,13)?
  6:8-10. Katika mstari wa 9 kuna maneno mawili ya Kiebrania kumwelezea Noa : mtakatifu (tsaddik) na bila lawama (tamim). Utakatifu ni neno muhimu katika Biblia. Inamaanisha mtu ambaye amekubalika mbele za Mungu.
 • Soma kwa makini mistari 8-9 na jaribu kupiga picha katika mawazo yako uhusiano wa Noaa na Mungu na kwa majirani zake. Unaweza kusema nini juu yake?
 • Je Noa ni mtakatifu kwa sababu ya Imani yake au matendo yake? Toa sababu zako.
 • Ebu fikiria jinsi Noa aliweza kutunza Imani yake katika ukatiri ule.
 • Je unafikiri watu walifikiri nini juu ya Noa?
  6:13-16. Safina ilikuwa na ukubwa wa mikono 10000 (108000 square feet) katika mazimulizi tatu; ilikuwa kubwa kama vile tanki la mafuta la wakati huu. Kumbuka haya yalitokea kabla ya karne ya chuma. Katika kipindi cha Noa mtu angeweza kupata chuma kutoka kwa mawe na hilo tu.
 • Badilisha vipimo vya safina kwenda katika meta/futi. Je urefu, upana na kina ulihesabiwaje?
 • Je kulikuwa na tofauti gani kati ya meli na safina?
  6:17-22. Waandishi wengine wa agano la Kale wamefikiri mistari ya 5:32, 6:3, 7:6 kwamba Noa aliweza kujenga safina kwa miaka mia moja. Kama hili ni sawa basi hakuwa na watoto wakati alipoanza jenga safina. Lameki babake alikuwa bado hai;; alikufa miaka mitano kabla ya kumalizika safina.
 • Ebu fikiria hatua mbalimbali za ujenzi. Je Noa alipata shida gani hasa?
 • Unfikiri watu walisema nini juu ya mradi wa meli kubwa iliyojengwa katika nchi kavu.
 • Petero anamuita Noa "mtangazaji wa utakatifu" (2.Petero.2:5) na mwandishi wa Waebrania anatwambia kuwa ali "alihukumu ulimwengu kupitia kwa imani yake" (Waebrania 11:7). Hii inamaanisha kuwat Noa aliwahubiria watu wake akiwa anajenga safina. Inawezekanaje luwa hakuna aliye tubu kwa kipindi cham miaka mia moja ?
 • Je unafikiri baba yake Noa na ndugu zake walifikiri nini juu ya mradi huu wa kunjenga safina (5:28-30)?
 • Mke wa Noa je? Je alikumbana na shida gani?
 • Watoto wa Noa walizaliwa wakatika ujenzi wa safina ulikuwa unaendelea. Linganisha miaka yao ya awali na watoto wa lika yao?
 • Ebu fikiria wasichana ambao waliotoka katika familia ambazo si wacha Mungu lakini walikubaliana kuolewa na watoto wa kiume wa Noa. Ni nini kilichowafanya kufanya hivyo? Fikiria uwezekano mbalimbali.
  Hitimisho:
 • Je umepewa kazi gani na Mungu ambayo unahitaji kuwa mwaminifu kama Noa alivyofanya katika kujenga safina?
 • Tunawezaje kuvumilia matusi ya dunia inayotuzunguka pasipo kukata matumaini?

  INJILI:
  Noa alikuwa mtakatifu machoni pa Mungu na aliamini huruma za Mungu. Hakujenga safina ili aweze kuwa matakatifu lakini tayari alikuwa mtakatifu "akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani." (Waebrania 11:7).

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  2. GHARIKA Mwanzo 7



  UJUMBE WA AWALI. Linalofuata ni hitifaki ya Agani Jipya juu ya maisha ya Noa: Kwa imani Noa akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani. (Heb.11:7)
  Mstari wa 1. Hapa Noa kwa mara nyingine anaitwa "mtakatifu" (tsaddik).
 • Je Noa aliamini nini hasa kulingana na Waebrania 11:7?
 • Je Imani na utakatifu vinausianaje kulingana na msatari huu wa Waebrania?
 • Je Imani ya Noa alibadilishaje maisha ya mke wake, wanaye na wakwe zake?
  7:1-5
 • Je unafikiri Noa alijiskiaje aliposikia sauti ya Mungu baada ya ukimya wa miaka mia mojae (2-4)?
 • Je ungefanyaje kama utasikia ghafula tu kuwa kutatokea na balaa kubwa la naman hii lingeikumba dunia (4)?

  7:6-16.
  Wanyama wote walifugwa wakati ule kwa sababu hawakuwindwa wala kuliwa
 • Je unafikiri Noa awawezaje kuwaongoza wanyanyama hawa wote kuingia katika safina katika kipindi cha juama mmoja (2-3, 8-9, 14-16)?
 • Je unafikiri majirani wa Noa wasikiaje walipoona uhamiajia wa ajabu wa wanyama?
 • Familia za wakwe wa Noa hawakuamini Mungu na safina.
 • Je unafikiri wanawake hawa waliingia katika safiana kwa Imani zao au ni kwa sababu ya Imani ya baba mkwe wao? ?
 • Kwa nini Mungu hakutana Noa afunge safina (16b)?
  11-12, 17-24. Dunia pengine ilizungukwa na wingu zito ambalo liliweza kupazuliwa. (Katika tafsiri zingine za Mwanzo2:5-6 anapata hizia hizo.) Yesu analinganisha wakati wa Noa na wakati wa miwsho wa dunia: Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Noa, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 38Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Noa katika safina, 39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.. (Matt.24:38-39).

 • Ni mambo gani ambayo yaliwafutia watu wa wakati wa Noa? Linganisha na watu wa kizazi chetu.
 • Kwa nini tukio hili liliwashangaza wengi japo Noa alihubiri miaka mia mmoja?
 • Ebu fikiri jinsi watu walijaribu kujiokoa na watoto wao wenyewe katika siku za kwanza za (21-23)?
 • Je unafikiri watu wa wakati wa Noa walifikiri nini juu ya mahubiri yake walipokuwa natazamia kufa?
 • Je watu wasio mcha Mungu wa wakati wetu wanaweza kukubali kuwa Wakaristo walikuwa sawa?
 • Je ni mawazo gani pengine waliyokuwa nayo familia ya Noa katika kipindi cha siku arobaini wakati dunia nzima ilijaa maji?
 • Je unafikiri Noa na familia yake walitumiaje mda wao ndani ya safina (24)?
  Petero anandika kama alama ya ubatizo (1.Petero.3:20-21): Katika safina roho nane ziliokolewa kwa maji. N ahili liliashiria ubatizo ambao unakuokoa sasa- si kwa kuosha uchafu wa mwili ila kwa kukubaliwa kwa dhamiri safi kwa Mungu - kwa kufufuka kwa Yesu Kristo.
 • Je kuna uhuziano gani katika ya ubatiso wa Kikristo na safina ya Noa?
 • Je maneo ya Petero yanatuonyesha nini kuwa upatiso ni kitu ambacho Mungu anatutendea kwa huruma zake na wala si yale ambayo tunamfanyia?

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  3. MWANZO MPYA Mwanzo 8



  1-5. Mstari wa 1b unafanana na mistari ya kwanza katika Biblia Takafitu. Neno la Kiebrania "upepo" unaweza kutafsiriwa kuwa "roho". Hakukuwa na ngazi katika safina; ndo sababu kuwa haikwendeshwa/ ujanja. Mtu aingalifikiri kuwa familia ya Noa ingalikuwa katika safina kwa mda wa mwaka mmoja.

 • Ni wangapi katika familia ya Noa waliweza kufahamu kuwa ni wao tu wanadamu waliokuwa katika dunia?
 • Fikiri hali mbali mbali ambazo zilifanya mwaka katika safiana kuwa majaribu ya Imani kwa Noa na familia yake.
 • Ni nini kilichowapa matumani Noa na familia yake?
 • NI majaribu aina gani ambayo yanaweza kulinganishwa na maisha ya Noaru katika safina?
 • Ni miezi mingapi ilipita, safina ilipotwaa juu ya mlima (4, ling. 7:11)?
 • Mlima wa Ararat uko katika mpaka wa Uturuki na Armenia ya siku hizi ambayo inakaliwa na Wakurdi. (Taz. ramani). Haijawahi kutokea katika historia ya binadamu kuweza kufika mahali hapo. Je unafikiri nii juu ya uvumi kuwa imewahi kuoneka meli kubwa ambayo imefunikwa na theluji kwa sehemu?
  6-12
 • Kwa nini haya yaliyoandikwa kwa kina yako katika Biblia?
 • Je Noa alikuwa na sababu gani alipotuma ndege kutoka safina?
 • Je unafikiri kunguru alikaa nje ya safina kabla ya nchi kuwa kavu (4,6,14)?
 • Je wale njia watatu walimwambia nini Noa juu ya hali mbayo nchi ilikuwa inakauka (8-12)?
 • Kwa nini waliweza kusubiri kwa mda wa miezi miwili hata kama mti wa misabibu ulikuwa na matawie.

  13-19
 • Je kulikuwa na tofauti gani katika ya safina iliyo na paa na ile iyokuwa na paa (13)?
 • Je unafikiri ni kitu gani kilikuwa cha ajabu katika wanadamu na wanyama walipofunguliwa kutoka nje baada yam waka mmoja kufungiwa humo (16-17)?
 • Ni nini cha kushanganza juu ya jinsi wanadamu na wanyama waliondoka kutoka safina (18-19)?
 • Ni kwa njia gani kuodonka katika safina ni ishara ya mwisho wa dunia mwanzo wa uumbaji mpya?

  20-22. Mistari hii inanyehs jinsi mwanadamu ana mawazo ya ajabu juu ya wanyama safi (Kwa ajili ya kutoa kafara) hata kabla ya sharia ya Musa haijawekwa. Noa alikuwa amenunua wanyama kundi saba kwa kwa ajili ya Safina (7:2).
 • Kwa nini Noa alitaka kitu cha kwanza kujenga madhabahu kwa Bwana mara tu alipokanyaga katika dunia mbayo uliumba upya (20)?
 • Kwa nini Mungu alitoa ahadi yake aliposikia harufu ya kafara na wala si kabla ya hapo (21)?
 • Je hadi katika mstari wa 21 inamaanisha gani? Tazama pia mwanzo wa mstari wa 22 na 2.Pet.3:7.
 • Linganisha mistari 6:5 na 8:21. Inaonyesha nini juu ya mwanadamu kabla na baada ya anguko?
 • Je ubaya uliokidhiri unajidhihirishaje katika siku zetu?
 • Ni mambo gani ambayo hayabadiliki hadi mwisho wa dunia, bila kujali mabadiliko ya hali ya hewa na vita vya nishati ya nyuklia (21-22)?

  Matumizi:
 • Je kuna ujumbe gani katika somo hili kwa wakati wetu?
 • Ni vitu gani ambavyo vinafanya wanadamu wa siku hizi kuamini hisotira ya mafuriko? (Hata hivyo Yesu aliamiamini juu ya mafuriko...)
 • Ni tendo gani ambalo linazungumza juu ya historia hii kuwa kweli? (Kwa mfano katika upande wa jiologia au maumbile)
  INJILI: Gharika haikufuta dhambi ya asili. Mawazo na mipnago ya mwanadamu zilikuwa za kibinafsi na ubaya hata baada ya gharika nab ado zipo. Lakini kafara ya Noa ilikuwa ni iliashiaria kifo cha Yesu. Damu ilimwagika ili dhambi za mwanadamu zipate kusamahewa na kupata mwanzo mpya.

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com

  4. AGANO LA Noa NA DHAMBI YA Noa Mwanzo 9



  1-4. Uhusiano katika ya mwanadamu na wanyama ulibadilika baada ya gharika.
 • Kwa nini Bwana alisema Baraka kwa familia ya Noa vile alivyosema katika siku ya tano ya uumbaji (1,7, cf. Mwanzo.1:22,28)?
 • Unafikiri ni kwa nini Noa alitaka kupanga upya uhusiano katika wanadamu na wanyama katika hatua hii (2)?
 • Ni nini kingefanyika kama mwanadamu asingalihuhusiwa kula wanyama hadi leo hii (3)?
 • Kwa nini hali ya vita katika ya wanadamu na wanyama katika dunia hii iliyoanguka?
 • Je kuna uhusiano gani juu ya kukatazwa kula damu ingaunganisha kafara katika Agano la Kale and kifo cha Yesu. (4)?
  5-7. Tukikumbuka, ukatatiri ulikuwa umeendelea katika viwango vya juu kabla ya anguko (6:5). Mistari hii inachukuliwa kuwa mwanzo wa mahakama ya dunia.
 • Ni kwa nini si vema kwa jamii kwamba kila mtu afanya anachofikiri kuwa chema?
 • NI kwa nini Mungu lazima awe kiini cha mahakama yoyote - Ni kwa nini mwanadamu hatoshi?
 • Je Mungu anakubalije adhabu ya kifo kwa wauaji?
 • Je Mungu anaonekama kufikiri nini juu ya adhabu ya kifo kwa jumla (Linga..Warumi.13:4)?
 • Je ni mwanga wa aina gani mistari hii unatoa juu ya dhamani ya mwanadamu?
 • Je sharia ya nchi ina mipaka gani juu ya kutoka fanya mabaya na ubaya?
  8-17. Mungu aliahidi kufanya agano na Noa (6:18). Anafanya sasa.
 • Kwa nini Agano katika ya Mungu na uumbaji wake ulihitajika hasa katika hali hii (8-11)?
 • Kwa nini Mungu alitaka kutengeneza Agani kati aya uumbaji wote na wala si wanadamu tu (10)?
 • Kwa nini ni lazima kuepo alama ya kuonekana katika kufanya Agano (12-16)?
 • Je Mungu anaka ufikiri nini, useme, juu ya mabadiliko ya hali ya hewa unapoona upinde wa mvua katika mawingu?
  18-23
 • Je unafikiri nini: Je Noa alifahamu alichokuwa anafanya alipokuwa nakunywa pombe wala hakujua (20-21)?
 • Linganisha Noa ambaye alijenga safina and kuhubiri neno na Noa ambaye anonyeshwa katika mstari wa?
 • NI kwa nini ilikuwa jambo la kuzangasha kwa watoto wa kiume wa Noa kuona uchi wa baba yao (22-23)?
 • Je kuna madhara gani kwa watoto kuona wazazi wao wankunywa pombe?
 • Kwa nini Biblia inanyamaza juu ya dhambi za mashujaa wake?
 • Je Mkristo nahitaji kuhusiana na pombe? (Je nahitaji kuhusiana nayo katika nchi mbayo pombe na ulevi viko kila mahali au ni shida kubwa?)
  24-27. (Unaweza kuacha hili nje kama mda ni mfupi.) Maneno haya yametumika katika kutetea dhidi ya upaguzi, kutenga na kugandanmiza pia utumwa na siasa ya upaguzi wa rangi. Si sahihi, kwa sababu, a) hakuna neno "jamii" katika Biblia nzima na b) miongoni mwa jamii ya kulikuwa na watu weupe na weuzi. Wayahudi na Waarabu ni kizazi cha Shem na Wauropa ni kizazi cha Yapheti.
 • Je unafikiri ni kwa nini laana imeandikwa katika Biblia?
 • Kwa Ulaya na Marekani ya kaskazini wamepoteza Baraka ambayo iliahidiwa kwa Yafethi (27a)?
 • Unafikiri ni kwa nini dini ya Kikristo imashamiri miongoni mwa kizazi cha Ham katika Africa sasa hivi?

  INJILI: Baraka za aina yake kwa zilimaanisha kuwa mwana wa Mungu na Mwokozi wa mwanadamu angezaliwa katika kizazi chake. Lakini katika Yesu dunia nzima alichanguliwa tena kuwa mpeaji wa Injili ya Mungu na Baraka zake. Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; 10wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo. (Ufu.7:9-10).

  ***


  ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com