SEHEMU YA 1. NINI MAANA YAMAFUNDISHO YA BIBLIA KUHUSU HABARI NJEMA?
Shughuli ya Kiinjili
Tunaweza kujifunza kutoka historia ya kanisa kuwa daima kikundi kimekuwa chombo cha kuwafikia wafuasi wapya. Unaweza kumtambulisha Yesu kwa marafiki na jamaa kwa kuanzisha kikundi cha Habari Njema. Kwanza, huwa rahisi kwa watu wengine kuhudhuria mkutano unaofanyiwa nyumbani kuliko kanisani.
Shughuli ya mtu wa kawaida
Kikundi cha Habari Njema huwa rahisi kuongozwa na ni lazima kiongozwe na mtu wa kawaida wala si mchungaji. Hii ndiyo sababu tunaweza kuwa na vikundi kama hivyo katika usharika mmoja.
Kujifunza kwa kugundua
Kwa kuwa washiriki huyajibu maswali, daima wanayagundua mengi kuhusu kifungu/matini husika. Watu hujifunza mengi zaidi ya kuwafaa kwa kuligundua jambo fulani wenyewe kuliko kulisikiliza lile ambalo wengine wameligundua tayari. Haya Mafundisho ya Biblia hukusaidia wewe pia katika usomaji binafsi wako wa Biblia.
Pahali pa kukutana na Yesu
Yesu ni Neno lililofanywa kuwa mwili, kumaanisha kuwa daima tunaweza kukutana naye tunapoifungua Biblia. Lengo la kikundi cha Habari Njema hasa sio tu kufundisha kuhusu Ukiristo bali ni kuwaruhusu watu wakutane na Mwokozi aliye hai. Yesu mwenyewe huzungumza na washiriki wakati wa Mafundisho ya Biblia, huwafariji na kuwasaidia. (Tazama Mt 18:20)
Ushirika wa Wakristo ambapo wasio Wakristo wanakaribishwa pia
Tunapolijadili fungu la Biblia pamoja, jambo fulani pia hutendeka ndani yetu na miongoni mwetu. Mioyo inafunguliwa na matatizo yanagawanwa. Wakati ushirika unakuwa muhimu, watu huwaleta marafiki zao na kikundi kinaanza kukua.
Kuna tofauti gani kati ya Mafundisho ya Biblia ya desturi na ya kikundi cha Habari Njema?
Maneno ”Mafundisho ya Biblia”, yanahusishwa na aina nyingi za mikutano. Wakati mwingine mchungaji huielezea Biblia tu. Kwa kawaida, washiriki wanatarajiwa kuwa na ufahamu wa awali kuhusu Ukristo. Sivyo ilivyo katika kikundi cha Habari njema – maswali kwa mafundisho haya yameandikwa kwa namna fulani ili hata wageni waweze kufahamu asilimia 80% ya maswali hayo. Hii ndiyo sababu yeyote anaweza kushiriki katika majadiliano kwa kuliangalia tu fungu. Washiriki wanaongozwa pia kukitumia kifungu/matini hiyo katika maisha yao wakisaidiwa na maswali. Jambo moja zaidi: katika vikundi vya Habari Njema, hatutafuti ”majibu sahihi” bali tunataka kuwatia moyo washiriki wakiseme wanachokifikiria kuhusu kifungu/matini.
SEHEMU 2. UNAHITAJI NINI ILI KUKIANZISHA KIKUNDI CHA HABARI NJEMA?
Mahali: Mnaweza kukutana katika nyumba za watu, kanisani au chini ya mti.
Viongozi wawili: Kiongozi ayaulizaye maswali na naibu wake amsaidiaye.
Viongozi hawa lazima wapate mafunzo ya Mafundisho ya Biblia kuhusu Habari Njema kabla ya kuianza kazi. Kazi ya Naibu wa Kiongozi ni kusaidia katika majadiliano na kuwaelekeza wachelewao.
Biblia: Katika hali ya kawaida, kila mtu awe na kifungu/matini kutoka kwa injili mkononi. Tafsiri iliyo rahisi lazima iteuliwe kwa ajili ya mafundisho haya. Katika Afrika, lugha nyingi na kutojua kusoma kunasababisha shida. Kiongozi lazima ahakikishe kuwa kila mtu amekisoma/amekisikia kifungu/matini hiyo katika lugha aifahamuyo kabla ya majadiliano kuanza.
Maswali: Kwa kuwa msingi wa Mafundisho ya Biblia kuhusu Habari Njema ni maswali, kiongozi lazima awe na mwongozo wa Mafundisho ya Biblia kuhusu Habari Njema mkononi mwake. Unaweza kuupata kutoka: www.gladtidings-bs.com
Washiriki: Idadi bora ya kikundi ni ya watu 4 - 8. Wakristo na wasio Wakristo wanakaribishwa. Ni rahisi kukijadili kifungu cha Biblia miongoni mwa kikundi cha watu 4 -8 kuliko kikundi kikubwa. Iwapo washiriki zaidi ya 12 wanahudhuria mkutano wako, wagawe katika vikundi viwili ili ukiongoze kikundi kimoja na naibu wako akiongoze kikundi cha pili. Iwapo wengi zaidi wanahudhuria mara kwa mara, uwe na mikutano miwili katika nyumba.
Mapumziko kwa Chai: Kuwapa washiriki chai ni jambo la hiari si la lazima lakini kila kitu sharti kiwe cha kawaida. Mlo uandaliwe tu kabla ya Krismasi au nyakati maalumu.
UNAYAANDAAJE MAFUNDISHO YA BIBLIA?
Kiongozi na naibu wake wayapitie maswali wakiwa pamoja na wahakikishe kuwa wanayaelewa.Viongozi wote wawili wawaombee washiriki.
SEHEMU 3. KIONGOZI AFANYE NINI WAKATI WA MAFUNDISHO?
UTAMBULISHO: Iwapo washiriki hawajuani, anze kwa kuwapa nafasi wajitambulishe.
MAOMBI: Mwombe Yesu awazungumzie washiriki kupitia kifungu/matini. (Iwapo kuna washiriki ambao watakerwa na maombi ya Kikristo, omba kimoyomoyo tu wala si kwa sauti.)
KANUNI: Kiongozi lazima azielezee kanuni tatu za Mafundisho ya Biblia kuhusu Habari Njema (MBHN) ambazo ni: 1) Wakati wa mafundisho haya kiongozi hatayajibu maswali yake. 2) Kiongozi hatasema kuwa jibu fulani si sahihi. 3) Kiongozi atayarejesha majadiliano katika kifungu/matini ikiwa mshiriki fulani ataanza kuyazungumzia mambo yaliyo nje ya kifungu/matini.
KUKISOMA KIFUNGU: Washiriki waisome kifungu/matini kutoka kwa Biblia mara mbili. Iwapo washiriki wanazitumia Biblia zilizoandikwa katika lugha mbili tofauti, kisome kifungu/matini katika lugha zote mbili. Iwapo kuna washiriki wasiozielewa vizuri lugha zote mbili, waelezee kifungu/matini hiyo tena kwa lugha nyepesi.
TAARIFA MUHIMU: Kiongozi azisome taarifa muhimu zilizo mwanzoni mwa maswali na ahakikishe kuwa zinaeleweka.
KUYAULIZA MASWALI: Kiongozi aliulize swali moja moja na alisubiri jibu zaidi ya moja. Swali linatambuliwa kwa * au nambari. Swali lililo katika mabano lazima lisomwe tu iwapo hakuna aliyelijibu swali lililotangulia.
KUYAJIBU MASWALI: Kujibu ni kwa hiari. Usimlazimishe yeyote kulijibu swali. Washiriki wakiinua mikono, usiwape nafasi walio wa kuanza kuuinua mikono bali wasubiri wengine. Iwapo una nakala za ziada za maswali, wapatieni wale ambao wana shida ya kuelewa maana ya maswali.
WATAZAMENI WASHIRIKI: Unapokiongoza kikundi, usizingatie tu maswali. Angalia kinachoendelea miongoni mwa kikundi. Kiongozi akiwa mkweli, wangine watakuwa wakweli pia.
HAKUNA KUANDIKA: Usimruhusu yeyote kuandika katika kikundi cha Habari Njema. Iwapo washiriki wanaandika, wasizungumze.
ZITUNZE SAA: Kikao kimoja kisichukue zaidi ya saa moja na nusu. Mafundisho yakiendelea zaidi, washiriki watachoka na wataacha kuhudhuria. Iwapo kikundi ni cha wanaozungumza sana na majadiliano yanaendelea zaidi na zaidi, kiongozi anaweza kuyaacha maswali mengine. Hata hivyo, asiyaruke maswali ya mwisho kwani hayo ndiyo huwa muhimu zaidi.
MWISHONI MWA HABARI NJEMA: Mwishoni mwa maswali, daima kuna sentensi ya au swali la Habari Njema liwaongozalo washiriki hadi chini ya msalaba. Likiwa swali, kiongozi analisoma mara mbili na anahakikisha kuwa washiriki wameilewa Injili.
MWISHO: Wakati sehemu ya Habari Njema imekwisha, kiongozi anasema: ”Sasa, tafadhali niambieni mmejifunza nini kutoka kwa haya Mafundisho ya Biblia.” Washiriki wote sasa wanatarajiwa kusema jambo. Wapatieni dakika moja kufikiria kwanza. Mwulize mmoja baada ya mwingine.
MAONI YA KIONGOZI YA KUMALIZIA: Hatimaye, wakati umefika kwa kiongozi kusimulia ugunduzi wake. Anaruhusiwa kuhubiri kwa dakika chache ikiwa anataka.
MAOMBI: Mwishoni, kiongozi anamshukuru Mungu kwa Neno lake na anawaombea washiriki kwa matatizo yao ikiwa mambo kama hayo yalizungumziwa wakati wa mafundisho.
UTATHMINI: Iwapo hata mshiriki mmoja aliguswa na upendo wa Yesu, kiongozi anaweza kuhitimisha kuwa mafundisho yalifanikiwa.
Majukumu ya Naibu wa Kiongozi
Naibu wa kiongozi anaruhusiwa kuyajibu maswali.
Anawahudumia wachelewao kwa kuwaonyesha vifungu/matini na kuwaelezea kwa kifupi yale ambayo yamejadiliwa.
Kikundi kinapokua na kinalazimisha kugawanwa katika vikundi viwili, naibu wa kiongozi anakuwa kiongozi wa kikundi kipya.
SEHEMU 4. BAADHI YA SHIDA ANAZOWEZA KUKUMBANA NAZO KIONGOZI
Ufanye nini wakati hakuna anayekisema chochote?
Shida hii ni ya kawaida kwa kikundi kipya wakati wa maswali ya kwanza mawili au matatu. Usibabaike! Washiriki wataanza kuyajibu maswali iwapo wataona kwamba hufanyi hivyo kwa niaba yao. Kwa kawaida, ni kiongozi tu ahisiye kuwa kunyamaza kumeuchukua muda mrefu. Wengine huwa wanafikiria kuhusu kifungu/matini kutika Biblia! Iwapo hakuna anayejibu kabisa, liulize swali lilo hilo tena.
Liulize swali hilo kwa njia tofauti kidogo.
Endelea na swali linalofuatia ikiwa jibu halitatolewa.
Ufanye nini iwapo hulijui jibu kwa swali unaloulizwa na mmoja wa washiriki?
Wahimize washiriki wengine kulijibu. Mshiriki fulani anaweza kuwa analijua usilolijua.
Mwahidi kulijibu mtakapokutana tena - na uitimize ahadi yako.
Unaweza kukubali kuwa hulijui jibu – na uendelee.
Ufanye nini wakati mshiriki fulani analitoa jibu lisilo sahihi?
Usimwambie mshiriki moja kwa moja kuwa amekosea kwa sababu anaweza kuaibika.
Tena waulizeni wengine. Kwa kawaida, mshiriki fulani hulitoa jibu.
Mwulize mshiriki huyo: ”Nini kilichokufanya ufikirie hivyo?” Na itarajiwe kuwa atatambua kuwa kifungu/matini haisemi mambo aliyofikiria inayasema.
Ufanye nini ikiwa mshiriki anatoka nje ya kifungu/matini?
Kuna washiriki ambao daima hufanya hivyo.
Ili kuepukana na shida hii, lazima uzitoe kanuni tatu tangu mwanzo wa mafundisho, mojawapo ikiwa, ”Iwapo utaanza kuyazungumzia mambo mengineyo, nitakurejesha katika kifungu/matini.”
Iwapo mshiriki ataanza kuusimulia uzoefu wake, ambao hauna uhusiano na kifungu/matini, unaweza kusema, ”Hebu tuisikilize hadithi hii hadi mwisho baada ya kuyamaliza maswali (au wakati wa mapumziko ya chai.)”
Ufanye nini iwapo mshiriki fulani ana uzoefu wa kuyatoa majibu marefu sana yanayoyakaribia mahubiri?
Ikiwa una mshiriki kama huyo katika kikundi, sema mwanzoni mwa kila mafundisho, ”Tafadhali yatoe majibu mafupi ili tuweze kuyasikiliza maoni mengi iwezekanavyo!”
Endelea na swali linalofuatia wakati mshiriki huyu atakuwa amekoma kupumua.
Ufanye nini iwapo mshiriki uyo huyo anakuwa wa kwanza kulijibu kila swali?
Katika kila hali, waulizeni wengine wayatoe maoni yao wakati mshiriki huyu atakuwa amemaliza.
Jadiliana naye faraghani kuhusu shida hii.
Ufanye nini iwapo kutokubaliana kutazuka kuhusu jambo fulani la kiimani?
Mara nyingi, hili halitokei katika vifungu/matini za injili, lakini likitokea:
Utoe muhtasari wa mitazamo yote miwili.
Kubali kuwa mmetofautiana na uendelee.
Iwapo jambo hilo ni muhimu sana, basi mwombe mchungaji ahudhurie kikao kitakachofuatia na ulielzee jambo hilo.
Ufanye nini iwapo mmoja wa washiriki hasemi lolote kamwe?
Usimlazimishe kuongea. Jaribu kuchunguza iwapo mshiriki huyu, kwa kweli, anataka kunyamaza. Wale wanaopenda kukaa kimya kwa kawaida hawamtazami kiongozi.
Ufanye nini iwapo nusu ya washiriki wanachelewa?
Ufanye nini iwapo washiriki hawazielewi kanuni za Mafundisho ya Biblia?
Ufanye nini iwapo baadhi ya washiriki hawajui kusoma na kuandika?
Ufanye nini iwapo mtoto atayatatiza majadiliano?
Ufanye nini iwapo mshiriki fulani katika kikundi hazielewi lugha unazozizungumza?
Ni mambo yepi muhimu utakayoyatilia maanani iwapo Mwislamu atahudhuria Mafundisho ya Biblia yako?
SEHEMU 5. KUYAPANGA MAFUNDISHO YA BIBLIA KUHUSU HABARI NJEMA KANISANI
Kamati ya Mafundisho ya Biblia kuhusu Habari Njema kwa kanisa zima.
Mhusishe mchungaji anayehusika na kazi hii. Wanakamati wengine wanaweza kuwa mashemasi, viongozi wa vijana n.k.
Kamati iishughulikie kazi ya utafsiri.
Kamati izipange kozi za mafunzo kokote katika nchi.
Kamati ya Mafundisho ya Biblia kuhusu Habari Njema kwa usharika.
Mchungaji au mfanyakazi yeyote wa kanisa aiongoze timu ya viongozi wa vikundi vya Mafundisho ya Biblia.
Katika mkutano wa kila timu lazima pawe na Mafundisho ya Biblia halisi ambayo viongozi watayaongoza katika vikundi vyao.
Waulizeni viongozi waviongoze vikundi vyao kwa zamu ili uweze kuona kama wanaviongoza sawasawa.
Jadiliananeni shida za kila kikundi.
SEHEMU 6. NAMNA YA KUIENDESHA KOZI YA MAFUNZO
1. Kikao cha Kwanza
Kwanza, waonyesheni mazoea ya Mafundisho ya Biblia. Iwapo kuna zaidi ya washiriki 12, kiteue kikundi cha washiriki nusu na uwe na Mafundisho ya Biblia nacho mbele ya vingine. Kifungu: Mwana Mpotevu (Luka 15:11-24). Washiriki wengine wanaweza kutazama kinachofanyika. Baada ya hayo ifundishe Sehemu 1: Ni nini Mafundisho ya Biblia kuhusu Habari Njema?
2. Kikao cha Pili
Ifundishe Sehemu ya 2 – 3.
Naibu wa kiongozi pamoja nawe myaongoze Mafundisho ya Biblia katika vikundi viwili. Kifungu: Yesu Anamponya Mtu Aliyepooza (Marko 2:1-12). Iwapo kuna wakurufunzi zaidi ya 20, lazima ujiandae na viongozi zaidi waliohitimu kwa kikao hiki.
3. Kikao cha Tatu
Wakurufunzi waziandae seti mbili za maswali katika jozi kwa kukisoma kifungu/matini na kuyapitia maswali. Nusu yao iandae, Mhalifu Msalabani (Luka 23:32-43) na nusu nyingine iandae, Yesu Anamwita Mathayo (Mathayo 9:9). Kisha wale walioandaa Mhalifu Msalabani wayaongoze Mafundisho ya Biblia katika vikundi vya washiriki wanne wanne.
4. Kikao cha Nne
Kisha jozi iliyokiandaa kifungu/matini ile nyingine (Yesu Anamwita Mathayo) kiongoze vikundi vya washiriki wanne. Baada ya hayo uifundishe Sehemu 4. Ifundishe kwanza kwa kuzielezea shida na wakurufunzi wanaweza kupendekeza masuluhisho.
5. Kikao cha Tano
Yafundishe masomo mengine yote na viunde vikundi vitakavyoyaendesha Mafundisho ya Biblia bila matayarisho.
SEHEMU 7. KUYACHAGUA MAANDIKO
Kijitabu cha kwanza lazima kiwe cha Habari Njema kwa Vijana na Habari Njema kwa Waanzishi (= Marko Rahisi). Kitayarishe hicho kijitabu kimoja na daima kitumie kwa vikundi vipya.
Kisha itafsiri Injili ya Marko yote. Baada ya hiyo itafsiri Injili ya Mathayo na ya Yohana. Itafsiri injili moja moja kila mwaka.
Kinyota kimoja * kinamaanisha maswali rahisi, vinyota viwili ** vinamaanisha maswali rahisi kiasi na vinyota vitatu *** vinamaanisha maswali magumu kiasi.
Version for printing
Downloads
Contact us
Webmaster